Ni jengo la Utawala ambalo ni Ofisi ya Ubaya Suleiman Salum ambaye ndiye Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Songea
HALI
TETE CHUO CHA UALIMU SONGEA, WIZARA YA ELIMU YAMBEBA MKUU WA CHUO.
Na, Stephano Mango,
Songea
Ni takribani miezi
nane sasa tangu nianze kufuatilia uendeshaji wa chuo cha Ualimu Songea kama
kinaweza kuendana na kauli mbiu ya sasa ya Serikali ya Big Result Now (Matokeo
Makubwa Sasa)
Nimelazimika
kukifuatilia Chuo hicho kutokana na mgogoro mkubwa uliopo kati ya wafanyakazi
(wakufunzi) na mkuu wao wa chuo Ubaya Suleiman.
Mgogoro huo umetokana
na uongozi mbovu usiozingatia misingi ya uongozi na Demokrasia katika vyuo vya
ualimu Tanzania kwani Mkuu huyo wa chuo amekuwa na lugha za matusi,vitisho kwa
wafanyakazi na wanachuo, kutopokea ushauri kwa washauri wake, mbinafsi,
kutowaamini watendaji wake kwa nafasi alizowateua, kufanya kazi kwa kutumia vyanzo
visivyo rasmi, Matumizi mabaya ya fedha za Serikali na vyombo vya usafiri
Pamoja na hayo mkuu
huyo wa chuo amediriki kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi wake kwenye vyombo vya
dola (polisi) (kuwatishia) akiwatuhumu kuwa wanataka kumuua. Baada ya mgogoro huo
kutopata suluhu kupitia vikao vya ndani, Jitihada zifuatazo zilifanyika na
wafanyakazi wa chuo hicho ili kuleta hali ya amani na utulivu wa chuo;
Tarehe 27/04/2013
walifanya kikao na mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti, tarehe 15/05/2013
na tarehe 01/06/2013 walifanya kikao na Bodi ya ushauri ya Chuo, hata hivyo
suluhu ya mgogoro huo haikupatikana.
Kutokana na hali hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome aliunda
tume ya watu watano ikiongozwa na Mkaguzi Mkuu wa shule na vyuo wa nyanda za
juu kusini ambaye alifahamika kwa jina moja la Lyapambile, kuja kufanya utafiti
wa chanzo cha mgogoro, lakini mpaka sasa tume hiyo haijatoa majibu ya uchunguzi
wa jambo hilo
Tume hiyo haikuishia
hapo tarehe 13/08/2013 wafanyakazi walifanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu, ambaye baada ya kusikiliza mgogoro huo aliahidi kuleta suluhisho la
kudumu mapema iwezekanavyo ili kuleta amani na utulivu(peace and Tranquility)
chuoni hapo.
Lakini cha kushangaza hadi sasa yapata miezi mitatu hakuna
kilichofanyika hali ambayo imeendelea kuwavunja moyo wafanyakazi wa chuo hicho.
Licha ya jitihada
zilizofanywa, Mkuu huyo wa Chuo Ubaya Suleiman anaendelea kuwanyanyasa
wafanyakazi wake na kusema pigeni kelele lakini wakuning’oa mimi hapa hayupo na
lugha zingine ambazo sio za ustaarabu anazitoa, na kuwafanya wafanyakazi
wenzake wahoji nguvu aliyonayo katika utendaji, mfano wa lugha zake mbovu ni “kwani
mizizi yangu ni mirefu”. Kitendo hicho kinawafanya wafanyakazi wa chuo na wadau
wengine watilie mashaka juu ya sifa za uteuzi wake kushika nafasi kubwa kama
hiyo.
Tunamuomba Waziri wa
Elimu na mafunzo ya ufundi Shukuru Kawambwa na Naibu wake Philipo Mulugo
kumuondoa mkuu huyo wa chuo madarakani na kumtafutia shughuli nyingine ya
kufanya kwa ustawi wa chuo cha ualimu songea, taaluma ya ualimu Tanzania na ili
kuleta ufanisi wa kauli mbiu ya serikali ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now)
Sababu zinazopelekea
hilo ni nyingi ila kwa sasa nitazitaja chache ili kuweka kumbukumbu sawa, ya
kwanza Novemba 1, 2013 Mkuu huyo wa chuo bila kuwasiliana na Mtaaluma wake wa
Chuo Maiko Luoga, alidiriki kuwaandikia Barua Wakufunzi kuwataka watunge
Mtihani wa Moko wa Ualimu viwango vya Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA) kwa
lugha ya kejeri hali ambayo imesababisha maudhi na utulivu wa akili miongoni
mwa wafanyakazi katika kufanikisha utungaji wa mitihani hiyo
Kitendo
hicho licha ya kuwa ni kinyume na utawala bora , lakini pia kimekiuka maagizo
ya Bodi ya Chuo ambayo yalitolewa tarehe 28/8/2013 (……. mambo yote yanayohusu
fedha yaendeshwe kwa uwazi na ushirikishwaji mkubwa miongoni mwa wanaidara /
taasisi kwani inaonekana mambo yanaenda kwa usiri mno).
Sababu ya pili
amekuwa na vitisho vingi katika utendaji wake na maneno ya kuudhi dhidi ya
viongozi wenzake , mfano wa maneno yake ambayo anayatamka huku akigonga meza
kuashiria ubabe na kiburi cha madaraka ni kama vile,(…. Ukiingia ndani ya kumi na nane zangu nakumaliza,
Angalieni msije mkaumia wengine tunambavu za chuma, Nipo tayari kuua inzi
kwenye kioo cha TV hata kama itavunjika potelea mbalimbali raha yangu ni
kuhakikisha inzi amekufa, Mkitoboa mtumbwi nitahakikisha kabla sijazama mimi
nawazamisha ninyi kwanza, Angalia wengine watakaanga mbuyu na kuwaachia wenye
meno watafune, Amekuwa akitishia kung’oa mtu kwa kumwendea (kumpandia)wizarani
ndani ya siku mbili na kumchukulia barua ya uhamisho kwenda vyuo vya pembezoni
mwa Tanzania, Mimi nafanya haya hata niking’olewa kwa muda mfupi potelea pote
nitakuwa nimejenga historia)
Sababu ya tatu ni kutokuwa na uwazi, ukweli na ushirikishwaji kwa njia
ya kidemokrasia miongoni mwa idara zake katika chuo hicho na hasa katika fedha
ambazo zinakuja kwa ajiri ya manunuzi ya vitu mbalimbali, fedha ya kuendeshea
mafunzo ya ualimu kwa vitendo(BTP)
Fedha hiyo licha ya kuchelewesha kuitoa kutokana na ufisadi wake
lakini pia hakuitoa yote na wala hakueleza kwa uwazi na ukweli, hali ambayo
haikuwezesha wakufunzi kwenda kufanya
kazi stahiki kwenye maeneo kusudiwa ya kuwatahini wanachuo ambao walikwenda kwenye
shule mbalimbali kwa ajili ya mazoezi ya kufundisha kwa vitendo.
Sababu ya nne ni uwezo wake wa kiuongozi kwani kumekuwepo na mashaka
mengi katika Wasifu wake wa kielimu na kiutendaji, hali inayopelekea kuendesha
Chuo katika misingi binafsi bila kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu za
Wizara.
Kutokana na hayo yote Chuo hicho kimejikuta kikiingia kwenye mgogoro
wa muda mrefu na mkubwa na kupelekea shughuli zote za kiutendaji chuoni hapo
kutofanyika katika viwango vyenye ubora na kwa wakati na hasa pale anaposafiri
mambo huwa yanasimama, kwani mara nyingi utendaji wote anaufanya yeye mwenyewe
na wakati mwingine huwa anajiita Chief Accountant na kumuona Makamu wake kuwa
hana uwezo wala mamlaka ya kutoa maamuzi kwa mustakabali wa chuo
Ni mengi ambayo nimeyabaini na ushaidi upo wazi kuwa Mkuu huyo wa Chuo
hafai kuendelea kuongoza Chuo hicho kwani Wakufunzi, Wafanyakazi na Wanachuo
hawana imani nae, na wanafanya mambo mengi bila morari ya utendaji kutokana na
mazingira mabovu ya utendaji kazi katika chuo hicho
Nimefanya jitihada za kukutana na baadhi ya Wakuu wa Idara Chuoni hapo
na kupata majibu ambayo yanaonyesha ukataji wa tamaa kutokana na mazingira
mabovu ya kiutawala ambayo yanaonyeshwa na Mkuu wa Chuo hicho katika
kufanikisha mpango mkakati wa matokeo makubwa sasa,
Pia nimebahatika kuwauliza viongozi wa Bodi akiwemu Kaimu Mwenyekiti
wa Bodi ya Chuo ambaye amejitambulisha kwa jina la H,Lugome naye pia ameonyesha
masikitiko makubwa sana juu ya utendaji wa Mkuu wa Chuo hicho
Lakini pia Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti ambaye pia
ameshiriki kusuluhisha mgogoro huo katika kikao chake cha April 27, 2013 lakini
ameshindwa na kukata rufaa kwa kulipeleka swala hilo kwa Mkuu wa Mkoa ili aweze
kuliingilia kati
Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Philipo Mulugo alipo tafutwa
kupitia simu yake ye kiganjani yenye namba
hii 0754315922 alijibu kuwa swala hilo bado halijafika mezani kwake na
endapo likifika basi atachukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria dhidi ya
Mkuu yoyote wa Chuo ambaye atakwamisha malengo na ufanisi wa kazi nchini
Kutokana na hayo na mengine mengi ni dhahiri kuwa utendaji wa kazi
katika chuo cha Ualimu Songea kilichopo
eneo la Matogoro Mkoani Ruvuma wilayani Songea ni mgumu miongoni mwa
Wafanyakazi na kusababisha hali ya sintofahamu katika Saikolojia zao na
mustakabali wa Elimu ya wanachuo
Ni vema sasa mamlaka zinazohusika zikachukua hatua stahiki za kumaliza
mgogoro huo ikiwemo na kumuondoa Mkuu huyo wa Chuo ili kurudisha Amani na
Utulivu chuoni hapo miongoni mwa wanajumuia wanaokizunguka chuo hicho ili
kuweza kufanikisha mikakati mbalimbali iliyopo nchini ya kuhakikisha kuwa elimu
bora inafikiwa nchini hapa
Mwandishi wa Makala hii
Anapatika kwa 0755-335051 AU 0715-335051
Barua pepe,stephano12mango@yahoo.com
www.stephanomango.blogspot.com
Uongozi wa sasa sio shuruti bali ni kushauriana na unaowangoza
ReplyDeletenikimuona huyo Ubaya nitamcheka kwa ujinga wake, hao wanaompa kiburi nao ni kuwanyonga hadharani
ReplyDeletenimesoma ualimu pale. Mwaka wetu alifukuza watu na wengine tulipigwa suspesion ya hatari December 2011
ReplyDeletenimesoma ualimu pale. Mwaka wetu alifukuza watu na wengine tulipigwa suspesion ya hatari December 2011
ReplyDeleteMnazingua.
ReplyDeleteMnazingua.
ReplyDelete