About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, July 5, 2012

CHADEMA WAISHUKIA ZIARA YA PINDA MKOANI RUVUMA

 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime akiwahutubia mamia ya wananchi jana (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Soko la Samaki la Zamani
 Kutoka kushoto ni Katibu wa Wanawake Jimbo la Songea Asia Ngonyani, Mwenyekiti wa Wanawake Jimbo la Songea na Diwani wa Vitimaalum Chadema Manispaa ya Songea Rhoda Komba na watatu ni mwanachama wa chama hicho Kudeka
 Wananchi wakisikiliza mkutano huo jana


 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime akimvua gamba mwanachama wa CCM Kaumeme kwenye mkutano wa jana
 Wapenzi wa kumbukumbu wakichukua tukio hilo jana la KAUMEME kujiunga na Chadema
Na Mwandishi Wetu, Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Ruvuma kimemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufanya ziara yenye maslahi kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma na Taifa kiujumla badala ya kufanya ziara ya kuliingizia Taifa hasara kubwa

Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Soko la Samaki la Zamani mjini hapa

Fuime alisema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kufanya ziara ya siku mbili kuanzia julai 6 hadi julai 7 katika mkoa wa Ruvuma yenye lengo la kupokea taarifa ya Mkoa ya shughuli za Maendeleo na kupokea taarifa ya maendeleo ya Chama Tawala

Alisema kuwa julai 7 mwaka huu ataenda Kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea na kupokea taarifa ya shamba na kukagua maandalizi ya kilimo cha kahawa,pia atakagua maandalizi ya ununuzi wa mahindi msimu wa 2012/2013 katika hifadhi ya Taifa ya NFRA-Ruhuwiko na baada ya hapo atazindua kampeni ya kimkoa ya matumizi ya matrekta makubwa ya kilimo

Alieleza kuwa Waziri Mkuu ni kiongozi mkubwa sana katika nchi yetu hivyo pamoja na kufanya ziara hiyo ambayo kimsingi haina tija kwa wakazi wa Ruvuma zaidi ya maslahi ya watu wachache wenye makampuni

Alifafanua kuwa mkoa wa Ruvuma ni umeathilika kwa matumizi ya mbolea zilizokosa ubora na ripoti zipo wazi kutokana na utafiti uliofanyika, hakuna umeme wa uhakika, wananchi hawanufaiki na uchimbaji wa Uraniam Namtumbo, Makaa ya Mawe Mbinga na rasilimali zingine

Alieleza zaidi kuwa Wilaya ya Songea kulikuwa na kiwanda cha kusindika Tumbaku lakini kilihamishwa kihuni na kupelekwa mkoani Morogoro, jambo ambalo linaendelea kuwaumiza wananchi kutokana na kuwa na mzunguko mdogo wa fedha katika mji wa Songea

Alisema kuwa Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda haitakuwa na maana yoyote ile kwa wakazi wa Ruvuma kama hata tatua matatizo makubwa ya wananchi kuhusu mbolea, umeme,ajira kwa wakazi wa Ruvuma katika migodi na kero zingine

Alisema kuwa Chadema mkoa wa Ruvuma kinamtaka Waziri Mkuu kuacha kulalamika na badala yake kuchukua hatua madhubuti ya kuiagiza Shirika la Viwango Nchini (Tbs) kuchunguza ubora wa mbolea ambazo zinauzwa mkoani Ruvuma kwa sababu zimeleta kiama kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma

Alieleza zaidi kuwa Chadema kinamtaka Pinda atoe kauli kuhusu kiwanda cha Tumbaku cha Samcu, ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Namtumbo hadi Tunduru kwani mkandarasi yule ameonyesha wazi kushindwa kazi,pia tunamtaka atoe kauli kuhusu uharibifu mkubwa wa uwanja wa Majimaji na Uwanja wa Zimanimoto kwani bila kufanya hivyo ziara yake haitakuwa na tija kwa wazazi wa Ruvuma

Alisema ziara ya Waziri mkuu inatumia gharama kubwa sana ambazo zinatokana na kodi ya wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kuzilipa kodi hizo hivyo matumizi yake ni lazima yawe yenye maslahi kwa wananchi wenyewe ndio maana chadema kwa kuwa ni chama ambacho kinapigania wanyonge na kinatetea ufujaji wa fedha za walipa kodi hivyo ni lazima tutoe maagizo kwa waziri mkuu na tunamtakaayatekeleza maagizo hayo kikamilifu

Awali Katibu wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Dorphin Ghazia alisema kuwa Viongozi wa Serikali wamekuwa wakitumia fedha nyingi za walipa kodi bila kujali maslahi ya wananchi hivyo wananchi wanatakiwa wawe makini katika uchaguzi ujao ili kuweza kupata viongozi wenye mipango madhubuti kwa maendeleo ya wananchi

Ghazia alisema kuwa Chadema ni fursa ambayo watanzania wanapaswa kuitumia ili kuweza kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa chama cha Mapinduzi ambacho miaka zaidi ya 50 sasa toka tupate uhuru bado wananchi wana mahangaiko makubwa
MWISHO