About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, September 2, 2011

WACHAWI WAKUTANA KUPANGA KUMUUA MGANGA WA JADI

                            Frola Ndembo maarufu kwa jina la Binti Ndembo akionyesha miliki yake ambayo inaonekana kuwa tishio kwa waganga wenzake na watu wananao daiwa kuwa ni WACHAWI
 Na Joseph Mwambije,Songea
WATU wanaosadikiwa kuwa wachawi wanadaiwa kufanya vikao viwili usiku vya kumuua Mganga mmoja maarufu Mkoani Ruvuma aitwaye Frola Ndembo ambaye hulisaidia jeshi la Polisi kukamata wahalifu wanaokuja kwake kujizindika.
Wachawi hao watatu akiwemo akiwemo binti wa miaka tisa walinaswa na Mganga huyo anayefanyia shughuli zake kwenye kijiji cha Namabengo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma na kujisalimisha huku wakieleza jinsi shughuli za ushirikina ziavyofanyika.
Mwandishi wa habari hizi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ,Joseph Mwambije alishuhudia mtoto huyo Loveness Mapunda(jina linahifadhiwa)akijieleza kwenye eneo maaalumu kwa Mganga huyo ambalo huitwa Uwanja wa dhambi ambalo Mshirikina hueleza jinsi anavyofanya ushirikina na kutubu kwenye umati mkubwa wa watu unaokuwa umemzunguka.
Akijieleza katika eneo hilo mtoto huyo ambaye ana maendeleo mazuri darasani alisema uchawi alipewa na Bibi yake ambaye alikuwa pamoja naye kwa mganga huyo alisema yeye na Bibi yake huyo walihudhuria  vikao viwili vya Wachawi vya kumuua Mganga huyo lakini hawakuchangia hoja yoyote.
Akisimulia huku akitoa machozi katika Uwanja wa dhambi alisema Bibi yake amemtia muhuri mama yake mzazi kwa ajili ya kumla Krismas ya mwaka huu na kwamba amemuweka yai sehemu za siri jambo linalomfanya aumwe ugonjwa usiojulikana.
Alisema sababu za kufanya kikao hicho ni kutokana na Mganga huyo kuwaumbuanakuwasumbua jambo linalowafanya kushindwakula nyama za watu kwa raha.
 Alijieleza kuwa yeye ni mchawi na huwa anakwenda makaburini usiku na Bibi yake na kwamba alipewa uchawi bila kujijua hivyo anapenda Mganga huyo amuondoe uchawi.
 Kwa upande wake Mganga huyo maarufu kwa jina la Binti Ndembo alijigamba kwamba Wachawi hawawezi kumuua bali atakufa Mungu atakapopenda na kwamba ataendelea kuwaumbua wachawi na Majambazi na wezi.

No comments:

Post a Comment