About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, October 24, 2011

SANGOMA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMTOA MIMBA BINTI YA MIAKA 19

Na Cresensia Kapinga,Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mganga wa jadi Christian Ngonyani (58) mkazi wa kijiji cha Ngahokola Songea Vijijini kwa tuhuma za kumtoa mimba yenye umri wa miezi tisa  ya Mwanamke  Rehema Njerekela (19) mkazi wa kijiji cha  Magagula  wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Inspecta  Paul Mashimbi amesema kuwa tukio hilo limetokea  oktoba 18 mwaka huu majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Magagula  ambapo Mganga huyo alipatiwa kiasi cha shilingi elfu arobaini na tano kwa lengo la kumtolea mimba  ya miezi tisa.
Alisema kuwa,awali mwanamke huyo alienda kwa Sangoma huyo wakati akiwa na ujauzito wa miezi minne ambapo walipojaribu kumtoa mimba hiyo iligoma kutoka  lakini ilipofika oktoba 18 mwaka huu akiwa na sangoma huyo walirudia tena kuharibu mimba hiyo lakini safari hii Kilitoka kiumbe chenye jinsia ya kiume kikiwa hai .
Inspekta mashimba ameongeza kuwa,mara  baada ya kufanya jaribio hilo na kufanikiwa kutoa mtoto akiwa hai  siku mbili baadaye Mwanamke huyo alimfukia akiwa hai baada ya kumchimbia shimo upenuni mwa nyumba yao na kumfukia akiwa hai.
Alisema, mara baada ya tukio hilo polisi walipokea taarifa toka kwa wasamaria wema zikiwaeleza kuwepo kwa tukio la mwanamke huyo kumfukia mtoto wake akiwa hai na walipofika  na kufukua  walimkuta mtoto huyo akiwa ameshafariki .
Alisema, Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo pamoja na Sangoma kwa kosa  la mauaji na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea ,na ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.
Aidha,Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa  Dkt.Benedicto Ngaiza amethibitisha kumpokea mwanamke huyo ambaye amelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu  baada ya kupata maumivu makali baada ya kuharibu mimba hiyo.
MWISHO.

WAKAZI WA MKENDA WAHAHA KUSAKA MAJI SAFI NA SALAMA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA


Wakazi wa Kitongoji cha Mkenda Kijiji cha Nakawale Kata ya Muhukuru wakihaha kuchota maji kwenye bomba maarufu kwa Danida ikiwa ni miaka 50 ya UHURU na wakati mwingine ulazimika kusaka maji hayo zaidi ya kilometa 3,wananchi hao wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa huduma za afya,elimu,miundombinu na maji

MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYE NDIVYO INAVYOTAFSIRIKA PICHA HII

Vijana ambao hawakuweza kufahamika majina yao mara moja wakiwa wanasukuma mkokoteni jilani na Kanisa Katoliki Jimbo la Songea Mjini ikiwa ni kuelekea miaka 50 ya UHURU wa Nchi yetu kama walivyokutwa na mpiga picha wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/