About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, April 17, 2012

MADIWANI WALILIA ONGEZEKO LA POSHO KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA

Na Augustino Chindiye,Tunduru

MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameibuka na kulilia nyongeza ya
maslahi yao likiwemo ongezeko fidia,nauli na posho za vikao.

Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao cha kawaida cha Baraza la halmashauri hiyo lililo keti katika ukumbi wa Klasta Mjini hapa.

Huku akishangiliwa na Madiwani wenzie katika kikao hicho Diwani wa kata ya Marumba Msenga Said Msenga alisikika akilalama na kuiomba Serikali kutambua na kuona umuhimu wa kuwaongezea mafao pamoja na posho wakati wa vikao.

“Umefika wakati wa Serikali kutuona sisi tunao wawakilisha wananchi ngazi hiyo ya kata maeneo yaliyopo vijijini fedha tunazopata zote zinaishia njiani kutokana na gharama za usafiri na za maisha kuwa juu “ alisema Msenga

Katika taarifa hiyo Diwani huyo alitolea mfano wa madiwani hao kulipwa nauli ya Shilingi 3500 kwa madiwani wanaotoka vijijini lakini wakati huo hali halisi wao hutozwa kati ya shilingi 7,000 na 8,000 kutokana na hali ya maisha kupanda.

Diwani huyo ambaye alionekana wazi kuungwa mkono na madiwani wenzakealifikia hatua ya kupendelezwa kuwa posho zao ziongezeke hadi kufikia shilingi Milioni 3 kutoka Shilingi 120,000 ambazo wamekuwa wakilipwa hivi sasa  kwa mwezi.

Mambo mengine yaliyo ibuka katika kikao hicho ni lawama za madiwani hao kwa Serikali wakiituhumu kuchelewesha fedha hali ambayo imepelekea miradi mingi kukwama na kusababisha kero kwa wananchi.

Akifafanua kero hiyo Mtoaji wa kero hiyo Makamu mwenyekiti wa halamashauri ya Wilaya hiyo Diwani wa kata ya Nakayaya Charles Haule alisema kuwa pamoja na kukiweka chama tawala katika wakati mgumu katika chaguzi zijazo.

Alima pamoja na hali hiyo pia hivi sasa asilimia kubwa ya wananchi imeonekana kukatishwa tamaa na utendaji wa viongozi waliopo madarakani kutokana na kushindwa kusimamia maendeleo na kufanya miundombinu hasa ya barabara kushindwa kupitika wakati wote wa mwaka.

Hata hivyo Haule alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenzake kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi ili waongeze juhudi za kushiriki katika shughuli za kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakigoma kufanya kazi hizo wakiamini kuwan miradi yote imekuwa ikitengewa fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo kwa asilimia 100.

Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo alikiri kuwepo mrundikano wa mirani viporo hali iliyoonesha kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa fedha za miradi kutoka Serikali kuu.
Mwisho
Mratibu wa Mradi wa TOT juu ya uchanganuzi na uchambuzi wa sera ya maendeleo ya wanawake na Jinsia Wilaya ya Songea Samwel Chiwangu akieleza neno la utangulizi wakati wa mafunzo hayo jana

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama akifungua mafunzo hayo, kulia ni Katibu wa mafunzo Mathew Ngarimanayo na kushoto ni Mwenyekiti wa mafunzo Fatuma Misango

Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kusikiliza mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji

Katibu wa CCM Wilaya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alfonce Siwale akisikiliza mada zilizokuwa zikiwakilishwa jana, aliyekaa nyuma yake ni Diwani wa Vitimaalum wa Manispaa ya Songea Rehema Millinga

Washiriki wakiendelea na mafunzo

Mwandishi wa Habari Mwandamizi Nyanda za Juu Kusini na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Juma Nyumayo akichukua kumbukumbu ya Hotuba ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo kutoka kwa Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama

Washiriki wa mafunzo ya Uchanganuzi na Uchambuzi wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia Wilaya ya Songea wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama

WANANCHI WATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wametakiwa kuheshimu haki za binadamu kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria ili kila mtu aweze kuishi kwa amani na upendo katika jamii yake na nchi kwa ujumla kuliko kujichukulia sheria mkononi na kusababisha kukatisha uhai wa mwenzio
Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa mafunzo  ya uchanganuzi na uchambuzi sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia  Wilaya ya Songea Samwel Chiwangu yaliyoitishwa na Asasi ya Ruwodefu ambayo yanayofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Saccos kwa ufadhiri wa shirika la The Foundation For Civil Sociaty
Chiwangu alisema kuwa inasikitisha kusikia matukio ya ukatili wa kijinsia yakiendelea kushamiri kwa kasi kubwa mkoani Ruvuma tofauti na utamaduni uliozoeleka miongoni mwa wananchi wa jamii za mkoa huo hali ambayo inatishia ustawi wa jamii
Alisema kuwa taarifa ya vifo vya kujinyonga,kupigana,kuchinjana kutokanana  na mahusiano ya kimapenzi na matatizo mengine ya kijamii vinashamiri kila siku hali ambayo inaonyesha mashaka makubwa kwa wananchi
“Wanaharakati tunapaswa tusikitike sana na taarifa hizo na tuchukue hatua kukomesha hali hiyo, kwani mtu unayempenda huwezi kumuua kwa sababu za kukunyima penzi au kumkuta mpenzi wako na mwanaume  au na mwanamke mwingine hivyo kama kweli unampenda utamlinda na vishawishi vinavyoweza kupunguza upendo wake kwako na sio kumuua”alisema Chiwangu
Alisema kuwa haki ya kuishi ni haki kubwa kuliko zote na kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mwenzake kwa sababu yoyote ile kwani mwenye uwezo na mamlaka hayo ni mwenyezi mungu pekee yake ni vema kazi yake tukamuachia
Alisema kuwa jambo hilo halipaswi kuvumiliwa hata kidogo hivyo ni vema viongozi wa dini na wakijamii pamoja na Serikali kushirikiana kikamilifu kudhibiti jambo hilo kwani kabla vifo havijatokea kunakuwepo na dalili za kutokuwa na amani miongoni mwa wapenzi hao tujaribu kusuluhisha migogoro kwa taratibu za mila na desturi na kwamba ikishindikana basi sheria itumike kudhibiti vifo hivyo
Akifungua mafunzo hayo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama alisema kuwa wanawake nchini wanatakiwa kuacha uwoga wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya habari ili kuweza kujenga mazingira ya kukomesha ukatili mbalimbali wa kijinsia uliokithili miongoni mwa jamii zinazotuzunguka
Mhagama alisema kuwa vyombo vya habari ni wadau muhimu sana katika harakati za ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi hasa wakati huu ambao taifa letu linaelekea kwenye miaka 50 ya uhuru ili kuweza kuzibaini changamoto mbalimbali za wanawake zilizokuwa zinawakabili wanawake miaka hiyo na sasa tuweke mikakati mingine ya kuzikabili changamoto za sasa
Awali Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Ruwodefu Hieromina Lugomi alisema kuwa mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo wananchi kutambua fursa zilizomo ndani ya sera ya wanawake na jinsia ili waweze kunufaika nayo
Lugomi alisema kuwa watu wanaohudhuria mafunzo hayo kwa lengo la kupata elimu,kubadilishana mawazo na kuangalia maeneo muhimu yaliyopo kwenye sera hiyo na kuishawishi Serikali iyafanyie kazi maeneo hayo ni pamoja na vikundi vya wajasiriamali, viongozi wa dini, viongozi wa siasa,na vikundi vya wafanyabiashara
Alisema kuwa washiriki watapata fursa ya kujadili kwa upana haki za binadamu,madhumuni ya sera ya wanawake na jinsia, malengo ya sera, maana ya jinsia, usawa wa kijinsia,mgawanyo wa madaraka, umiliki wa rasilimali sheria ya ndoa na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia
MWISHO

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA UBAKAJI

NA DUSTAN  NDUNGURU, MBINGA.

MKAZI mmoja wa kijiji cha Kihuru wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma amehukumiwa na mahakama ya wilaya adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 15.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Mbinga Joakim Mwakyolo alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kuwa Dickson Komba alitenda kosa hilo la ubakaji.

Mwakyolo alisema kuwa mahakama imemtia hatiani Komba na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Mara baada ya kusomewa hukumu hiyo mshitakiwa alibubujikwa na machozi huku akiangua kilio mahakamani hapo na kuomba kwa sauti apunguziwe adhabu.

Awali mwendesha mashitaka wa polisi inspekta Mwamba alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Komba alitenda kosa la kumbaka msichana huyo akiwa anaenda dukani machi 5 mwaka jana majira vya saa 3 usiku.

Aliendelea kudai kuwa pamoja na kumfanyia kitendo hicho pia alimpora simu moja aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 130,000 na fedha tasilimu shilingi 15,000 mali ya Essau Dukila.

                            MWISHO.