About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, October 2, 2012

WANANCHI WAILALAMIKIA SERIKALI KUCHELEWESHA MAENDELEO

Na Stephano Mango, Tunduru

WANANCHI wa Kijiji cha Kalanje Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameilalamikia Serikali kuwa imekuwa kikwazo cha kupeleka maendeleo kwa wananchi wake.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Barton Chuma wakati akichangia mada ya changamoto za maendeleo vijijini katika kikao cha Wazee kilicho fanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini hapa. Chuma alisema kuwa mbali na kuwepo kwa changamoto kubwa ya wananchi kukataa kujitolea yeye kwa kuwa shirikisha viongozi wa vyama vya Siasa wamefanikiwa kufyatua tofari laki nane zilizopangwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Kijiji chao.

 Alieleza kuwa kinacho washangaza wananchi wa kijiji hicho ni kutopokea Shilingi Milioni 15 ambayo ni asilimia 60% waliyo ahidiwa na Serikali kupitia halmashauri yao ili kuwa wezesha kuanza kwa ujenzi huo. Alisema kufutia hali hiyo wananchi wameanza kupoteza imani kuwa huenda asilimia hiyo 40% ya nguvu zao hizo zikapotea bure na kuendelea kuvunja ari ya wananchi kupenda kujitolea pindi wanapo himizwa kufanya shughuli za maendeleo.

Chuma aliendelea kufafanua kuwa hofu hiyo inatokana na kuanza kwa dalili za kunyesha mvua huku mradi huo ukiwa haujulikani utaanza lini na kwamba endepo fedha hizo zitaendelea kuchelewa ipo hatari ya kuwakosa hata watu wa kusaidia ujenzi katika kipindi hicho ambacho kila mtu huhamia mashambani.

Wakizungumzia vitendo vya jamii kugomea maendeleo kwa madai kuwa kazi zote zinatakiwa kufanywa na Serikali Adam Ausi, Chikambo Mapunda na Eluminata Mdamu walisema kuwa tatizo hili linalelewa na Serikali yenyewe kutokana na kutoa Uhuru wa kuongea uliopitiliza.

Walisema pamoja na kuruhusu vyama vingi ambavyo hivi sasa vinatumiwa kama mwamvuli wa kuficha kundi hilo la wavivu na wapinga maendeleo kama Serikali ikitumia vizuri makali ya Mamlaka iliyopewa vitendo hivyo vilitakiwa kuondolewa kwa kukemewa na kuchukua hatua kwa walengwa bila kujali vyama wanavyo toka.

Akijibu kero hiyo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Wilaya hiyo Rashid Mandoa pamoja na kukiri kuwepo kwake alisema kuwa tayari taratibu za kukamilisha na kuingiza fedha hizo katika akaunti ya kijiji zinaendelea vizuri.

 Alisema Kijiji hicho ambacho kilipangiwa jumla ya Shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, fedha hizo zilikwama kutokana na kuchelewa kufanyika kwa ukaguzi uliotakiwa kufanywa na kamati ya Fedha uongozi na mipango inayo undwa na madiwani wa halmashauri hiyo.

Mandoa aliendelea kufafanua kuwa baada ya kamati hiyo kutembelea eneo la ujenzi na mahali zilipo hifadhiwa tofari Septemba 26 mwaka huu na kujiridhisha tayari kamati hiyo imetoa ruhusa na baraka zote kwa ajili ya kuruhusu fedha hizo.

Nae Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho katika hotuba yake alisisitiza kuwa serikali haita kuwa na mchezo na haita mvumilia mtu yeyote atakaye pita na kuhamasisha wananchi kugoma kujitolea.

 “Sita kuwa tayari kuwavumilia watu wanaopinga maendeleo huku majengo ya taasisi mbali mbali yakiwemo majengo ya Shule za Msingi na sekondari yakiwa Chakavu na mahitaji ya majengo mapya yakiwemo’’ alisema Dc, Nalicho.

Alisema katika kipindi chote cha Uongozi wake atahakikisha kuwa Wilaya yake inapiga hatua za kimaendeleo pamoja na kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinalindwa kwa nguvu zote. Mwisho