About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, February 4, 2015

KICHANGA CHATUPWA CHOONI, MWINGINE ATUMBUKIA KISIMANINA, STEPHANO MANGO,SONGEA

JESHI la polisi mkoni Ruvuma linawasaka wanawake watatu akiwemo mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri kati miaka 20 na 24 mkazi wa eneo la mahenge C manispaa ya Songea  ambaye anadaiwa kutoa  mimba kisha kukitupa kichanga kwenye shimo la choo huku kikiwa kimeviringishwa mfuko wa Rambo.


Akizungumza na Tanzania Daima jana mchana ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:20 mchana huko katika eneo la Mahenge C.


Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio aliopolewa mtoto mchanga anayekadiliwa kuwa na miezi kati 7 na 8 wa jinsia ya kike akiwa amefungwa ndani ya mfuko wa Rambo kwenye shimo la choo ambacho kipo kwenye nyumba inayomilikiwa na Philibert Komba (60) mkazi wa Mbagala jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa mwanamke huyo anayedaiwa kutoa mimba na kutupa kichanga chooni alishirikiana na wanawake wenzake wawili ambao ndio waliomsaidia  kutimiza hadma yake hiyo ya kutupa kichanga na kwamba kwa sasa hivi polisi inawasaka na kwamba wakipatikana watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayo wakabili.

WAKATI huo huo Salah Silenge(10) ambaye  ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi kilimani wilaya ya Songea vijijini amefariki dunia baada kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati alipokuwa akicheza na wenzake.

Alieleza zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya kisima cha maji na askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga walikutwa salah ameshakufa kwa kunywa maji mengi.

MWISHO

Friday, January 30, 2015

NAPE NNAUYE AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUIAMINI CCM MWAKA 2015


NA, STEPHANO MANGO,SONGEA

WANANCHI Wametakiwa Kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi (Ccm) Kuwa Ndicho Chama Pekee Kinachopaswa Kuendelea Kuwaongoza na kutatua Changamoto Zinazowakabili Kuliko Vyama Vingine Vya Siasa Kutokana na Uchanga Wake Pamoja na Sera Zao Kutokukidhi Matakwa ya Wananchi Katika Karne ya sasa

Hayo yalisema Jana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akiwahutubia Mamia ya Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kwenye Mikutano yake Tofauti aliyoifanya Mjini hapa baada ya Maandamano Makubwa yaliyoanza Katika Ofisi ya Ccm Mkoa wa Ruvuma Hadi Kata ya Lizaboni na kufanikiwa kufungua matawi ya chama, miradi mbalimbali ya chama na kuwapatia kadi wanachama wapya

Nnauye Alisema Kuwa Vyama Vingi Vya Siasa Havina dhamira ya Kweli ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo bali Vimekuwa vikipiga Kelele ili viwalaghai Wananchi wapate Uongozi ili wajinufaishe wenyewe binafsi na Vyama Vyao

Alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatarajia Februari Mosi Mwaka Huu kufanya Sherehe ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwake miaka 38 iliyopita katika Sherehe hizo chama kinajivunia utekelezaji wa ahadi zake na maendeleo makubwa yaliyopatikana kwa kipindi chote cha uwepo wake madarakani.

Alieleza kuwa CCM inaendelea kutekeleza ilani yake vizuri na wataendelea kuisimamia Serikali katika kutimiza ahadi za mwaka 2010 na kwamba  maeneo machache yalienda kwa wapinzani kimakosa na kuahidi makosa hayatorudiwa tena katika uchaguzi wa mwaka huu


“ Naomba Niviambie vyama vya Upinzani kuwa kauli mbiu ya Mwaka Huu ya Maadhimisho ya Ccm ni Umoja ni Ushindi, Katiba yetu nchi yetu hivyo chama kimejipanga kuelimisha wananchi namna ya upigaji wa kura katika katiba mpya pia kurudisha maeneo yaliyochukuliwa na vyama vya upinzania katika uchaguzi wa mwaka 2010”.


Alisema kuwa wananchi wana imani kubwa na Ccm hivyo Wapinzani walipanga kwa muda wa miaka mitano na kwamba kodi yao imesha wanapaswa kuondoka kabla hawajafukuzwa na mwenye nyumba kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini
Alifafanua kuwa Mafanikio ya Ccm yametokana na Watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kumesaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.


Alisema pia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi kwani ni lazima tutangulize utumishi wa umma.
Pia aliwataka vijana kuacha kuingia kwenye makundi ya watu watakaowatumia kisiasa na kabla ya kuwashabiki viongozi fulani kuna umuhimu watafute historia za viongozi hao
MWISHO

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA SONGEA AJINYONGA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA


MWANAFUNZI wa Kidatao cha kwanza katika shule ya Sekondari ya msamala iliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma James Mbano (16) amekutwa chumbani kwake alikokuwa analala amejinyonga kwa kutumia kamba aina ya Katani kwa kuifunga kwenye kenchi za paa la nyumba ya Mjomba wake.
 

Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Yahaya Athumani zimesema kuwa tukio hilo limetokea Janua 29 mwaka majira ya saa 1030 za jioni huko katika eneo la Mkuzo Ruwawasi kata ya Msamala manispaa ya Songea.
 

Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio James alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani ambayo ilifungwa kwenye kenchi la paa katika chumba alichokuwa analala ambapo tukio hilo liligunduliwa na mjomba wake Castory Silvesta (37) ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi mfaranyaki.

Alieleza zaidi kuwa Mwalimu Silvesta baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi  cha mjini Songea ambapo baadae timu ya askari wa idara ya upelelezi Mkoa wakiongozana na Dkt. Toka hospitali ya Mkoa Songea walikwenda eneo la tukio na kufanikiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na hakuwa na jerhaa sehemu yeyote ya mwili na kwamba chanzo cha kujinyonga mpaka sasa hakijafahamika na hakuna ujumbe wowote aliouacha marehemu.

MWISHO.

WAZEE SONGEA WAIOMBA SERIKALI WAPATIWE MATIBABU BURE

     Wazee wakiwa kwenye tafakari ya changamoto zao
 
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA

WAZEE wa kata ya Misufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameiomba  serikali iweze kuangalia upya suala la kupata matibabu bure kwa wazee wenye umri kaunzia 60 kwa kuiboresha kwa kuwa sasa imekuwa haionyeshi kama matibabu hayo hutolewa bure kutokana na kushindwa kupata dawa na baadala yake kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa yaliyoko nje yaeneo lahospitali.

Ombi hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya wazee Mfaranyaki  [MMWM] ,Lawrence Mbewe wakati wa mdahalo uliofanyika kata ya Misufini mjini hapo ambao ulikuwa ukijadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee hasa katika upande wa upatikanaji wa matibabu bure ambayo ni sera iliyowekwa na serikali.

Akiongea kwenye mdahalo huo uliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Civil Society la mjini hapo ,Mbewe alisema kuwa licha ya kuwepo kwa sera inayowataka wazee kutibiwa bure lakini bado wanakabiliwa na changamoto za matibabu hayo ikiwemokushindwa kupata dawa na kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya madawa.

Alisema kuwa kama wanakuwa wamepata bahati ya kupata dawa ,hupewa za kutuliza maumivu hasa Panadol na siyo dawa za kutibu ugonjwa wanaosumbuliwa nao jambo ambalo amedai kuwa baadhi ya wazee wengi kushindwa kutibiwa kwa kutokumdu gharama za dawa.

‘’Tunaiomba serikali iweze kuliangalia hili namna ya kutusaidia maana sasa hali ya wazee siyo nzuri maana unaweza ukapokelewa na daktari vizuri lakini unapozidi kuendelea kupata huduma ya matibabu unakuta unaambiwa dawa hakuna labda tukusaidie za kutuliza maumivu Panadol na dawa nyingine ukanunue kwenye maduka ya madawa”alisema mwenyekiti
,Mbewe.

  Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Songea ,Victor Nyenza akitolea ufafanuzi wa sera ya wazee kutibiwa bure kwenye mdahalo huo alisema sera hiyo ilianzishwa mwaka 2015 ya kuzitaka kila  Halmashauri kuhakikisha wazee wanatibiwa bure
Nyenza alisema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni upungufu wa madawa kwenye vituo vya afya na mahospitalini jambo ambalo hufanya wazee wengi kuona hawatendewi haki katika sera inayowataka watibiwe bure.

MWISHOWednesday, January 28, 2015

WAFANYABIASHARA SONGEA WAFUNGA MADUKA YAO KUMLILIA MINJA


NA STEPHANO MANGO, SONGEA.

WAFANYABIASHARA wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kupinga kitendo cha kukamatwa Mwenyekiti wao wa Jumuia ya Wafanyabiashara nchini David Minja na kwamba mgomo huo utadumu mpaka hapo watakapopata uhakika wa usalama wake na si vinginevyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jana Ofisini Kwake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Tawi la Ruvuma Isaya Mbilinyi Mwilamba Alisema Kuwa Tumefunga Maduka tukiwa Tunamtafuta Mwenyekiti wetu Minja kwani hatuna sababu ya kuendelea na biashara zetu wakati Kiongozi kakamatwa na Jeshi la Polisi Nchini

Mwilamba Alisema kuwa Tunasitisha Shughuli mpaka Tujue Hatma ya Kiongozi wetu ambaye Kimsingi ndiye Mtetezi wa Unyonyaji wa Serikali Kupitia Mgongo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hata hivyo Hatufungui Maduka Mpaka Serikali ituambie kwa kina kwanini wamemkamata kiongozi  huyo na endapo wakimuachia sisi tupo Tayari kufungua Maduka

Alifafanua kuwa Kiongozi wetu alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Majadiliano ambayo imeundwa kwa Pamoja Kati ya Wafanyabiashara na TRA yenye lengo la Kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu matumizi ya Mashine za Kietroniki za kulipia Kodi EFD

“Tunaitaka Serikali Izingatia Nia Njema ya kuundwa kwa kamati hiyo ya Majadiliano na itoe taarifa stahiki kwa wafanyabiashara kwani tunapata wasiwasi kuwa kukamatwa kwake kiongozi wetu kunatokana na juhudi za wafanyabiashara kupinga ongezeko la kodi kwa Asilimia mia moja na matumizi ya mashine za EFD” Alisema Mwilamba

Alisema Serikali inapaswa kutumia njia za kidemokrasia kumaliza changamoto zake na sio kutumia nguvu kuzima madai ya msingi ya wafanyabiashara hivyo ni vyema ikasikiliza kilio cha wafanyabiashara ambao kimsingi ndio wachangiaji wakubwa wa kodi za Serikali

Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Ruvuma Kipara Nziku alisema kuwa  serikali imekurupuka kumkamata mwenyekiti wao kwani tayari walishakuwa kwenye mazungumzo na TRA juu ya mashine za EFD na swala la wafanyabiashara kukataa kulipa kodi hivyo ingekuwa vyema kusubili muafka wa majadiliano hayo.

Alisema kuwa  madai ya serikali juu ya mwenyekiti huyo ya kwamba anachochea wafanyabiashara wasinunue mashine za EFD pamoja na wafanyabiashara nchini wakatae kulipa kodi kimsingi hayana mantiki yeyote hivyo ni lazima busara itumike.

Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara mkoani humo kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu kwa kipindi hiki ambacho wamesitisha hutuma hadi hapo hatima ya mwenyekiti wao Minja itakapopatikana.

Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Apili Mbaruku akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema kuwa mgomo wa wafanyabiashara ahuhusiki kabisa na TRA bali jambo hilo linahusika na jeshi la polisi ambalo ndilo linajuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Minja amekamatwa kwa sababu gani.

Hata hivyo Meneja huyo alipohojiwa na waandishi wa habari juu ya athari gani ambazo wanazipata juu ya mgomo huo alisema kuwa kwa sasa ni mapema mno kujuwa hasara kwani TRA wamekuwa wakikadilia mapato ya wafanyabiashara kwa mwaka na sio kwasiku hivyo ni vigumu kuelezea.

Nae kaimu Afisa biashara Mkoa wa Ruvuma Furaha Mwangakala alisema kuwa swala kwa sasa wapo mbioni kumfikishia mku wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ili aweze kutoa kauli ya mwisho ya serikali ya Mkoa.

Katibu mtendaji wa Chemba ya wafanyabiashara ,Kilimo na Viwanda (TCCIA)mkoa wa Ruvuma Philimon Moyo alisema kuwa kwa sasa hana cha kusema kwa sababu jumuia hiyo ya wafanyabiashara mkoani humo imeonesha kutowatambua TCCIA.

Jitihada za kumpata Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ziligonga mwamba baada ya Katibu wake Revokatus Kasimba kuwaambia waandishi kuwa mkuu wa Mkoa yupo kwenye kikao hivyo hataweza kuongea na waandishi wa habari hadi hapo atakapomaliza kikao.

MWISHO.
Monday, January 26, 2015

SABABU ZA MWAKYEMBE KUHAMISHWA WIZARA HIZI

WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE

Na Mwandishi Wetu
Kwa taarifa zilizopatikana ambazo si rasmi saana ni kwamba mpango mahususi wa kumuondoa waziri Mwakyembe kwenye wizara yake ya uchukuzi na kuhamishiwa kwenye wizara nyingine umepangwa na mtoto wa rais bwana Riziwan si yeye peke yake bali na vigogo wengine wakubwa serikalini na wafanyabiashara wakubwa. 

Kuna ushahidi wa kutosha kuwa Riziwan alimsisitiza baba yake kutomrudisha Mwakyembe kwenye wizara hiyo ya uchukuzi kutokana na waziri huyo kuleta usumbufu kwenye biashara za Riziwan,vigogo na wanafaofanya biashara haramu hapa nchini.Kuna wafanyabiashara wengi walikua hawalipi ushuru walikuja kuanza kulipa baada ya waziri Mwakyembe kukamata wizara hiyo.

Mtoto kwa baba hakui kwa minaji hiyo ni dhahiri kuwa baba kamsikiliza mtoto kwa kufuata matakwa ya mtoto.

Saturday, January 24, 2015

NEWFORCE YAGONGA SONGEA , MAJERUHI ATELEKEZWA PERAMIHO

NEWFORCE YAGONGA SONGEA , MAJERUHI ATELEKEZWA PERAMIHO
NA ,GIDEON MWAKANOSYA, SONGEA.

MKAZI wa Matogoro  Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ,Hamis Kinana (20)amelazwa katika Hospital ya  Rufaa ya Misheni Peramiho baada ya kugongwa na  gari la Abiria la Kampuni ya Newforce linalofanya safari zake Songea na Dar-Es salaam na kumsababishia kulazwa katika chumba cha Wagonjwa  Mahutitu [ICU] .

Akiongea na Nipashejana Swalehe Kinana ambaye ni Kaka wa Majeruhi huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 17 mwaka huu majira ya 2:15 jioni katika maeneo ya stendi kuu msamala wakati mdogo wake alipokuwa akirudi Nyumbani akiwa anatokea shambani kwao Mlete.

Kinana ambaye ndiye anayemtunza mdogo wake Hamis Kinana hospitalini hapo  alisema kuwa baada ya gari hilo kufanya tukio hilo liliendelea na safari bila dereva kuchukua hatua zozote dhidi ya mwathirika huyo.
Alisema kuwa wao kama familia walipata taarifa kuwa ndugu yao amegongwa na gari la abiria linalofanya safari zake kutoka ,Songea kwenda Dar es salaam kisha kubebwa na Wasamalia wema hadi Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma na ndugu walipoona hali yake ni mbaya wakaamua kumpeleka katika Hospital ya Rufaa ya Misheni Peramiho ambako amelazwa Chumba Maalum cha Uangalizi kwa Wagonjwa Mahututi [ICU]

“Tangu ndugu yetu Tumlete hapa Hospitalini hatujamuona hata Mfanyakazi yeyote wa Kampuni hiyo ambayo imefanya tukio hilo kufika kumjulia hali jambo ambalo limetusikitisha sana sisi wanafamilia”alisema ,Swalehe
Kwa upande wake Mganga  Muuguzi wa zamu katika Wodi hiyo ,Adili Msanga  alikili kumpokea ,Hamis Kinana akiwa ana Majeraha ya kichwani na Mdomoni ambayo alidai yameonyesha yametokana na ajali na kuwa kulingana na hali yake waliamua kumuweka chumba cha uangalizi Maalumu  [ICU]

Naye kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela Akizungumzia Tukio hilo jana alikili kutokea kwa tukio hilo lililotokea Katika Barabara ya Songea-Njombe na kuhusisha Gari ya Kampuni ya  NewForce yenye namba za Usajiri T.485 CTF ikiwa inaendeshwa na Godwin Boniface Mkazi wa Jijini Dar Es Salaam aina ya Zongtong na Pikipiki yenye Namba za Usajiri MC.287 ADF aina ya Sanlg iliyokuwa inaendeshwa na Hamis Kinana

Msikhela  Alisema kuwa hali ya Majeruhi ni mbaya na amelazwa Katika Hospital ya Rufaa ya Misheni Peramiho  akiendelea kupatiwa Matibabu na Kwamba Dereva wa NewForce  Amekamatwa, amehojiwa na Jarada lake Limepelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  wa Serikali Kanda ya Songea kwa Hatua Zaidi
       MWISHO.


Friday, January 23, 2015

WANAHARAKATI WALALAMIKIA VURUGU ZA MCHINA SONGEA

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KISIWA SPORTS BUS , KISIWA KISIWA

NA, STEPHANO MANGO,SONGEA

WANAHARAKATI wamelalamikia Kitendo cha Raia wa Nchi ya China Zhouguang Zheng  (27)maarufu kwa jina la Dani Johnson Kumpiga na Kumsababishia Maumivu Makali Mfanyabiashara Maarufu Na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Kisiwa Sport,  Kisiwa Kisiwa (40) na kumsababishia Kulazwa Siku Mbili katika Hospital ya Serikali ya Mkoa wa Songea na Wengine wawili walijeruhiwa katika Vurugu hizo

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti na Gazeti Hili jana Walisema kuwa Kitendo hicho ni kibaya sana kwani kimekiuka Sheria za Uraia na Uwekezaji, ingawa pia ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu na kinavuruga amani na Utulivu Miongoni Mwa Jamii

Hamis Abdala Ally alisema kuwa kitendo cha Mwekezaji  huyo wa Kampuni ya Mabasi ya NewForce inayosafirisha Abiria kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam kimevuka mipaka yake ya Uwekezaji na Ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Taratibu

Ally Alisema kuwa ni kosa sana Raia wa Kigeni kwenye Nchi ya Watu kufanya Vurugu na Kusababisha Raia wa Nchi Husika kupata Maumivu Makali katika Mwili wake , kwani kitendo hicho kinaweza Kusababisha chuki na amani kuvurugika miongoni mwa Jamii

Alisema kuwa Tukio hilo linahatarisha uwekezaji wake, ushirikiano uliojengeka kwa kipindi kirefu kwenye jamii husika kwani mahusiano ya Watu yamepungua kutokana na Jambo hilo

“Tunalitaka Jeshi la Polisi Kutenda Haki Katika Jambo Hili la Mchina Kufanya Vurugu na Kusababisha amani kutoweka Katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Songea kwa Zaidi ya Masaa sita na kuongezeka kwa Chuki Miongoni mwa jamii ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Super Feo na NewForce”Alisema Ally

Alieleza kuwa Wananchi wa Songea hatuna utaratibu wa kuwadhuru au kuwanyanyasa Raia wa Kigeni wawapo kwenye Shughuli zao lakini Tumeshangazwa na Mchina Huyu ambaye ameanzisha Utamaduni  Mpya wa Kuwajeruhi Wazawa
Mukhtar Simba Alisema kuwa Wanaruvuma ni watu Waungwana na Wakarimu sana na kwenye Swala la 

Uwekezaji  Kuna Sheria na Taratibu ambazo zinamuongoza Mwekezaji kufanya shughuli zake pia ana mipaka ya uwekezaji wake katika eneo husika
Simba Alisema Tunalaani na kushangaa Kumuona Mwekezaji Huyo bado anaendelea Kutamba Mitaani huku Mwenzake akiendelea na Matibabu ambayo yamesababishwa na Kipigo chake wakati sheria zipo wazi

Akizungumzia Tukio Hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Super Feo Omari Msigwa Alisema kuwa Kitendo alichokifanya Mchina Siku hiyo Cha Kumpiga Msaidizi wake Haruna Msigwa na Kisiwa Kisiwa na Kuifanya Stendi kuwa ni Uwanja wa Vurugu kimemshtua Sana kwani Hakukitegemea katika Sekta ya Usafirishaji Mkoani Ruvuma

Msigwa Alisema kuwa licha ya Jambo hilo kuwa ni Ukiukwaji Mkubwa wa Haki za Binadamu na Sheria za Nchi Lakini pia kimeleta picha mbaya sana Katika Sekta ya Usafirishaji kiujumla kwani Vurugu hizo zimetokea Mbele ya Abiria ambao hawajawahi kuona wala kutarajia vurugu katika Stendi hiyo

Alieleza kuwa Sheria ziko wazi za Uwekezaji na za Kijinai hivyo ni Muhimu Mamlaka zinazohusika kuchukua Hatua Stahiki Katika Jambo hilo kwani kutochukua hatua madhubuti kutasababisha ulipizaji wa Kisasi miongoni mwa Jamii hizo

“Ili Kuepuka chuki hizo ni Vyema Mamlaka zinazohusika Zikatenda Haki kwa Kila Mmoja aliyeenda Kinyume cha Sheria na Taratibu katika Tukio hilo Kwani Kitendo cha Kumpendelea Mtu huku Ukweli wa Jambo ukiwa wazi kitaanzisha utamaduni mbaya ambao utaleta athari nyingi baadaye” Alisema Msigwa

Alieleza zaidi kuwa Siku za Nyuma Kulikuwa na Kampuni Nyingi za Usafirishaji Abiria kama Vile Sabco, Saibaba,Scandnavia,Ottawa, na Nyinginezo lakini hakuna Siku Hata Moja Wafanyakazi wake au Wafanyakazi wa Kampuni nyingine hizo Kupigana lakini leo Mwekezaji wa Kigeni Amempiga Mwekezaji wa Ndani hali ambayo inazua Mashaka sana

Akizungumza na Gazeti hili Nyumbani Kwake Kisiwa Kisiwa alisema kuwa Ni ukweli ulio wazi kuwa nimepigwa tena kipigo Kikali na Mchina hadi kulazwa Siku Mbili kutokana na Maumivu Makali Katika Sehemu mbalimbali za Mwili wangu

Kisiwa Alisema licha ya Kushonwa Nyuzi kumi na nne Mdomoni kutokana na Kipigo bado mwili wangu haujatengamaa na maumivu makali bado nayasikia na sijaanza kufanya kazi zangu za kila siku kama ilivyo ada

Alisema kuwa Mchina huyu amekosa Utu wala aibu Toka anisababishie Maumivu katika Mwili wangu ameshindwa hata kunijulia hali bali yeye amekuwa akiendelea na shughuli zake huku mie nikiendelea kuumwa

Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela  alisema Tukio hilo lilitokea Januari 13 Majira ya Saa 12:10 asubuhi katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi Kilichopo  Msamala Mjini hapa , ambako ilizuka Vurugu kubwa baina ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya  Usafirishaji Abiria ya New  Force na Kampuni ya Super Feo wakigombaniana ratiba ya kuondoa Mabasi yao kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam

Msikhela Alisema kuwa Katika tukio hilo Watu watatu wamejeruhiwa ambao ni Zhouguang Zheng (27) ambaye ni Raia wa China, Danford Thomas (40) Mkazi wa Mfaranyaki na  Abdurabi Kisiwa ambaye pia ni Mkazi wa Mfaranyaki na Mmiliki wa Mabasi ya Kisiwa Sports

Alieleza zaidi kuwa inadaiwa katika vurugu hizo vitu mbalimbali vimepotea zikiwemo Simu mbili aina ya Tecno ambazo thamani yake bado haijafahamika ambazo zilikuwa mali ya Kisiwa, simu moja ya IPhone 5s yenye thamani ya milioni 1.5 pamoja na fedha taslim shilingi milioni nne zimeporwa na watu wasiofahamika ambazo ni mali ya Zhouguang Zheng

Alisema kuwa kufuatia tukio hilo watu 14 wamekamatwa na Kuhojiwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha katika vurugu hizo na wapo nje kwa dhamana na kwamba Jarada la Uchunguzi Limefunguliwa na Kupewa namba SO/IR/ 189/015 Na kwamba upelelezi bado unaendelea kufanywa na kwamba ukikamilika Jarada hilo litapelekwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ili kulifanyia kazi kabla halijaenda Mahakamani
MWISHOThursday, January 22, 2015

WAKAZI WA SONGEA WAVIPONGEZA VYOMBO VYA ULINZIASKARI WA JESHI LA POLISI WAKIWAWEKA CHINI YA ULINZI WAHALIFU

NA,STEPHANO MANGO,SONGEA

SERIKALI kupitia Vyombo Mbalimbali Vya Ulinzi na Usalama Mkoani Ruvuma Imepongezwa kwa Hatua Iliyozichukua za kuwabaini na  Kuhakikisha Mtandao wa Wahalifu wa Mabomu ya Kutegwa ya Kienyeji unasambaratishwa kwa kukamatwa na Vyombo vya dola

Pongezi hizo zimetolewa na Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Songea ambao wamesema kuwa Kitendo cha Kuunasa Mtandao huo kimewafanya wakazi wa Manispaa hiyo Kuondokana na Hofu Iliyokuwa imetanda kufuatia kutokea Matukio Matatu tofauti ya milipuko ya Mabomu

Kwa Upande wake Michael Westi Mkazi wa Bombambili amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na Vyombo Vingine Vya Ulinzi na Usalama kwa Juhudi zilizofanywa za Kuunasa Mtandao huo ambao  ulikuwa unahatarisha Amani na Usalama kwa Wananchi

Westi Alisema kuwa Kukamatwa kwa Mtandao huo Wananchi hao kwa sasa hivi wamekuwa na Utulivu na amani imerejea tena kwa Wakazi wa Manispaa hiyo hivyo Vyombo vya Dola vinapaswa kuendelea kufanya kazi zaidi ya kuwabaini wahalifu katika maeneo yote Mkoani Ruvuma hasa Ukizingatia kuwa Mkoa wa Ruvuma upo Mpakani mwa Msumbiji na Malawi

Selestini Komba Mkazi wa Mfaranyaki ameiomba Serikali Mkoani Ruvuma Kuona Umuhimu wa Kufanya Misako ya Mara kwa Mara katika Maeneo Mbalimbali yenye lengo la kuwabaini Waharifu ambao walishaanza kuleta hofu kwenye maeneo mengi

Jonas John Mkazi wa Majengo Manispaa ya Songea alisema kuwa ni vyema Wananchi  Katika Maeneo MBlimbali Mkoani humo wawe wanaonyesha Ushirikiano na Vyombo vya Dola Na Kama Kuna Mtu wanakuwa na Mashaka naye sio vibaya kutoa Taarifa kwenye vyombo husika ili akamatwe na ahojiwe

Alifafanua zaidi kuwa Wamiliki wa Nyumba wajitahidi kuweka utaratibu wa kuwatambua wapangaji wao na shughuli wanazo fanya na sio vinginevyo na Serikali ione umuhimu wa kuwa na daftari la Wakazi wa eneo husika ili kuwabaini wakazi ambao sio Raia wema

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mwambungu aliiambia Tanzania Daima kuwa Matukio hayo matatu ya Mabomu yaliyotokea Songea yalimfanya atumie muda kufikiria njia gani sahihi ya kuwadhibiti wahalifu hao

Mwambungu alieleza zaidi kuwa pamoja na jitihada kubwa  ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini walifanikiwa kugundua kuwa Matukio yote Matatu ya Mabomu yaliyotokea Mjini Songea yalikuwa ni ya Kigaidi na Kwamba kwa sasa hivi Mtandao wote umeshabainika hivyo amewataka wananchi waondoe hofu ambayo ilikuwa imetenda miongoni mwao
MWISHOMonday, January 19, 2015

AFARIKI AKIFANYA MAPENZI SONGEA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela Akizungumza Jambo

NA,STEPHANO MANGO,SONGEA.

John Haule (35)Mkazi wa Lupapila Manispaa ya Songea amefariki Dunia ghafla wakati akifanya mapenzi nyumbani kwa mpenzi wake jina linahifadhiwa (winifrida Ndalama-35).

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 17 mwaka huu majira ya saa 8 usiku huko katika kijiji cha Subira manispaa ya Songea.

Alisema kuwa siku ya tukio Haule alienda nyumbani kwa mpenzi wake majira ya saa 2 usiku akitokea hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alikwenda kwaajiri ya kumuuguza mjomba wake na alipokuwa hospitali alimuaga mjomba wake kuwa amemkumbuka mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi  11.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kwa mjomba wake alimruhusu kurudi nyumbani lakini Haule akufika nyumbani kwake badala yake alipitiliza hadi nyumbani kwa mpenzi wake ambapo alipofika aliandaliwa chakula lakini marehemu alikataa chakula hicho kwa madai kuwa ameshakula alikotoka hivyo ilipofika majira ya saa 3 usiku waliingia chumbani kulala na kushiriki tendo la ndoa mpaka majira ya saa 5 usiku ambapo walipumzika huku wakijadili mahusiano yao.

Alisema kuwa ilipofika majira ya saa 8 usiku Haule ambaye ni marehemu alimuomba mpenzi wake warudie tena tendo la ndoa ambapo mpenzi wake alikataa akidai kuwa amechoka lakini baada ya kumlazimisha alikubali ndipo akiwa kwenye tendo hilo Haule alisikika akitoasauti ya kukoroma na kuanza kutetemeka jambo ambalo lilimshtua mpenzi wake huyo ambye alichukuwa jukumu la kwenda kuwaita majirani zake pamoja na mjumbe wa serikali ya mtaa Winney Mwingira ambaye naye alitoa taarifa katika kituo kikubwa cha polisi cha mjini Songea.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa walienda eneo la tukio wakiwa wameongozana na Dkt. Ambaye alithibitisha kuwa Haule ameshafariki Dunia na kwamba jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa upepelezi .
 
MWISHO.

NAPE AWAPIGA MKWARA WAGOMBEA URAIS 2015

 . Asema wanapoteza muda na pesa zao
>. Awataka wakumbuke salaam za mwaka mpya 2015 za CCM.
>. Ajivunia uzoefu wa CCM kudhibiti wasio waadilifu
>. Atamba CCM kufanya vizuri uchaguzi mkuu 2015.
>. Awataka Watanzania kuiombea nchi ipate kiongozi mwadilifu.
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali wa vikao husika.

Nape ameyasema hayo jana kwenye  mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii.


Pamoja na Nape ambaye aliwakilisha CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama vingine vya upinzani nchini.


Akizungumzia mada ya nafasi na uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa taifa.


Nape alisema CCM ipo kila kona ya nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo ndio moja ya siri za uimara wa CCM.


Akizungumzia swala la maadili Nape alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.


Alisema Nape kuwa wasaka urais wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.


Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni kukaribisha laana kwa nchi.


" Nawahakikishia kuwa hakuna mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii" alisisitiza Nape.


Nape alisema mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM  Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.


Anasema Nape hakuna atakayeingia madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa laana kwa nchi.


Semina hiyo inayofanyika Kibaha mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini Kenya.

HABARI KAIKA PICHA
 MTUME na Nabii wa Kanisa la EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.

WAPIGA KURA NAMTUMBO WATAKIWA KUMFANYIA TATHIMINI MBUNGE WAO
                                             MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO VITA KAWAWA

NA, STEPHANO MANGO,NAMTUMBO

WAPIGA KURA  wa Jimbo La Namtumbo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Wametakiwa Kumfanyia Tathimini Mbunge wao  Vita Kawawa Waliomchagua  katika vipindi viwili Mfululizo Mwaka 2005 na Mwaka 2010 kama ametekeleza vyema Ilani ya Chama chake na Ahadi alizozitoa wakati anaomba kura katika Chaguzi mbili hizo

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini hapa Jana Afisa Elimu Mstaafu na Mfanyabiashara Ally Mbawala Alisema kuwa Mwaka huu ni Mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni fursa Muhimu Sana kwa Wananchi kuchukua tafakari Stahiki ya utendaji Kazi wa Wawakilishi wao waliowachagua vipindi vilivyopita na Kuwahukumu katika sanduku la kura

Mbawala Alisema Kuwa Kipindi hiki sio cha kufanya mchezo ni kipindi cha kujitendea haki kwa Kuangalia utatuzi wa Changamoto zilizokuwepo kabla ya kumchagua Kiongozi husika hadi leo ili kujiridhisha utendaji kazi wake na kama anataka kugombea tena basi ahukumiwe kwa mujibu wa kipimo chake cha utendaji Kazi

Alisema kuwa Jimbo la Namtumbo lina Fursa Nyingi  sana za Kimaendeleo kwani kuna ardhi nzuri, Misitu, Madini , Mbuga za Wanyama na Maliasili zingine nyingi na wananchi wake ni wakulima wazuri wa mazao mbalimbali ya chakula , hivyo ni muhimu kupima kama rasilimali hizo zimeweza kusimamiwa na kutumika vizuri na kama zimewezesha kuinua maisha ya wakazi wa Jimbo hilo

Alieleza Kuwa Jimbo hilo ndilo ambalo lilikuwa Maarufu kwa Kilimo Cha Tumbaku na Mbunge wa Jimbo hilo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania hivyo ni vyema  tukamtafakari kwa kina kama  ameweza kushiriki kikamilifu kufufua vyama vya Ushirika na kukuza zao hilo ambalo ndilo zao kubwa la kiuchumi kwa Wakazi wa Namtumbo

Alifafanua kuwa kabla ya uchaguzi ni muhimu sana Wapiga Kura wa Jimbo hilo wakawa na vipaumbele vyao vya Kimaendeleo ili waweze kutengeneza ajenda ya pamoja badala ya kusubiri ilani za Vyama au matakwa ya Mbunge ambayo kimsingi hayana tija katika maisha yao

“Mimi ni Mzaliwa wa Namtumbo lakini kila Siku Maisha ya Wakazi Wa Jimbo hili yanazidi kuwa magumu kwa sababu mbalimbali hali ambayo ina hatarisha amani na utulivu katika jamii kwani kundi la walionacho wanaendelea kunufaika huku kundi kubwa la wasio nacho wakiendelea kuhangaika”

Alieleza zaidi kuwa  hadi leo bado kuna Wakazi wa Jimbo hilo hawajafikiwa na huduma za Maji Safi Na Salama, Elimu,  Afya, Miundombinu, huduma za kiuchumi na Mawasiliano hali ambayo inaendelea kuwafanya wawe masikini zaidi
MWISHO