About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, February 15, 2012

KAPTENI KOMBA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYA SHILINGI MILIONI 3 MASHINDANO KOMBE LA MBUNGE

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimkabidhi Chogo Wachogo sare 3 za waamuzi wa Mashindano ya Kapteni Cup ambayo yanashirikisha timu 10 za Kata ya Lituhi

Kiongozi wa Timu ya Polisi Fc akikabidhiwa jezi kwa ajiri ya mashindano hayo

Kiongozi wa Timu ya Shujaa Fc akikabidhiwa jezi

                                     Kiongozi wa Timu ya Ngingama akikabidhiwa jezi

Viongozi wa Timu mbalimbali shiriki katika mashindano hayo wakikabidhiwa jezi za mashindano na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba


MVUA YA MAWE ILIYOAMBATANA NA UPEPO YAEZUA NYUMBA SONGEA


                         MKUU WA WILAYA YA SONGEA THOMAS OLEY SABAYA

Na Gideon Mwakanosya,Songea

NYUMBA  kumi na tatu zimeezuliwa kata ya Ruvuma  Manisipaa ya Songea kutokana na  mvua ya mawe iliyo ambatana na upepo ambayo  ilinyesha jana kuanzia majira ya saa tisa  mchana hadi saa kumi .

Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com katika kata za Mshangano ,Bombambili ,Mfaranyaki ,Lizaboni, Ruhuwiko ,Majengo ,Subira na Ruvuma  umebaini kuwa kata ya Ruvuma  mtaa wa mjumbe  Saidi Ndenyende  ndio ulioathirika sana na mvua hizo.

Hata hivyo mitaa yote ya katikati ya mji wa Songea  mvua hizo zimeangusha baadhi ya miti ya kivuli ,nguzo za umeme , nyaya za simu  na zile za kuingizia picha za runinga .

Akiongea kwa uchungu Laita Swedi  alisema  “Umekuja upepo mkali ulioambatana na mvua ya mawe nikasikia kishindo kwuuuuuapo ndipo niliona mbingu na bati likawa limeondolewa nyumbani mwangu na kuacha vyumba vitatu vikinyeshewa mvua “Alisisitiza Laita Swedi .

Naye Stella  Komba wa kata hiyohiyo ya Ruvuma ameleza kuwa  yeye alikuwa anatoka hospitali ambako alikuwa amempeleka mwanaye kwa matibabu lakini  alipoikaribia nyumba yake akakuta imeezuliwa na paa limetupwa mbali  na nyumba yake  hivyo  kuacha vyumba zaidi ya vinne kuwa wazi .

Mtandao huu ulilifanya juhudi ya kumtafuta Mwenyekiti wa mtaa Said Ndenyende  ili aweze kueleza iwapo amewatembelea  waathirika  wa mvua hizo lakini taarifa zilizo patikana nyumbani kwake alikuwa amekwenda  shambani kwake eneo la  Sanangula umbali wa kilometa 24 kutoka  katikati ya mji wa Songea  ,pia mtendaji wake hakupatikana ofisini kwake .

Mtaaramu mmoja ambaye hakutaka jina lake  litajwe alisema yeye ni fundi  wa ujenzi  kama angeweza  kufanya ukandarasi wa kutengeneza nyumba hizo kila nyumba angeitengeneza kwa shilingi  milioni mbili na kwamba  nyumba zote kumi na tatu zingegharimu shilingi milion ishirini na sita .

Mtandao huu, bado unaendelea  na uchunguzi wa uharibifu uliofanywa na mvua hizo hasa upande wa mazao ,miti ya kupandwa na mifereji ya maji,Hata hivyo jitihada za kumpata mkuu wa wilaya  ya Songea  Thomas Ole  Sabaya ili aweze kutoa tathimini ya hasara iliyojitokeza  hakuweza kupatikana  kwa kuwa alikuwa kwenye shughuli maalumu za kikazi.

Mwisho.