Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini
Na
Stephano Mango,Songea
MSAFARA
wa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wapigwa mawe na
wananchi waliojitokeza kuzungumzia kero ya daraja la Matarawe ambalo linadaiwa
kusababisha vifo vya watu zaidi ya watatu katika mwezi huu wa octoba mwaka huu
Wananchi
hao wa kata ya Matarawe Manispaa ya Songea,wakiwemo waendesha Pikikipiki
maarufu kwa jina la Yebo Yebo walifunga barabara kwa zaidi ya masaa
mawili na kufanya fujo za kung’oa kingo za daraja pamoja na kuweka
magogo na mawe katikati ya daraja na kuchoma matairi moto ili
Mbunge huyo asipite mpaka atoe majibu ya kina kuhusu daraja
Hali hiyo
ililazimisha Jeshi la polisi kuwatawanya wananchi hao kwa kuwafyatulia mabomu ya machozi
kwa lengo la kuzuia uharibifu zaidi na kuufanya msafara upite wakati ukirudi
kutoka kwenye Mkutano wa hadhara wa Matarawe baada ya kuzuiriwa wakati wa
kwenda na wakati wa kurudi ambapo hadi sasa watu nane wanashikiliwa na Jeshi
hilo kutokana na vurugu hizo.
Tukio
hilo limetokea jana kati ya saa kumi hadi saa kumi na mbili jioni
ambapo wananchi hao wakiwa na hasira walifanya fujo hizo wakiwa na lengo
la kumshinikiza Mbunge wa Jimbo la Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi awasaidie kupanua
daraja la mto Matarawe ambalo ni dogo kwani kwa muda mrefu limekuwa likisababisha ajalli mara
kwa mara katika eneo hilo kutokana na ufinyu wa daraja hilo.
Awali
Mbunge huyo akiwa katika ziara yake ya siku ya pili akitokea mtaa wa
Liumbu kata ya Mletele kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja
na kuzungumza na wananchi akiwa anaelekea kata ya matarawe kwenye mkutano
wa hadhara ndipo alikutana na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo waendesha
piki piki walikuwa wamezuia njia na kusimama njiani ili asikilize kero
zao kutokana na watu kufa mara kwa mara ambapo siku moja kabla ya mbunge huyo
kufanya ziara kuna kijana aliyetambulika kwa jina la Mashaka Nuhu mkazi wa
Matarawe akiwa anaendesha piki piki alitumbukia mtoni na kufariki dunia papo
hapo.
Hata
hivyo Dkt.Nchimbi alilazimika kusimama na kushuka kwenye gari yake akiwa
ameongozana na viongozi mbali mbali wa chama na Serikali akiwemo Mkuu wa
Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ambapo Mbunge huyo aliwapa pole
kwa ajali zinazotokea na kwa watu ambao wamepoteza ndugu zao alizungumza nao na
kuwataka wawe na subira wakati ombi lao linashugulikiwa, majibu ambayo
wanachi hao hawakulizika nayo
“Natoa
pole sana kwa msiba na ajali ambazo zimetokea nimewasikia, na ninaahidi
nitawajengea daraja hili ,kama nimeweza kujenga barabara hii kwa kiwango
cha lami bila maandamano wala kufungiwa barabara nitashindwa daraja? hivi ni
vitu vinavyozungumzika hili ni jambo dogo hivyo naomba twende
kwenye mkutano wa hadhara na tutaongea vizuri zaidi , kwani ni kweli daraja ni
finyu na linahitaji kufanyiwa maboresho zaidi, ‘alisema Dkt. N chimbi.
Dkt.Nchimbi
akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
viwanja vya Shule ya sekondari ya kutwa ya matarawe
amesema,amesikitishwa na tukio hilo kwani tabia hiyo haipendezi ,haikubaliki na
haina maadili na aina
tija kama
wangekuwa na busara wangefika kwenye mkutano na kutoa kero zao badala ya
kufanya fujo ambapo ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka wahusika wa fujo
hizo.
Amesema,
ni kweli daraja hilo ni dogo ila siyo ustarabu kufunga barabara kwa masaa
mawili kwani wamesababisha shughuli mbali mbali za maendeleo kusimama kutokana
na barabara hiyo kufungwa na kwamba tayari ameshamuagiza Mhandisi wa
halmashauri ya Manispaa hiyo kufanya tathmini ili kujua gharama zinazohitajika
ili liweze kupanuliwa.
Mapema
Diwani wa kata ya Matarawe James Makene aliungana na kundi kubwa la wananchi hao
na alimweleza Nchimbi kuwa hiyo ni changamoto ambayo wakazi wa
matarawe wamekuwa wakilia kila mara hivyo wanahitaji msaada wa kupanua
daraja hilo ambalo limeonekana kuwa ni kero ya muda mrefu.
Kwa
upande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki ameeleza kuwa
kufatia vurugu hizo tayari watu nane wanashikiliwa na wanaendelea kuhojiwa
zaidi ili kuwabaini vinara wengine wa fujo waliowashawishi wananchi kufanya
fujo hizo .
MWISHO.