About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, September 5, 2011

POLISI RUVUMA INAWASAKA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA MAUAJI

                             Na Gideon Mwakanosya, Songea.
 
POLISI mkoani Ruvuma inawasaka watu watano wakazi wa kijiji cha Likuyuseka kilichopo wilayani Namtumbo kwa tuhuma za kumuuwa Issa Lupia (47) wakati wakiwa kwenye kilabu cha pombe  za kienyeji.
 
Akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoani hapa Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja usiku huko katika eneo la kilabu cha pombe za kienyeji kijiji hapa.
 
Alisema kuwa watuhumiwa hao baada ya kugunduwa kuwa wametenda kosa walitoroka na kutokomea kusikojulikana na kwamba kwa sasa hivi polisi inaendelea kuwasaka watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuwa wametorokea nchi jirani ya msumbiji.

Amefafanua kuwa inadaiwa kuwa kabla ya tukio Lupia aliondoka nyumbani kwake na aliaga kwamba anaenda kwenye kilabu cha pombe za kienyeji kilicho karibu ambako alipofika alimkuta Hamza Saidi ambaye ni rafiki yake akiwa na wenzake wane.
 
Alisema kuwa Lupia aliungana na wenzake walianza kunywa pombe na baadae walianza kutofautiana ndipo ulipotokea ugomvi ambapo Lupia alipigwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwilini na kumsababishia kifo papo hapo.
 
Kamanda alisema kuwa watu waliokuwa jirani na eneo hilo walipofika kwenye tukio ghafla watuhumiwa hao walianza kutawanyika mmoja baada ya mwingine na kutokomea kusikojulikana ndipo taarifa ya tukio hilo ilipelekwa kwenye ofisi za serikali ya kijiji na baadae polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga wa hospitali ya Mkoa alithibitisha kuwa Lupia amekufa kutokana na kipigo.
 
Alisema kuwa chanzo cha tuki hilo ni ulevi ambao baadae uliwafanya watofautiane na kuanza kumpiga mwenzao Lupia na kumsababishia kifo.
 

ASAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA DADA YAKE

                                        Na Gideon Mwakanosya,Songea.
 
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka Rashuel Mapunda mkazi wa mtaa wa misheni Mbinga mjini kwa tuhuma za kumbaka dada yake mwenye umri wa miaka 14  ambaye jina lake limeifadhiwa anayesoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya kutwa ya Makita.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9.alasali nyumbani kwa wazazi wao ambako inadaiwa Mapunda alimkamata dada yake kwa nguvu na kumfanyia kitendo cha unyama.
 
Kamuhanda alifafanuwa zaidi kuwa inadaiwa kuwa siku ya tukio msichana huyo akiwa anajiandaa kufanya shughuli za usafi nyumbani kwao ghafla alimkuta kaka yake amefika na kumkamata na kumalazimisha avue nguo kasha alifanya nae mapenzi.
 
Alisema kuwa wakati Mapunda anafanya tendo hilo la kinyama kwa dada ake ambaye alipiga kelele kwa ishara ya kuomba msaada majirani wasikia na walipofika kwenye nyumba hiyo walimkuta mapunda tayari ameshambaka msichana huyo.
 
Kamuhanda alisema kuwa majirani pamoja na wazazi wake wakiwa kwenye eneo la tukio walianza kumkimbiza Mapunda kwa lengo la kutaka kumkamata walishindwa baada ya yeye kuwatoroka a kutokomea kusikojulikana.
 
Alisema kuwa baadae msichana huyo walimpeleka kwenye hospitali ya wilaya ya Mbinga kwa matibabu ambako ilibainika kuwa mwanafunzi huyo ameumizwa vibaya sehemu zake za siri ambazo zimeonekana kuwa na michubuko mingi.
 
Kamanda alisema kuwa jeshilake linaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo na kwamba akipatikana atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
 
MWISHO.  

CHADEMA WAMFYATUKIA MGOMBEA UMEYA WA CCM SONGEA CHARLES mHAGAMA

                                Diwani wa kata ya Misufini kupitia Chadema Salum Mfamaji
                                         Katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma Dorphini Ghazia
                                         Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime
Na,Stephano Mango,Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimemshukia mgombea wa nafasi ya Umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kupitia Chama cha Mapinduzi(Ccm) Charles Mhagama kwa madai kuwa sio kiongozi makini na muadilifu anayeweza kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa maslahi ya wananchi
 
Akihutubia mamia ya wakazi wa Manispaa ya Songea katika viwanja vya soko la Manzese,kata ya Misufini Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa nafasi ya Umeya ni nafasi nyeti sana katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea hivyo ina hitaji mtu makini,mwenye hekima,busara na muadilifu wa kuweza kushirikiana na wadau mbalimbali kuweza kulisukuma gurudumu la maendeleo
 
Fuime alisema kuwa kutokana na umuhimu huo mgombea aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi (Ccm)Charles Mhagama ili kuweza kuziba nafasi ya Umeya iliyoachwa wazi na Marehemu Ally Manya aliyefariki mwezi julai 29 mwaka huu,kuwa hana uwezo wa kushika nafasi hiyo kutokana na kujaa tamaa ya kujitajirisha kiharamu kupitia fedha za wananchi
 
Alieleza kuwa Mhagama ni kiongozi mbabe na mwenye kupenda rushwa hali inayodhorotesha maendeleo ya wananchi kwani alishawahi kufanya vitendo viovu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ushawishi wa rushwa katika ununuzi wa gari ya kuzima moto,uuzwaji wa Katapila la Halmashauri akiwa ni Diwani wa kata ya Matogoro na kiongozi wa Kamati mbalimbali za baraza la madiwani
 
“Mhagama hawezi kuwa kiongozi bora na atakayeweza kutupeleka kwenye ustawi stahiki wa maisha kwani vitendo vyake vingi ni viovu kwani kuna kipindi alikuwa na mahusiano na mwanafunzi mmoja miaka ya nyuma ambapo alikutwa naye kwenye nyumba ya wageni na wazazi wa mwanafunzi huyo na kupelekewa kupigwa viboko hadharani”alieleza Fuime
 
Alifafanua kuwa vitendo hivyo vinadhihirisha ni jinsi gain alivyokuwa mchafu na kiongozi mbovu asiyestahili kupewa majukumu makubwa ya Umeya hasa katika kipindi hiki kilichogubikwa na ufisadi,rushwa na urasimu mkubwa Serikalini
 
Alisema kuwa siku zote Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwaacha viongozi wazuri na kuwateua viongozi wabovu ili waweze kukinufaisha chama kwa maslahi yao binafsi hivyo hatuwezi kuongozwa na kiongozi wa aina hiyo na ndio maana tunapaza sauti ili umma ujue na kuwaambia Madiwani wao waliowachagua kutokumpigia kura mgombea huyo wa Ccm kwenye uchaguzi wa Serikali unaotegemewa kufanyika Septemba 25 mwaka huu
 
Alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni mali ya wananchi wote na sio mali ya chama fulani hivyo wananchi pazeni sauti zenu kwa maslahi ya vizazi vilivyopo na vijavyo ili waweze kufaidi rasilimali zilizopo kuliko kuwaachia watu wenye dhamira mbaya wazizoe rasilimali hizo
 
Alieleza kuwa kwa kuwa chama cha Mapinduzi kipo kwa ajili ya kuwanyonya watanzania,kunyanyasa haki za binadamu kwa maslahi ya wachache basi Chadema tutatetea haki za binadamu na kuzuia unyanyasaji wowote na ndio maana tunapaza sauti zetu ili wananchi muamke na kudai maisha yenye ustawi kwani ni haki zenu
 
Awali Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma Dorphine Ghazia akingua mkutano huo alisema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali katili sana kwa watu wake ndio maana wanaona wananchi wanahangaika kwa maisha magumu wao wanaendelea kuwakandamiza
 
Ghazia alisema kuwa watanzania hawana huduma bora za afya,miundombinu,elimu,maji wao wanawatukuza wanyama kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi mfano mzuri wa vyura vya kihansi wanalindwa kuliko binadamu,hivyo Chadema kitaendelea kuthamini utu wa binadamu kwa kuwatendea mambo yenye ustaarabu katika maisha yao
MWISHO