About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, June 27, 2012

WAKULIMA WA KOROSHO WALILIA MADAWA YA KUUA VISUMBUFU


Na Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa Korosho Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuwa na msukumo na kuhakisha Madawa ya Pembejeo za bei ya ruzuku ambayo hutumika kwa ajili ya Kupulizia na kuua visumbufu katika mikorosho yao yanafika kwa wakati.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima hao walisema kuwa malalamiko hayo yametokana na kuwepo kwa taarifa za kutatanisha juu ya ujio wake huku mikorosho yao ikiwa katika hali ya kuhitaji kupuliziwa baada ya kuchanua
Mtua issa,Kawanga Abdala na Milanzi Athuiman ni miongoni mwa wakulima waliopaza sauti zao na kuongeza kuwa endapo madawa hayo yataendelea kucheleweshwa kuna hatari ya wakulima hao kuanguka kimavuno msimu huu wa mwaka 2012/2013.

Walisema hali hiyo inatokana na wakulima wengi kushindwa kumudu bei ya Shilingi 45,000/= kwa mfuko wa kilo 25 za madawa hayo kutoka kwa wafanyabiashara walanguzi tofauti na bei ya ruzuku ambayo mfuko huo ulipangwa kuuzwa kwa Shilingi 12,000.
Akizungumzia hali hiyo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Chiza Marando alisema kuwa tayari ofisi yake imekwisha kabidhi kazi hiyo kwa Mzabuni aliyeteuliwa kusimamia usambazaji wa madawa ya ruzuku ya y a asilimia 50% kutoka Serikalini yakiwemo ya viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya wadudu katika Mikorosho ya wakulima hao tangu mei 29 mwaka huu.

Marando aliendelea kufafanua kuwa uteuzi huo ulifanyka katika kikao kilichofanyika mei 8 mwaka huu baada ya kamati inayosimamia zao hilo kuridhika na sifa zilizohitajika kati ya Wazabuni Wanne (4)
wakiwemo Halima Luambano, Mohamed kionjo na Alli Chimwa.

Alisema katika mkataba huo unaomruhusu Namhala kusambaza pembejeo hizo unaonesha kuwa jumla ya Madawa yenye thamani ya shilingi 144,294,600/= yamepangwa kusambazwa kwa Wakulima wa wilaya hiyo zikiwemo Kilo 234,194 za Sulphur ya Unga madawa ya maji lita 6183 zikiwemo lita 2,108 za Mupavil,Lita 1,171 za duduali, lita 1,405 za Faipro na lita 234 za dawa aina ya Rav.
Upande wa Mzabuni huyo aliyeteuliwa na Kamati inayosimamia usambazaji wa Pembejeo za Ruzuku kwa Wakulima wa Korosho Wilayani Tundudru Mkoani Ruvuma Zuberi Rashid Namahala alipo takiwa kuzungumzia maendeleo ya mradi huo alianza kwa kuulalamikia uongozi wa Mfuko unaosimamia
ukuzaji wa zao hilo kwa urasimu na ucheleweshaji wa Madawa ya mgao uliyopangwa kupelekwa kwa wakulima wa Wilaya hiyo.
Aidha katika taarifa hiyo Namahala alidai kuanza kupoteza imani na uongozi wa mfuko huo ambao tayari amekwisha walipa fedha hizo tangu Mei 29 mwaka huu kupia katika akaunti namba 0150237061700 inayomilikiwa na mfuko huo katika Mabenki ya CRDB tawi la Mtwara na toka wakati huo hajakabidhiwa hata mfuko mmoja wa madawa hayo kitendo alicho kitilia mashaka kuwa huenda wanapanga mambo ya kufanyia utapeli wa fedha hizo.
Alisema kufuati hali hiyo ofisi yake ina andaa utaratibu wa kutafuta mwanasheria ili amsaidie kuangali utaratibu wa kukatisha mkataba huo na kudai arudishiwe fedha zake kwa madai kuwa ucheleweshaji huo utamfanya ashindwe kumudu kulipia mkopo wake benki na kumsababishia hasara.
Akiongea kwa njia ya Simu Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza uzarishaji wa Korosho Tanzania Athumani Nkinde mbali na kukiri kupokelewa kwa fedha za mzabuni huyo, alisema kuwa chanzo cha kuchelewa kwa madawa hayo kunatokana na kuangushwa na Mzabuni aliyeteuliwa na Mfuko huo
kampuni ya Export Treding iliyo pewa kazi ya kusambaza Tani 5000 ambayo hadi wanakatisha mkataba Mei 4 mwaka huu ilikuwa imemudu
kuingiza tani 800 tu.
Alisema baada ya kukatishwa kwa mkataba huo Mfuko ulimteua wakala mwingine kampuni ya HAMAS (T) LTD katika kikao kilicho keti Mei 31 mwaka huu na kuahidiwa kuletewa madawa hayo mwishoni mwa mwezi huu.

Kufuati hali hiyo Nkinde pamoja na mambo mengine aliwaomba radhi wakulima hao na akawataka kuwa wavumilivu wakati taratibu za ufuatiliaji wa madawa hayo zikiendelea na akatumia nafasi hiyo
kumuomba Namahala kwenda kuchukua madawa ya maji aliyodai kuwa tayari yapo kwa wingi iIi yasambazwe ili wakulima wapulizie mikorosho yao awamu ya kwanza huku akiahidi kuwa awamu itakayo fuata watapuliza dawa ya Sulpur ya unga waliyo izowea.

Nae Mbunge wa Jimbo la Tunduru kusini alhaji Mtutura Mtutura alipotakiwa kuzungumzia ucheleweshaji wa madawa hayo aliahidi kutoa taarifa sahihi baada ya kuwasiliana na Waziri mwenye dhamana.
Mwisho