Waandishi wa habari wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali katika kikao cha waandishi wa habari na Waziri Dkt Nchimbi
Waziri Dkt Nchimbi aliyekaa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Waliokaa kutoka kushoto Charles Mhagama(Anayedaiwa kuwa Mstahiki Meya),Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Dkt Nchimbi,Endre w Kuchonjoma(Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club),Waliosimama kutoka kulia Nathan Mtega(Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Ruvuma),Endrew Chatwanga(Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini),Gerson Msigwa(TBC),Emmanuel Msigwa(Channel Ten) Ngaiyona Nkondora(Star Tv na Redio Free) Juma Nyumayo(Uhuru Fm) Alpius Mchucha(HabariLeo)Stephano Mango(Dira ya Mtanzania) Amon Mtega(Mtanzania) Joseph Mwambije(Majira) Anuciata Ngatunga(Ps wa Dkt Nchimbi)Cresencia Kapinga(Majira) Meja Mgumba(Msaidizi wa Waziri) Joyce Joliga(Mwananchi) Naftan Saiyoloi(Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la kudaiwa kukimbia na sanduku la kura kabla ya kudhibitiwa na Madiwani wa Chadema juzi katika uchaguzi wa nafasi wazi ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Akisoma tamko lake katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea alisema kuwa amesikitishwa na vyombo vya habari,magazeti ya Tanzania Daima,Majira na Mwananchi vilivyolipoti habari hiyo iliyojaa upotoshaji mkubwa
Dkt Nchimbi amevitaka vyombo hivyo kukanusha na kumuomba radhi katika matoleo yao ya Septemba 26 katika ukulasa wa mbele kwani vimemshushia hadhi yake katika jamii na kumjengea misingi ya ukosefu wa uaminifu
Alisema kuwa mnamo tarehe 23 Septemba 2011 magazeti ya Tanzania Daima,Mwananchi na Majira yaliripoti taarifa inayofanana kwamba Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo amekimbia na sanduku la kura kufuatia vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Songea
“Napenda kuutaarifu umma kwamba habari hizo siyo za kweli na ni uzushi mtupu,ukweli ni kwamba mimi katika kikao hicho sikukimbia na sanduku la kura wala hakuna diwani yeyote aliyetoka au kukimbia nje ya ukumbi na sanduku la kura kama ilivoripotiwa na magazeti hayo”alisema Dkt Nchimbi
Alieleza kuwa ukisoma upotoshwaji huu katika magazeti yaliyoandika habari hizo utagundua kwamba habari hizo zimeandikwa na mtu mmoja na kuwagawia waandishi wenzake wa magazeti mengine bila kuthibitisha wakazipeleka kwenye magazeti yao
“Taarifa hizo zilizopotoshwa kwa makusudi zimenidhalilisha,kunichafulia jina langu na kunifanya kuwa mtu nisiyeaminika kitaifa na kimataifa”alisema Dkt Nchimbi
Alieleza zaidi kuwa tabia iliyoanza kuzoeleka hivi sasa ya mwandishi mmoja kuandika kisha kuwasambazia wenzake unawazalilisha waandishi wenyewe na vyombo wanavyoviandikia
Alisema kuwa kwa taarifa hii nayataka magazeti ya Tanzania Daima,Mwananchi na Majira kukanusha na kusahihisha taarifa hizo kwenye magazeti yao ya kesho tarehe 26 September 2011
Kwenye ukurasa wa mbele na kuniomba radhi
MWISHO