About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, January 12, 2012

MFUMO DUME WAATHIRI MAENDELEO WILAYANI NAMTUMBO


Na Stephano Mango,Namtumbo
IMEBAINIKA kuwa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma inaukandamizaji mkubwa wa haki za wanawake na watoto kutokana na mfumo dume na kuwafanya wanawake wengi wasinufaike na kazi za uzalishaji mali wanazozifanya kila siku
Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Saveri Maketa wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya uwezeshaji wa uchanganuzi na uchambuzi wa sera ya maendeleo ya wanawake  na jinsia yanayoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Ruvuma(Ruwodefu) kwa ufadhiri wa Shirika la The Foundation For Civil Society
Maketa alisema kuwa hali hiyo imewafanya wanawake wengi kubeba mzigo mkubwa wa kazi ya uzalishaji na kutunza familia kwa ujira kidogo na kuwafanya wanawake hao kurudi nyuma kimaendeleo na kuendeleza kuzifanya kaya nyingi kuwa maskini
Alisema kuwa ni wajibu wa Asasi za kiraia kushirikiana na Serikali kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali wakiwemo wa sheria ili kuweza kuwajengea uwezo wananchi wa kutambua haki na wajibu wao katika jamii ili waweze kujiletea maendeleo kwa  mgawanyo ulio sawa wa kipato kadiri ya faida walizozipata kifamilia
Baadhi ya viongozi wa dini ambao wanashiriki katika mafunzo hayo walisema kuwa mafunzo yamewafikia muda muafa kabisa kwani wanashuhudia ongezeko la kuvunjika kwa ndoa na kusababisha watoto na wazee wengi kuishi katika mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu kutoka kwa wazazi na wategemezi wao kinyume na sheria na wajibu wa jamii
Viongozi hao wamesema mara kwa kuisha kwa mafunzo hayo wana wajibu wa kutoa elimu hiyo kupitia mahubiri yao katika nyumba za ibada ili kurekebisha hali hiyo kulingana na sera ya wanawake,jinsia na watoto
Awali Mwenyekiti wa Asasi ya Ruwedefu Siwajibu Gama alisema kuwa mafunzo hayo ya siku tano  yanashirikisha viongozi wa makundi mbalimbali zikiwemo taasisi za dini,asasi zisizo za kiserikali na wanawake wenyewe ambayo yana lenga kuandaa wawezeshaji watakaokwenda kuelimisha katika ngazi ya jamii Wilaya ya Namtumbo yenye kata 18
Gama alisema kuwa pamoja na kufundisha umuhimu wa usawa katika kuleta maendele,mada nyingine ni madhumuni ya sera ya jinsia,haki za binadamu,mgawanyo na umiliki wa rasilimali kati ya wanawake na wanaume na sheria ya ndoa
MWISHO