About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, December 31, 2011

HERI YA MWAKA MPYA WA 2012 UWE WENYE MAFANIKIO NA FANAKA KWA WATU WOTE



The New Year 2012 is going to be really amazing and will be full of new plans and ideas I am sue because what ever we do in past we try not to do that again in future. We will keep good things to be carried and we will surely not going to repeat the bad deeds again.


 The year of 2012 is kept as the part of secret mission as there are certain pretendances that this year will be the end. Now no body knows as we live in present so we don’t think about future bad happenings much.


 The New Year is going to be the rocking year for every one out there. The New Year eve party 2012 will bring out smiles on many faces as every one love to party out with friends and families.


On this day all of the crowd keep on jumping on dance floor with lots of good music till it hit the clock 12:00.
When it strikes at 12 o’ clock every one wishes New Year to the people around and the real celebration or we can say welcoming of the New Year begins.


The New Year eve celebration not only have the cool and grooving music it also have tasty and delicious food and drinks which are served to the guests presented over their.


New Year is the time of celebration and planning new events. No matter what the previous year holds for you, every one want to move on with happiness on their faces. The day of New Year has marked as the beginning of calendar year.

 The day of New Year has been marked very firstly in the calendars of “Gregorian” calendars and then it is used world wide with the date that comes up as the 1 January. This day is the most energetic day which is celebrated with joy, happiness, prayers and parties all around the world.

Time to celebrate New Year around the World then you must see the lightnings and party organized in every country.
Every country in the world have its own way of celebrating this day some have disco parties and some have street parties. Every one enjoys being part of this day and celebrates it with lots of joy and happiness and how can we forget the delicious meal.

Happy New Year
New Year is the time of joy and happiness which brighten up the whole year in everyone’s life. On this day all the people forget their past grudges and move forward in life with the love ones.

New Year is the day which signifies the ending of previous year and welcoming the new day. It is the time foe every one happiness as people have new plans and ideas for this day.

 Forgetting all past deeds and entering into New Year era gives you hope and confidence to start up new things and accept the new life. Making a remark in every New Year is very much important in your life so make every year memorable and remarkable.

The day of happy New Year is really happy and the day which is used is incremented. There are many events which are celebrated on this day and today it is on such a large scale that it can be viewed world wide.

On the final day of year that is 31st December night every one plans a party and night outs to make the last day of eve memorable. There are many hotels and cruises which organize all night parties for the folks to enjoy.

Every new year have its own amazing powers but the New Year 2012 will the most exciting to watch on. The year of 2012 is not predicted yet because according to science this year wont exists more so may be people are scared rather than being happy.

There are few opposite to this situation as many people in year 2012 have special for themselves and they believe they will make it more memorable as the previous year and will start new plans and ventures for themselves.

Wishes are the most believable part in human nature. Wishing any one new year brings a smile on their faces as it is a blessing. The New Year wishes can be in any form that is it can be verbal or it can be written. There are many beautiful cards that are available in the market to wish or greet your loved ones.

MVUA YABOMOA NYUMBA 23 NA RADI YAJERUHI WANAFUNZI WAWILI

Na, Augustino Chindiye Tunduru

WANAFUNZI wawili wa Shule ya Msingi Majala wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru baada ya kujeruhiwa vibaya na radi huku kukiwa na taarifa kuwa wakazi wa familia 23 kukosa sehemu za makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na Mvua.

Akizungumzia tukio lilo Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Tunduru, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Juma Madaha aliwataja Watoto hao kuwa ni Subira Mohamed  anayesoma darasa la Tatu na Stamili Mohamedi anayesoma Darasa la  sita wote wakiwa ni Watoto wa familia moja.

Kuhusu tukio la Nyumba 23 kubomolewa na mvua hizo Dc, Madaha alisema kuwa hivi sasa wananchi hao wanahifadhiwa katika nyumba za majirani zao wakati serikali ya Wilaya hiyo ikifanya tathimini ya athari zake.

Alisema kufuatia matukio hayo wananchi wanapaswa kujikinga kwa kuimarisha miundombinu ya nyumba zao pamoja na kuachana na tabia za kujificha katika miti wakati mvua zikiendelea kunyesha ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Akifafanua taarifa ya tukio la radi Kaka wa majeruhi hao Wada Said alisema kuwa mkasa huo ulitokea wakati Watoto hao wakiwa wamejificha katika kibanda cha jiko la kupikia ambapo mvua kubwa iliyo ambatana na upepo ikinyesha kwa muda mrefu huku radi zikipigwa na kusababisha kuwajeruhi ndugu hao   

Akizungumzia hali za majeruhi hao mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo Dkt. George Chiwangu alisema kuwa hali za majeruhi hao bado siyo mzuri na wanahitaji kuwa chini ya maafisa tabibu kwa muda mrefu ili kuokoa maisha yao .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibisha kuwepo kwa matukio hayo na kueleza kuwa majeruhi wa tukio la radi waliumizwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao kufutia tukio hilo .

Mwisho.

Friday, December 30, 2011

SONNGO WAMALIZA MDAHALO JIMBO LA SONGEA NA JIMBO LA PERAMIHO KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama akiwasalimia wananchi walioshiriki mdahalo wa wazi wa Katiba ya mwaka 1977,kushoto ni Katibu wa mtandao wa Sonngo Mathew Ngarimanayo,kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mtandao wa Sonngo Siwaji Gama,Makani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Andrwe Mbawala
 Viongozi wa ngazi mbalimbali katika Serikali,Siasa ,Asasi za Kiraia wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mdahalo ulioendeshwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society uliofanyika kwenye ukumbi wa Trade Jimbo la Peramiho



 Mwanaharakati Juma Nyumayo akisalimiana na Mwanaharakati mwenzake Fatuma Misango nje ya ukumbi wa Trade baada ya kumalizika kwa mdahalo wa Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977
 Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama wa pili kutoka kulia akiwa na wapiga kura wake baada ya kumalizika kwa mdahalo katika jimbo hilo
Mwandishi wa Habari wa TBC Catherine Nyoni akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Maposeni ambaye pia ni Afisa Kilimo wa Kata hiyo Esta Mango mara baada ya kumaliza mdahalo

WABUNGE WATAKIWA KUWASAMBAZIA WAPIGA KURA WAO KATIBA YA MWAKA 1977

Na Stephano Mango,Songea
WABUNGE wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wametakiwa kuona umuhimu wa kuwafikishia wapigakura wao Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ili waweze kuisoma na kuijadili kwa umakini kabla ya kutoa maoni yao wakati Tume itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kutoa maoni ya kuandika Katiba mpya itakapokuwa inapita katika maeneo yao
Wito huo umetolewa jana na wananchi kwenye mdahalo wa wazi wa mapitio na uchambuzi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Jimbo la Peramiho uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ufundi(Trade) wa Kanisa Katoliki la Peramiho ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Songea(Sonngo) kwa ufadhiri wa The Foundation For  Civil Society
Akizungumza kwenye mdahalo huo Deo Mbunda alisema kuwa wananchi wengi hawaijui Katiba ya mwaka 1977 kutokana na usiri mkubwa uliowekwa na Serikali kwa kushindwa kuzisambaza kwenye maeneo mengi kutokana na sababu zilizojificha na kuwafanya wananchi washindwe kuzipata kwa urahisi
Mbunda alisema kuwa kwa kuwa Serikali toka mwaka 1977 walipoitengeneza Katiba hiyo imeshindwa kuisambaza hivyo jukumu hilo lichukuliwe na Wabunge wetu ambao tuliwachagua kwa kura nyingi waweze kutuwakilisha hivyo nao waone umuhimu wa kutuletea Katiba hiyo ili nasi tuzipate na kuweza kuzisoma kisha tuweze kutoa maoni ya kuandika Katiba mpya
“Mwaka 2010 ulifanyika uchaguzi mkuu wa Wabunge,Madiwani na Urais ambapo wagombea wote waliweza kutumia nguvu kubwa kubandika mabango yao ya kushawishi wananchi waweze kuwachagua ni vema basi nguvu ileile waliyoitumia viongozi hao kwa wale walioshinda waitumie kuwasambazia wananchi Katiba ya mwaka 1977 ili tuweze kuzisoma kwa umakini na kutoa mwanga katika Katiba ijayo”alisema Mbunda
Akizungumzia jambo hilo Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama alisema kuwa Katiba ya mwaka 1977 zimesambaa katika maduka mengi ila kutokana na wananchi wengi hawakuwa na mahitaji ya Katiba hiyo na kwa kuwa sasa watanzania wamekuwa wakijadili uwepo wa Katiba mpya ndio maana wanajitokeza kwanza kuisaka katiba ya mwaka 1977
Mhagama alisema kuwa kila mmoja wetu ana haki ya kutoa maoni yake na kuijadili katiba iliyopo hivyo kwa Jimbo la Peramiho nitazileta Katiba hizo kwenye Ofisi ya kila Kijiji ili wananchi waweze kuisoma na kujadiliana wenyewe kwa wenyewe na kutoa maoni yao kwa amani na utulivu wakati utakapofika badala ya kuwa jambo la watu wachache
Awali akifungua mdahalo huo Mwenyekiti wa Sonngo Siwajibu Gama alisema kuwa mdahalo huo ni muhimu sana kwani unalengo la kuwajengea uwezo wananchi wa kuielewa katiba ya mwaka 1977 na kuwapa ujasiri wakati wa kutoa maoni wakati tume itakapo pita kuchukua maoni ya kuandika Katiba mpya
Gama alisema kuwa Sonngo imetoa fursa ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili waweze kuwa wazi katika mjadala wa Katiba mpya kwa kuweza kutoa maoni yao kwa mambo yatakayoleta mabadiliko chanya katika uandikaji wa Katiba mpya kwa faida ya vizazi vilivyo na vijavyo na kwamba kila mtu akielewa vizuri Katiba ya mwaka 1977 ataweza kutoa maoni yake kwa usahihi zaidi
MWISHO

JIMBO LA PERAMIHO NAO WAPELEKEWA MDAHALO WA ELIMU YA URAIA KUHUSU KATIKA YA TANZANIA YA MWAKA 1977

 Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo akiwakaribisha washiriki wa mdahalo katika ukumbi wa Trade Kanisa Katoliki la Peramiho
 Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Sonngo kutoka kushoto ni Komba,Francis Mhimila,Amon Mtega mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Sophia Limbuya,Magreth Ponera wakiendelea kusikiliza mdahalo huo
 Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wa Serikali wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na waendesha mdahalo
 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama,Mwenyekiti wa Sonngo Siwajibu Gama,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Andrwe Mbawala,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi wakifuatilia kwa umakini mdahalo huo

 Washiriki wa Jimbo la Peramiho wakifuatilia mdahalo huo
 Mwandishi wa TBC Catherine Nyoni,Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Mwandishi wa Chanel Ten Emmanuel Msigwa wakiendelea kunasa matukio yanayojili kwenye mdahalo huo
Mwandishi wa Habari wa Radio Maria Tanzania Jofrey Nilai akirusha mdahalo huo LIVE uliofanyika kwenye ukumbi wa Trade Peramiho

Thursday, December 29, 2011

MDAHALO WA WANANCHI NA VIONGOZI MBALIMBALI JIMBO LA SONGEA MJINI KUHUSU MAPITIO YA KATIBA UKUMBI WA KANISA LA BOMBAMBILI WAMALIZIKA NA SASA NI ZAMU YA JIMBO LA PERAMIHO





 Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo akizungumza katika mdahalo

 Mwanaharakati na Mwandishi wa Habari mkongwe Juma Nyumayo akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo
 Mwanaharakati Fatuma Misango kulia na Ifigenia Mbawala wakifuatilia mdahalo huo
Mwenyekiti wa Mtandao wa Sonngo Siwajibu Gama akiwa na Katibu wa Mtandao huo Mathew Ngarimanayo
SONGEA NETWORK OF NON – GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS
(SONNGO)
SLP. 791 SONGEA – RUVUMA TANZANIA
Simu Na:025- 2600877, Simu ya kiganjani: 0754-533032, 0752 - 202117
Baruapepe: sonngosongea @yahoo.Com
Ofisi – Barabara ya Sokoine Jengo la CCM Mkoa

                 
HISTORIA YA KATIBA TANZANIA
 NA MICHAKATO YA UANDIKAJI WAKE


1.0.   MAANA YA KATIBA
Wanazuoni, wanaharakati, wadau, wabia wa maendeleo na wananchi mbalimbali wanaielezea Katiba kwa mitazamo tofauti kutokana na mandhari na matumizi yake katika jamii.  Hata hivyo makundi yote hayo wanaielezea Katiba kuwa ni:-

·        Waraka wa Kisiasa, Kiutawala na Kisheria ambao unawawezesha wananchi kujitambua kama Taifa, unaelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola na kuongoza shughuli zote kisheria ambao ndio chimbuko la sheria zote nchini.

·        Pia Katiba ni muafaka wa Kitaifa na ni mkataba kati ya viongozi na wananchi.

2.0.         MISINGI NA SIFA YA KATIBA.
                                                          i.            Katiba lazima iwezeshe wananchi kuridhiana kitaifa.
                                                       ii.            Wananchi kuwa na nguvu ya kumiliki Katiba yao.
                                                     iii.            Katiba kuwa ya kipekee kutokana na historia ya nchi hisika.
                                                     iv.            Katiba kuwa na nguvu ya kisheria inayozingatia haki za binadamu, haitoi mwanya wa ubaguzi wala upendeleo wa aina yoyote.
                                                       v.            Katiba lazima itoe maono na mwelekeo wa Taifa.
                                                     vi.            Katiba lazima iweke bayana masuala ya msingi ya kitaifa na mustakabali wake.

3.0.         KATIBA ZILIZOTANGULIA TANGU UHURU
Tangu Tanganyika na Zanzibar zipate Uhuru na kuungana kumekuwa na Katiba 5 za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba kadhaa za Zanzibar.  Kwa upande wa Zanzibar tunagusia kwa muhtasari Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na marekebisho ya 10 ya Katiba hiyo ya mwaka 2010.

Katiba zilizotangulia tangu Uhuru ni hizi:-

3.1.         KATIBA YA UHURU (1961)
·        Katiba hii iliundwa kwa lengo la kuipatia Tanganyika Uhuru wake toka kwa Waingereza, ndio maana ikaitwa Katiba ya Uhuru.
·        Katiba hii iliundwa Uingereza na kuileta Tanganyika.
·        Katika uandikaji wake Katiba hii haikushirikisha wananchi wa Tanganyika.
·        Katiba hii ilimtambua Waziri Mkuu ambaye hakuwa na madaraka makubwa kwani yeye alikuwa anasimamia masuala ya serikali bungeni tu.
·        Malkia wa Uingereza bado alikuwa na madaraka makubwa kwani maamuzi mengi yalikuwa yanamtegemea Malkia.
·        Katiba hii haikutambua haki za binadamu.
·        Hata hivyo baadhi ya mambo mazuri yaliyokuwamo katika Katiba ya Uhuru ni kwamba:-
                                                         i.            Katiba ilitoa Uhuru wa Mahakama.
                                                       ii.            Baraza la Mawaziri na Waziri mmoja walikuwa wanawajibika kwa Bunge.

3.2.         KATIBA YA JAMUHURI (1962)
·      Katiba hii iliitwa Katiba ya Jamuhuri kwa sababu ndiyo iliyoanzisha mfumo wa Urais.
·      Mchakato wa kuiandika kwake haukushirikisha wananchi.
·      Bunge la wabunge 71 wa TANU walijigeuza kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha Katiba hii.
·      Katiba hii ilimtambua Rais kuwa mkuu wa Nchi na kiongozi wa serikali.
·      Baraza la mawaziri na Waziri mmoja mmoja sasa walikuwa wanawajibika kwa Rais.
·      Rais wan chi alikuwa na nguvu nyingi sana.
·      Sheria nyingi zilitungwa chini ya Katiba hii na nyingi zilikuwa kandamizi.

3.3.         KATIBA YA MUUNGANO (1964)
·        Katiba hii iliundwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuwa nchi moja. 
·        Katiba hii ilisimamia mambo 11 ya Muungano na mambo ya Serikali ya Tanganyika.
·        Katiba hii iliweka muundo wan chi wa serikali mbili (Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar)
·        Katiba hii ilimtambua Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano na mjumbe wa baraza la mawaziri.
·        Katiba hii ilianzishwa kwa tamko la Rais na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la wawakilishi Zanzibar.
·        Katiba hii ilikuwa ya muda ya Muungano na ilikusudiwa kutumika kwa muda wa mwaka mmoja tu.
·        Katiba hii iliweka utaratibu wa wa kuandaa Katiba ya kudumu ya Muungano kwa kuunda tume ya Katiba na bunge la Katiba ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

3.4.         KATIBA YA MPITO (1965)
·        Katiba hii iliitwa ya mpito.
·        Katiba hii ndio iliyoitambua nchi kuwa ni ya chama kimoja tu cha siasa (TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa upande wa Zanzibar).
·        Katiba hii ndiyo iliyotamka rasmi chama kushika hatamu kuu ya TANU (NEC) ilikuwa na nguvu zaidi kuliko bunge au hata Katiba yenyewe.
·        Katiba hii ilipitishwa kama sheria ya kawaida inavyopitishwa bungeni.
·        Katiba ya TANU ilikuwa sehemu ya Katiba ya Muungano.
·        Katiba hii iliongeza mambo ya Muungano.
·        Utata wa Uhuru wa Muungano (autonomy) kuwa nchi ulionekaka dhahiri.
·        Tume ya Rais ya Katiba ya kukusanya maoni kwa wananchi iliundwa.

3.5.         KATIBA YA KUDUMU (1977)
·        Katiba hii iliitwa Katiba ya kudumu.
·        Katiba hii ilikuwa ya Tano.
·        Uandikaji wa Katiba hii haukushirikisha wananchi.
·        Katiba hii ilipatikana kupitia tume ya Rais yenye wajumbe 20 (10     
     toka  Tanzania bara na 10 toka Tanzania Zanzibar).
·        Tume hii ya Rais iliongozwa na Sheikh Thabita Kombo na Katibu wa tume alikuwa ndugu Pius Msekwa.
·        Kabla ya kuandika Katiba ya kudumu, tume hii ilianza kuandika Katiba ya CCM baada ya kuunganisha vyama vya TANU na ASP tarehe 5/2/1077.
·        Katiba ya kudumu ilijikita katika misingi mikuu mitatu yaani:-
                                                       i.            Urais wenye nguvu zaidi.
                                                     ii.            Mfumo wa chama kimoja.
                                                  iii.            Mfumo wa serikali mbili.

·        Katiba ya kudumu ilipitishwa kwa Rais kuliteua Bunge la kawaida kujigeuza kuwa bunge la Katiba na kupitisha Katiba ndani ya masaa matatu tu.

4.0.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1977
·        Katiba ya kudumu ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko 14 na kwa kiasi kikubwa mabadiliko hayo yamewakwepa wananchi, isipokuwa mabadiliko ya mwaka 1984 ambayo yaliwashirikisha wananchi.
·        Badala ya NEC kufanya maamuzi ilianzisha mjadala wa mwaka mmoja wa wananchi na kuiagiza serikali kutekeleza.
·        Baadhi ya mapendekezo ya wananchi yalikuwa ni:-
                                                                   i.            Hati ya haki za binadamu.
                                                                 ii.            Kujitawala kwa Zanzibar ambayo haikuwemo kwenye mapendekezo ya chama.
·        Mwaka 1991 Rais mstaafu Hassan Mwinyi aliteua tume ya   
                          kuangalia hali ya kisiasa nchini.  Tume hii iliongozwa na                                      
                          marehemu Jaji Francis Nyalali.
·        Tume hii pamoja na mambo mengine ilipendekeza kufutwa kwa sheria kadhaa kandamizi na kufanyia mabadiliko Katiba ya Muungano nay a Zanzibar.
·        Mwaka 1988 iliundwa tume nyingine iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga ambayo nayo pia ilitoa mapendekezo yake mengi kuhusiana na masuala ya kisiasa nchini.

4.1.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1979.
·        Mabadiliko haya yalilenga kuanzisha mahakama ya Rufaa nchini yaani kwa Muungano na Zanzibar.

4.2.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1980
·        Mwaka 1980 Katiba ya kudumu ya mwka 1977 ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa malengo tofauti tofauti:-
                                                             i.      Mabadiliko yalifanywa kwa lengo la kuimarisha Muungano
     kwa kujibu masuala ya Zanzibar.
4.3.         ii. Kuweka mfumo wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
·        Kuweka mfumo wa Serikali ya Zanzibar.
·        Kuweka muundo wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
4.4.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1982
·        Mabadiliko haya yalilenga uteuzi wa wakuu wa mikoa ingawa hayakuweka uwajibikaji wa wakuu wa mikoa na Wilaya.

4.5.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko haya yalilenga kuingiza masuala ya haki za binadamu kwenye Katiba ya nchi.

4.6.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1990
          Mwaka 1990 Katiba ya kudumu ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa lengo la :-
·        Kuanzisha Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.

4.7.                                 Kuweka utaratibu wa kupata mgombea mmoja wa Urais kwa Zanzibar.

4.8.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1992
          Mwaka 1992 yalifanyika mabadiliko ya Katiba mara mbili kwa malengo ya :-
·        Kufuta mfumo wa chama kimoja nchini.
·        Kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
·        Kubadilisha mfumo wa bunge la Jamuhuri ya Muungano na kuanzisha viti maalum vya wanawake kufikia 15% na viti 5 toka baraza la wawakilishi.
·        Yalianzisha uandikishaji wa vyama vya siasa na uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa.


4.9.         Miezi sita baadae baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya nane ya Katiba
          yalifanyika mabadiliko mengine yaliyolenga:-
·        Kubadilisha utaratibu wa uchaguzi wa Rais.
·        Nguvu ya Bunge ya kumuondoa Rais madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye iliwekwa.
·        Ilianzisha nafasi ya Waziri Mkuu na uwezo wa Bunge wa kumuondoa madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
·        Masharti ya Rais kulivunja Bunge yaliwekwa.

4.10.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1993
·        Mabadiliko hayo yalifanywa kwa lengo la kuzifanya chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais kufanyika kwa pamoja.
·        Mabadiliko hayo pia yaliipa nguvu “Tume y Taifa ya Uchaguzi” kisimamia chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais.

4.11.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1994
·        Mabadiliko hayo yalikuja kutokana na mapendekezo ya Tume Paul Boman.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyomtambua mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ambaye angekuwa Makamu wa Rais.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyofuta Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
·        Mabadiliko hayo yaliendelea kumtambua Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe katika baraza la mawaziri la Jamuhuri ya Muungano.

4.12.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1995
·        Mabadiliko haya yalifanyika mwaka 1995 kabla ya kuvunja bunge.
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la :-
                                                       i.            Kumtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano na Makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kula kiapo cha kuulinda Muungano.
                                                     ii.            Mabadiliko haya pia yaliweka ukomo wa muda wa Urais wa kukaa madarakani kuwa ni awamu mbili za miaka mitano mitano.

4.13.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2000
·        Mabadiliko haya yalifanywa baada ya uchaguzi wa kwanza kwa mfumo wa vyama vingi na baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Jaji Robert Kisanga.
·        Mabadiliko hayo yalilenga:-
                                                       i.            Ilifafanua kura za ushindi wa Rais sio lazima awe ameshinda kwa 51% na zaidi bali Rais atatangazwa kuwa mshindi kwa uwingi wa kura.
                                                     ii.            Mabadiliko haya yalimpa uwezo Rais wa kuteua watu 10 kuwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano.
                                                  iii.            Mabadiliko hayo pia yaliongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 15% hadi 20%.

4.14.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2005
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la:-
                                                       i.      Kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 20% hadi 30% .
                                                     ii.      Uhuru wa kuabudu.
                                                  iii.      Uhuru wa kushiriki na watu wengine katika kujieleza.
                                                  iv.      Utaratibu wa kuteua wabunge wa viti maalum kwa wanawake kutegemea na uwiano wa ushindi katika uchaguzi.

5.0.         KATIBA YA ZANZIBAR YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yaliyofanyika mwaka 2010 yameleta maswali mengi kwa Watanzania kwani kwa kiasi kikubwa yamegusa sana masuala ya Muungano, hivyo tunaweza kusema Muungano umetikisika kwani:-
                                                 i.            Yameitambua Zanzibar kama nchi na mipaka yake, bendera na vikosi vyake.
                                               ii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar  kuigawa Zanzibar kama Wilaya na mikoa kinyume na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanashauriana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
                                            iii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar ya kuteua wakuu wa mikoa na Wilaya.
                                            iv.            Yameipa Zanzibar Mahakama ya Rufaa ambalo lilikuwa suala la Muunano hapo awali.
                                               v.            Yameongeza idadi ya viti maalum vya wanawake na kuwa 40% ambapo Muungano ni 30%.
                                            vi.            Yamemtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni mkuu wan chi.
                                          vii.            Yameanzisha makamu wawili wa Rais ambapo Katiba ya Jamuhuri ya Muungano haiwatambui.  Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inawatambua Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi.
                                       viii.            Yameweka wigo wa baraza la wawakilishi kutochezea na kubadilisha Katiba ya Zanzibar na hasa sehemu inayohusu tamko la haki za binadamu na ibara ya kwanza nay a pili mpaka kura ya maoni ipigwe.

6.0.         KWA NINI KATIBA MPYA SASA
·        Watanzania wengi wanajiuliza swali hili, kwa nini Katiba mpya sasa?  Lakini jambo la maana zaidi ni pale tunapowaona watanzania wanajibu swali hili ingawa kwa mtazamo tofauti tofauti.
·        Hizi nitakazozitaja hapa chini ni sababu chache zinazitajwa na watanzania walio wengi kuwa ndizo sababu hasa zinazopeleka Taifa kwenye utungaji wa Katiba mpya.  Sababu nhizo ni pamoja na:-
                                           i.            Katiba za awali hazikushirikisha wananchi hivyo Katiba hizo hazikutokana na matakwa ya wananchi.
                                         ii.            Katiba ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko mengi (14) hivyo ni dhahiri imepoteza sifa za kuitwa Katiba ya kudumu.
                                      iii.            Marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
                                      iv.            Mfumo wa kisasa nchini wa vyama vingi vya siasa, kwani Katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja cha siasa.
                                         v.            Kuweka sawa swala nyeti na muhimu la Muungano maana kuna mkanganyiko kati ya serikali na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar, suala hili linatakiwa liwekwe vyema katika Katiba mpya.

7.0.         MCHAKATO WA KUTUNGA KATIBA MPYA
Kuna njia mbalimbali za kutunga/kuandika katiba mpya nchini, lakini wanazuoni na wananchi walio wengi wanapendekeza njia/mchakato ufuatao kama nitakavyoeleza hapo baadae.

·        Nchi yoyote inaingia kwenye machafuko ya kivita kwa kuwa wananchi wake wanakosa jukwaa la kujadili na kukubaliana namna bora na inayofaa ya kufanya michakato mbalimbali inayohusu maamuzi wan nchi zao na namna bora ya kutumia rasilimali zao, hioy ikiwa ni pamoja na suala hili tunalozungumzia la uandikaji/utungaji wa Katiba mpya.

·        Wananchi kama Taifa ni muhimu na ni vema wakubaliane namna mchakato wa kuandika Katiba mpya utakavyokuwa.

·        Baadhi ya njia/mchakato wa kuandika Katiba ambao unapendekezwa na wanazuoni na wananchi mbalimbali mchakato ambao unatoa fursa kwa wananchi wote kushirikikatika hatua zote za uandikaji wa Katiba mpya ni huu

                                                          i.            Mijadala ya awali ya Katiba.
·        Hii ni hatua ya awali kabisa ambapo wananchi wanapata fursa ya kuibua, kujadili na kukubaliana mambo ambayo wanataka yazingatiwe katika Katiba mpya.  Hili laweza kufanyika katika mikutano ya vijiji, kata na mikusanyiko ya ibada.

                                                       ii.            Mkutano Mkuu wa kitaifa.
·        Mkutano huu utajadili mambo yaliyoibuka katika majadiliano ya makundi, kuyachambua na kuyapanga katika mafungu mambo yanayojadilika, kwa mfano mambo yanayohusu haki za binadamu, rasilimali za nchi, mgawanyiko wa madaraka na
masuala ya kubishaniwa (contentious issues).  Mkutano huu unatakiwa uhusishe uwakilishi mpana wa makundi mbalimbali ya wananchi.

Inashauriwa wajumbe wa mkutano huu wachaguliwe na wananchi kama sheria itakavyoelekezwa kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa kuhusu masuala muhimu.

                                                     iii.            Tume ya wataalamu wa Katiba (Constitutional commission)
·        Hii ni hatua ambapo tume ya wataalamu wa Katiba na sheria itateuliwa.  Kazi ya tume itakuwa ni kuratibu maoni ya wananchi na kuyaweka katika waraka maalum na kuhamasisha wananchi.

·        Tume hii ya wataalamu wa Katiba na sheria inapendekezwa iteuliwe na Rais na kuthibitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano ambalo litawawakilisha wananchi.

·        Tume hii inapendekezwa kuwa na wataalam wa kada mbalimbali na izingatie usawa wa kijinsia.

                                                  iv.                  Mjadala wa waraka maalum wa Katiba.
·        Matokeo ya kazi ya tume ya wataalam yatawekwa katika waraka maalum wa Katiba kwa ajili ya mjadala mpana zaidi wa wananchi juu ya yaliyomo.

                                                     v.                  Bunge maalum la Katiba (constituent Assembly)
·        Rasimu ya Katiba ikishaandaliwa ipelekwe mbele ya Bunge maalum la Katiba.

·        Bunge hili maalum la Katiba liundwe kwa utaratibu maalum tofauti na bunge lililopo la Jamuhuri ya Muungano.


·        Bunge hili maalum la Katiba liwakilishe makundi mbalimbali kama vile wanawake, wanaume, walemavu, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, madhehebu ya dini mbalimbali na kadharika.

·        Kazi kubwa ya bunge hili ni kupitia na kuridhia rasimu ya Katiba iliyoandaliwa.
·        Bunge maalum la Katiba litakoma mara tu baada ya kuridhia rasimu hiyo ya Katiba.

                                            vi.      Kura ya maamuzi (Referundum)
·              Baada ya rasimu ya Katiba kuridhiwa na Bunge maalum la Katiba, hatua ya mwisho katika kupata katiba mpya ni kwa wananchi kushiriki kwa njia ya kura ya maamuzi.

·              Kura hii itapigwa nchi nzima na wananchi wote wenye na sifa za kupiga kura watapiga kura.


·              Endapo kura za ndio kwa Katiba zitazidi zile za hapana Katiba itakubalika na kuanza kutumika/kufanya kazi.


AHSANTE SANA KWA KUNISIKILIZA NA KARIBU KWA MAJADILIANO.