About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, January 30, 2015

WAZEE SONGEA WAIOMBA SERIKALI WAPATIWE MATIBABU BURE

     Wazee wakiwa kwenye tafakari ya changamoto zao
 
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA

WAZEE wa kata ya Misufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameiomba  serikali iweze kuangalia upya suala la kupata matibabu bure kwa wazee wenye umri kaunzia 60 kwa kuiboresha kwa kuwa sasa imekuwa haionyeshi kama matibabu hayo hutolewa bure kutokana na kushindwa kupata dawa na baadala yake kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa yaliyoko nje yaeneo lahospitali.

Ombi hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya wazee Mfaranyaki  [MMWM] ,Lawrence Mbewe wakati wa mdahalo uliofanyika kata ya Misufini mjini hapo ambao ulikuwa ukijadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee hasa katika upande wa upatikanaji wa matibabu bure ambayo ni sera iliyowekwa na serikali.

Akiongea kwenye mdahalo huo uliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Civil Society la mjini hapo ,Mbewe alisema kuwa licha ya kuwepo kwa sera inayowataka wazee kutibiwa bure lakini bado wanakabiliwa na changamoto za matibabu hayo ikiwemokushindwa kupata dawa na kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya madawa.

Alisema kuwa kama wanakuwa wamepata bahati ya kupata dawa ,hupewa za kutuliza maumivu hasa Panadol na siyo dawa za kutibu ugonjwa wanaosumbuliwa nao jambo ambalo amedai kuwa baadhi ya wazee wengi kushindwa kutibiwa kwa kutokumdu gharama za dawa.

‘’Tunaiomba serikali iweze kuliangalia hili namna ya kutusaidia maana sasa hali ya wazee siyo nzuri maana unaweza ukapokelewa na daktari vizuri lakini unapozidi kuendelea kupata huduma ya matibabu unakuta unaambiwa dawa hakuna labda tukusaidie za kutuliza maumivu Panadol na dawa nyingine ukanunue kwenye maduka ya madawa”alisema mwenyekiti
,Mbewe.

  Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Songea ,Victor Nyenza akitolea ufafanuzi wa sera ya wazee kutibiwa bure kwenye mdahalo huo alisema sera hiyo ilianzishwa mwaka 2015 ya kuzitaka kila  Halmashauri kuhakikisha wazee wanatibiwa bure
Nyenza alisema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni upungufu wa madawa kwenye vituo vya afya na mahospitalini jambo ambalo hufanya wazee wengi kuona hawatendewi haki katika sera inayowataka watibiwe bure.

MWISHO



No comments:

Post a Comment