Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya SongeaoCharles MhagamaHALI YA USAFI KATIKA MANISPAA YA SONGEA IMESHINDIKANA?Na Stephano Mango,SongeaHALI ya usafi ambayo tulizoea kuiona katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa wa Ruvuma sasa imeanza kutoweka polepole hasa katika maeneo ya ghuba za kuhifadhia takataka na mifereji ya maji katika baadhi ya barabara mjini hapa .Uchunguzi wa kina uliofanywa na Dira ya Mtanzania umebaini kuwa Manispaa ya Songea kuna ghuba nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wakazi na kwamba ghuba hizo zina dalili zote za kuzalisha magonjwa ya kuambukiza hasa kipindi hiki tunapoelekea masika .Baadhi ya wakazi wa Manispaa hiyo wameulalamikia uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kujali afya za wananchi wake kwani pamoja na ghuba zao kujaa takataka na zingine kuanza kuzagaa na kusababisha watoto kuchezea hali inayoweza kupelekea hatari kwa ustawi wao.Kwa sasa hali ya Manispaa hiyo ilivyo haimvutii mtu kuja kupumzika au kufanya shughuli zozote za burudani kutokana na uchafuzi wa mazingira uliokithiri kwenye viunga vya mjini hapa.Hakuna bustani iliyotunzwa vizuri kwa kuvutia hata watalii kupumzika ukiachia wakazi wa mji wa Songea kutokana na mipango mibovu ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo inaonekana ndio chanzo cha uchafuzi wa mazingiraKwani imeshindwa kutenga maeneo ya kuweka bustani za kupumzika wakazi wa Manispaa hiyo wakati wa mchana au wa jioni tofauti na miji mingine ambayo inathamini maeneo hayo muhimu kwa wananchi wake.Hata bustani za miti,maua na mboga mboga zipo chache na hazionekani kiurahisi kutokana na mipango yake mibovu inayosabibisha hewa ya Manispaa kuwa nzito kutokana na uchafu wa mazingira unaoendelea kukithiriNi wazi kuwa swala la usafi wa mazingira katika Manispaa hiyo bado halijatiliwa mkazo kwani wananchi wanajitahidi kukusanya takataka pamoja lakini haziondolewi jambo hili linawakera na kuonekana wazi kuwa mamlaka husika haziwajibikiKwani ili wananchi wawe na afya njema na hatimaye waweze kumudu kazi zao vizuri kwa kutopata magonjwa ya mlipuko ni lazima usafi uzingatiwe katika maeneo wanamoishi.Kila mwaka kumekuwa na taarifa za watu kupatwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kushamiri kwa uchafu unaotupwa hovyo huku ikifahamika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.Licha ya kuzagaa kwa mifuko ya plastiki na makopo mitaani kutokana na kutupwa ovyo na watumiaji wake kutokana na kuzipuuza kanuni na sheria ndogo za Halmashauri au kutozijua kwa wananchi wengiUkipita katika mitaa ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni lazima utakutana na malundo ya takataka ambayo yameoza na kupelekea kutoa halufu mbaya kutokana na uzembe wa watendaji wa Manispaa hiyo.Hali hiyo pia ipo katika Masoko ya Manispaa hiyo kama vile Soko la Manzese,Mfaranyaki,Bombambili,Majengo na Soko kuu la Songea kwani kutokana na watendaji wake kutosimamia sheria na kanuni za usafi katika maeneo hayoKumepelekea wafanyabiashara kutupa taka ovyo na kusababisha harufu mbaya kutokana na kuoza kwa taka hizo ambazo nyingi huwa zile za majimaji ya nyanya,maembe,machungwa,maji yaliyooshewa utumbo wa nyama na vyakula vilivyolala.Ili suala la kuzagaa kwa uchafu katika maeneo ya Manispaa ya Songea libaki historia viongozi wa Serikali hiyo wanapaswa kuonyesha mfano wa kusafisha mazingira kwa vitendo.Endapo Serikali hiyo inataka ifanikiwe katika operesheni ya kuboresha usafi wa mazingira ni lazima waache kuzungumzia usafi maofisini na kwenye majukwaa na badala yake waonyeshe mfano kwa wananchi kwa wao kujumuika nao na kusafisha mazingira.Viongozi waonyeshe mfano kwa wananchi kwa sababu mfumo wa namna hii unafanyika duniani kote ili kuboresha mazingira ,kwani kwa wale viongozi wanaowaelimisha wananchi jukwaani baadae huwafuata katika maeneo yao na kujumuika pamoja katika kusafisha mazingira yao.Serikali inapaswa kubadilika kwa kuchukua suala la usafi wa mazingira kimatendo zaidi na si maneno mengi ambayo hayaleti mabadiliko yeyote katika suala zima la usafiIkiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto nyingi zilizopo ikiwemo za vifaa vya kuzolea taka,uelewa mdogo wa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi,ikiwa na kuziweka wazi kanuni na sheria ndogo za usafi wa mazingira.Ili wananchi waweze kutambua wajibu wao kikamilifu na umuhimu wa utunzaji wa mazingira yao kwa afya na ustawi wao kwani bila kufanya hivyo ufanisi wa jambo hilo unaweza usifikie viwango stahiki.Mwandishi anapatikana Simu 0755-335051 www.stephanomango.blogspot.com |
Friday, April 13, 2012
MKUU WA MKOA MWAMBUNGU UMENENA, NAKUUNGA MKONO KWANI NAMI NIMEWAHI KUANDIKA MAKALA HAYA
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI LIMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wafadhili Walter Reed, wanatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
1. PROGRAMME OFFICER: NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
· Kusimamia na kuratibu shughuli za mpango wa Huduma kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kushirikiana na Mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Mkoa (Tiba)
· Kutekeleza kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa Huduma za Afya Mkoa
Sifa za kuingilia:
- Wenye shahada ya Udaktari (MD) au Stashahada ya Udaktari (AMO) ambaye amehitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Asiwe mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine ya Serikali na Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
2. AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING & EVALUATION OFFICER 1 NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
· Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
· Kuwezesha na kutoa ushauri na tafsiri ya Sera, Mipango, mikakati na miongozo kuhusu taarifa za Afya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya
· Kutekeleza kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Meneja wa Mradi
Sifa za kuingilia:
- Wenye Shahada/Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipango, Uchumi na Takwimu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
3. MHASIBU:
Kazi za kufanya:
· Kufanya kazi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
· Kusimamia shughuli zote za Uhasibu katika Mradi
· Kudhibiti hati za malipo
· Kujibu hoja za Ukaguzi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
SIFA ZA KUINGILIA:
- Awe na Shahada au Stashahada ya Uhasibu kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
4. WATUNZA KUMBUKUMBU NAFASI TANO (5)
Kazi za kufanya:
· Kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Meneja wa Mradi
· Kuandaa na kutunza taarifa /kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Mradi
· Kukusanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Sifa za kuingilia:
- Awe na Shahada au Stashahada, au cheti cha utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Tawala wa Mkoa,
S.L.P. 74,
SONGEA.
AU
Mganga Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 5,
SONGEA.
Subscribe to:
Posts (Atom)