About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 9, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU KUJADILIANA MAENDELEO YA BARABARA ZA MIKOA HIYO NA VIONGOZI WA MCC

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na kiongozi wa miradi ya MCC Mzee Mchomvu walipokutana kwenye kikao maalumu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
 Wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, wa pili Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wakijadiliana maaendeleo ya barabara katika mikoa hiyo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kiongozi wa Miradi ya MCC
 Wakuu wa Mikoa ya Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakiagana na ujumbe wa viongozi wa MCC baada ya kumalizika kwa kikao chao maalum kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Kiongozi wa miradi ya MCC Mzee Mchomvu akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kuzungumza na wakuu wa Mikoa ya Rukwa na Ruvuma

ELIMU YA SAYANSI NI NGUZO MUHIMU KWA NCHI ZILIZOENDELEA KIUCHUMI DUNIANI

Na Stphano Mango,Songea
HAKUNA sululu itakayoweza kukidhi mahitaji ya Taifa lolote Duniani kwa kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi kama Serikali husika itashindwa kuwekeza katika elimu ya sayansi na teknolojia kwa wananchi wake
Kwani ni ukweli ulio wazi kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia katika nchi nyingi duniani ni nguzo muhimu ya maendeleo kutokana na umuhimu wake katika kuvumbua maarifa mapya ambayo hutumika viwandani ili kuzalisha bidhaa mbalimbali
Dhana ya sayansi kinadharia ni chachu  katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na kubadili mfumo wa maisha kutoka kwenye lindi la umaskini hadi kwenye ustawi stahiki wa maisha ya binadamu kwa kuweza kuwa na huduma bora za kijamii
Tafsiri sahihi ya dhana ya sayansi kama ilivyotafsiriwa na kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la 2004, inaeleza kuwa ni elimu inayotokana na uchunguzi,majaribio,vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo,utafiti huo unaleta jawabu sahihi la matumizi yake kwa wakati uliopo
Kamusi hiyo inaendelea kufafanua kuwa teknolojia ni maarifa ya sayansi yaliyowekwa katikamatumizi ya vitu mbalimbali kama zana au mitambo katika viwanda,mawasiliano,ufundi na kilimo
Kulingana na tafsiri hiyo ni wazi kuwa sayansi ndio baba wa teknolojia inayopandwa kwa binadamu ili kumwezesha kutumia maarifa hayo katika kuleta mapinduzi ya maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla
Nchi za Magharibi kama Marekani,Kanada,Uingereza,Ujerumani,Ufaransa na zile za Mashariki kama Urusi,China,Japan Na India  ni miongoni mwa nchi zilizojikita katika kupanua wigo wa taaluma ya sayansi
Ambapo mafanikio ya teknolojia ya sayansi katika nchi hizo yamesaidia kufanikisha malengo ya tafiti mbalimbali ambazo nyingi kati ya hizo zinatokana na uzalishaji katika sekta ya viwanda
Mfano wa uzalishaji huo upo wazi kama vile simu za mkononi,modemu za intaneti,flash disk,Cd,memori card ambapo uzalishaji huo umewezesha kufanyika kwa biashara za kimataifa katika muda mfupi
Idadi kubwa ya wafanyabiashara wamekuwa wakijihusisha na biashara hizo kutoka nchi za Mashariki ya mbali kwa kuagiza kupitia teknologia ya mtandao na kuziingiza kwenye nchi zao ikiwemo na wafanyabiashara wa Tanzania na kusifia ubora wa bidhaa hizo kupitia matangazo mbalimbali utafikiri huko kiwandani wakati bidhaa hiyo inatengenezwa alikuwepo
Tumekuwa mabingwa wa kusifia bidhaa za wenzetu bila nasi kushiriki katika ugunduzi wa teknolojia iliyozalisha bidhaa hiyo,hivyo sasa ni muda muafaka wa kujiuliza vitu tunavyotumia leo katika maendeleo ya sayansi na teknolojia watanzania tumechangia nini?
Tunafurahia kama mazuzu kuruka kwa ndege kutoka sehemu ya mkoa hadi mwingine,nchi mpaka nchi nyingine kwa haraka,je mchango wetu kwenye kifaa hicho uko wapi? Vifaa kama vile kompyuta,luninga ambavyo tunavitumia kuangalia mambo mbalimbali duniani mchango wetu upo?
Sayansi ndiyo iliyovumbua matumizi ya kompyuta,utengenezaji wa mitambo,ndege,meli,magari,roketi,rada,zana za kivita,ujenzi wa majengo na barabara vyote ni kutokana na dhana ya sayansi
Jambo la kujiuliza ni njia zipi zinazofanikisha teknolojia hiyo kufanikiwa katika nchi husika? Hapo sasa ni wajibu wa serikali kujipanga katika elimu elekezi na thabiti ambayo itafanikisha teknolojia hiyo kupatikana mashuleni
Tunahitaji elimu ya ubunifu ambayo imesheheni vitendo kuliko nadharia kwani elimu ya uvumbuzi ndio ambayo imesaidia nchi nyingi duniani kuwa na maendeleo endelevu na kuachana na maendeleo bandi ambayo sisi tumekuwa tunajivunia huku tukisubiri kila kitu kulishwa kutoka kwenye mataifa mengine kana kwamba siye tumekuwa mazuzu
Nchi zilizoendelea zilitumia muda mwingi kutoa kipaumbele cha elimu kwa wananchi wake katika Nyanja ya sayansi pamoja na ugumu wake na ukubwa wa gharama za kuisomea kuliko masomo mengine lakini faida yake ni kubwa sana
Kuendelea kuogopa kuwekeza elimu ya sayansi nchini ni kushindwa kuwapata wanasayansi halisi kwa kipindi chote toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kwani elimu ya chuo kikuu ilinayoendelea kutolewa leo nchini inamahusiano ya masomo ya jamii pekee yake
Kutolewa kwa elimu ya sayansi kunahitaji mitambo ambayo itamwezesha mwanafunzi kufanya majaribio ya vitendo na kubaini majibu ya nadharia aliyojifunza darasani,uwepo wa  na miundombinu  stahiki yatakuwa yanamsaidia mwanafunzi kuunda,kuvumbua vitu
Elimu hiyo ndio ya kujivunia kwani ndiyo wanayoitumia wenzetu kuitawala dunia yetu leo hii hivyo katika suala hili ni lazima masomo ya sayansi yapewe msukumo zaidi kwa kufundishwa na walimu waliobobea ili kuweza kuleta zao stahiki
Hapo Mitaala ya sayansi ni lazima ziwe na maabara nzuri zilizojitosheleza kwa vifaa vinginevyo wanafunzi wa shule hizo wataishia katika masomo ya nadharia na Taifa litaendelea kukodisha teknolojia kutoka katika nchi zilizoendelea kisayansia
Somo kama fizikia ni lazima wanafunzi  wapatiwe vitabu vya kutosha ambapo somo hilo linapaswa lifundishwe kwa kina hasa kwa vitendo hivyo somo hilo halipaswi kufundishwa kwa ajili ya kuwasaidia kufanya mtihani tuu
Wafundishwe somo hilo kuibua ubunifu  wa wanafunzi ,tuachane na tabia ya kuwafundisha kufaulu mitihani kwani dunia ya sasa inahitaji watu ambao ni wabunifu hata masomo ya kemia na bayolojia yanatakiwa yawajengee uwezo wa kisayansi wanafunzi hao
Teknolojia ni nguzo muhimu ya kuanzisha viwanda vya mitambo ya juu,kati na midogo ambapo mitambo mikubwa ni pamoja na ile ya kutengeneza magari,matrekta,mashine za kufuma nguo,ya kutengenezea barabara ,madaraja na inayotumika kuchimbia madini migodini
Elimu ya sayansi huwawezesha wataalam kubuni mambo mbalimbali ya vyombo vya mawasiliano,utengenezaji wa silaha na ufundi wa zana mbalimbali
Watafiti mbalimbali wa kisayansi wanafafanua kuwa ukosefu wa teknolojia unaongeza umasikini katika jamii na taifa kwa ujumla hivyo uwekezaji katika elimu ya sayansi ungesaidia kufanya tafiti mbalimbali za mafuta,makaa yam awe na mali asili zingine
Ukosefu wa elimu ya sayansi ndio chanzo cha ukodishaji wa maliasili za nchi kwa makampuni ya kigeni kwa makampuni ya kigeni kwa kuwa taifa husika halina uwezo wa kufanya tafiti hizo hata kwa upande wa viwandani utafiti wa dawa za binadamu na mifugo unahitajika ili kuboresha huduma zinazotolewa na sekta ya afya
Wakati umefika sasa tuwe na wataalam ambao wanaweza kutengeneza vifaa tulivyoviainisha hapo juu mfano upo wazi Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) waliweza kutengeneza gari aina ya Nyumbu hiyo ni ishara njema kwa taifa letu hivyo tuwekeze huko
Ni lazima tujiulize kuwa Japan inayozalisha utitiri wa magari ya aina ya Toyota ambayo yamesambaa dunia nzima wao wana nini zaidi yetu au India inayozalisha magari aina ya Tata wana nini zaidi yetu
Jibu ni rahisi,uwekezaji kwenye elimu ya sayansi ambayo italeta uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali kwani wenzetu wameweza kuwekeza huko na kuchukua muda mwingi kufikiria ubunifu wa kitu furani ambacho kitakuja kukuza uchumi wa nchi yao
Kama tutashindwa kuchukua hatua stahiki leo basi nchi za Marekani ,Korea,China,Urusi,India na mataifa mengine yataendelea kugeuza nchi za afrika maeneo ya kuuzia bidhaa zao kwa sababu sisi hatuna mchango katika uzalishaji
Hatari yake nyingine licha ya kwamba nchi yetu itageuzwa jalala la bidhaa nyingine hata watu wetu watageuzwa watumwa wa kuuza bidhaa za nchi hizo kwa sababu elimu ya uvumbuzi tumeishiwa hivyo tuzinduke kama kweli tunataka kuwa sehemu ya maendeleo yaliyopo duniani
Ni aibu kuendelea kuimba kuwa sisi tuna maendeleo ya sayansi na teknolojia wakati kila tunachotumia kinatoka nchi za wengine nasi kazi yetu kusifia tuu uzuri wa kitu hicho utafikiri tulikuwepo wakati kinatengenezwa
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0755-335051

MHANDISI MANYANYA MKUU WA MKOA WA RUKWA ATEMBELEA SHULE YA UFUNDI YA WALEMAVU YOMBO JIJINI DAR ES SALAAM NA KUWATIA MOYO WANAFUNZI HAO

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Ufundi Yombo mara baada ya kuwasili chuoni hapo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia jiko lililotengenezwa na wanafunzi wa chuo cha walemavu Yombo alipotembelea chuoni hapo na hasa katika darasa la wanafunzi wanaojifunza kutengeneza vyuma ambapo jiko hilo alilinunua kwa shilingi elfu ishirini 20000
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza Mwanafunzi pekee wa kike Mariam Kamala katika ufundi wa kuunga vyuma chuoni hapo
 Wanafunzi wa ufundi uselemala chuoni hapo wakimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya namna wanavyojifunza ufundi huo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikagua mitambo ya ufundi useremala alipotembelea darasa la ufundi huo katika chuo cha Yombo

 Wanafunzi wa Darasa la Ufundi Seremala wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya alipotembelea chuo hicho
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa kwenye darasa la ufundi kushona

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiamuangalia Mwanafunzi Catherine alivyokuwa anajifunza kushona nguo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia wanafunzi wa Uhazini katika chuo cha Ufundi Yombo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwasalimia wanafunzi wa darasa la Ufundi Umeme katika chuo cha Yombo

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimuelekeza Mwanafunzi wa Ufundi Umeme Yusuph Said alipotembelea darasa hilo la umeme
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi wa Umeme katika Chuo hicho cha Yombo, ikumbukwe kuwa Mhandisi Stella Manyanya ni msomi na mtaalamu wa ngazi ya juu katika fani ya ufundi umeme na kabla ya kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alikuwa Injinia wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania Tanesco

Chuo cha Ufundi kwa Wanafunzi wenye Ulemavu cha Yombo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu, vifaa na mitambo ya ufundi wa kada tofauti, walimu na gharama

Katika ziara yake Mhandisi Manyanya aliwapa moyo wanafunzi hao na kutoa kwa kila darasa shilingi 10000 ambapo jumla ya shilingi elfu tisini 90,000 alizitoa kwenye chuo hicho

WANANCHI WAUA SIMBA NA KUTAFUNA NYAMA YAKE

Na Steven Augustino Tunduru

WAKAZI wa Kijiji cha Mkowela Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamefanikiwa kumuua Simba na kula nyama yake ikiwa ni ishara ya kuonesha machungu waliyo kuwa nayo dhidi yake.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa Simba huyo ali uawa kufuatia msako mkali ulio washirikisha wananchi na mhifadhi wa wanyama Pori Ahmadi Ally aliye tumwa na Idara yake kuhakikisha kuwa Simba huyo anauawa.

Walisema msako wa Simba huyo ulianza Feb 23 mwaka huu baada ya Simba huyo kuonekana akizunguka katika mitaa ya Kijiji hicho na vijiji jirani na kusababisha hofu kwa wananchi.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu Afisa Wanyama pori wa Wilaya hiyo Peter Mtani mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa katika kipindi hicho Simba huyo alifanikiwa kuua Ng`ombe 2 Mbuzi 4 na Mbwa 2.

Mtani aliendelea kufafanua kwa kuwataja wamiliki wa Mifugo hiyo kuwa Ng`ombe walikuwa ni mali ya Hasan Mbwana na Mfugaji wa Jamii ya Kisukuma aliyetambulika kwa jina moja la Relesh.

Kuhusu Mbuzi na Mbwa Mtani alisema kuwa walikuwa mali ya  Alli Ngalaisho, Edward Immeni, Peter Hasani,James Ado na Lilasi Said  wote wakiwa niu wakazi wa Kijiji hicho.

Kufuatia tukio hilo Mtani alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wanapo waona wanyama wakali kama huyo wawahi kutoa taarifa katika idara yake ili waweze kuchukua hatua kabla hawajasababisha madhara kwao

Mwisho

KAMATI YA KUCHUNGUZA MAUAJI MKOA WA RUVUMA KUWASILISHA RIPOTI YAKE HIVI KARIBUNI

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU
Na Gideon Mwakanosya, Songea 
KAMATI huru ya kuchunguza vurugu zilizotokea katika Manispaa ya Songea February 22 mwaka huu ambazo zilisababisha vifo vya watu watatu vikiwemo vifo viwili vilivyotokana na kuuwawa kwa kutumia silaha za moto na Askari Polisi iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kupewa kazi ya uchunguzi ndani ya siku saba inatarajia kukamilisha kazi hiyo ya uchunguzi mwanzoni mwa wiki ijayo badala ya jana siku ambayo ilipangwa kuikamilisha.
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com  jana ofisini kwake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu alisema kuwa ofisi yake mpaka sasa bado haijapokea taarifa ya kamati aliyoiunda  kufanya kazi ya uchunguzi wa kina zaidi kwa lengo la kubaini chanzo na sababu  iliyosababisha na kuwepo kwa vurugu hiyo.
Alieleza zaidi kuwa wakati kamati hiyo inaendelea kufanya kazi yake hali ya utulivu imekuwa ni nzuri na usalama umezidi kuimarishwa zaidi na kwamba kila kata imeweka mikakati ya ulinzi shirikishi ambao kila mkazi wa Manispaa ya Songea anapaswa kushiriki.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mwambungu alifafanua kuwa bado jitihada zinaendelea kufanywa kwa kukutana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa mila na watu mashuhuri na wamedhehebu ya dini kwa lengo la kukemea uvumi na imani potofu zinazo sababisha uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali kwa ustawi wa nchi na amesisitiza kila mwananchi awe na utii wa sheria badara ya kujichukulia sheria mkononi.
Amewataka wakazi wa Manispaa ya Songea kuwa makini katika shughuri zao za kila siku na badara yake waachane na uvumi ambao ndio ulio onekana umesababisha kuwepo kwa vurugu kubwa mjini Songea lakini kwa vile kamati ya uchunguzi ipo tuiachie indelee kufanya kazi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Songea ambaye pia ni Kuu wa wilaya hiyo Thomas Ole Sabaya aliauambia mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com kuwa tangu majuzi anaendelea kufanya ziara kwenye kata zote 21 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuweka ulinzi shirikishi kwenye maeneo wanayo ishi .
February 22 mwaka huu kulitokea mauaji ya watu wawili ambao inadaiwa waliuawa kwa kupigwa risasi na Askari Polisi na mwingine mmoja alikufa hapohapo  baada ya kutumbukia kwenye shimo wakati wananchi wenye hasara kufanya maandamano yaliyokuwa na vurugu ambayo yalilazimika yadhibitiwe na chombo cha dola.
Kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Askari Polisi wanne walidaiwa kuhusika na mahuaji ya watu wawili walikamatwa na wanaendelea kuhojiwa na Polisi na watu 54 walitiwa mbaroni kwa kufanya maandamano bila kuwa kibali na kusababisha Manispaa ya Songea kutokuwa na amani.
Mwisho.