About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, December 11, 2011

WAKATI WA UCHAGUZI MKUU WA URAIS,WABUNGE NA MADIWANI MWAKA 2010,MGOMBEA MMOJA WA CHAMA FULANI ALIZUNGUKA NCHI NZIMA NA KUWAAHIDI WATANZANIA KUWANUNULIA BAJAJ ZITAKAZOSAMBAZWA NCHI NZIMA VIJIJINI KWA AJIRI YA KUWABEBA AKINA MAMA WAJAWAZITO ILI KUPUNGUZA VIFO VINATOVYOTOKANA NA UZAZI,JE BAJAJ HIZI NDIZO ZILIZOAHIDIWA AU TUSUBIRI ZINGINE?



WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA WAHITIMU WA VETA NCHINI

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya  Nyanda za juu kusini Monica Mbelle

Na Gideon Mwakanosya,Songea

WATANZANIA wametakiwa kutumia bidhaa za ndani zinazotokana na malighafi za hapa nchini badala ya kuendelea  kutumia bidhaa za China ambazo  asilimia kubwa ubora wake ni mdogo na zimekuwa zikahiribika baada ya muda mfupi na kuiletea hasara Serikali.
 
Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na  Mkurugenzi wa VETA Kanda ya  Nyanda za juu kusini Monica Mbelle wakati akizungumza kwenye Mahafali ya 26 ya Chuo cha Ufundi stadi Songea Mkoani Ruvuma .
 
Alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Taifa limeshuhudia bidhaa nyingi zenye ubora mdogo zikitoka nje ya Nchi ukilinganisha na za hapa Nchini ambazo zimekuwa na ubora mkubwa lakini zimekuwa zikikosa soko kutokana na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii na Serikali kwamba bidhaa bora ni zile zinazotoka ng’ambo.
 
‘Tumeshuhudia Ofisi zetu zikiwa zimejaa fenicha za kutoka nje ya Nchi ambazo baada ya mwaka mmoja zinakuwa zimeharibika na Serikali inaingia gharama nyingine kuagiza tena bidhaa hizo wakati tuna mafundi wetu wanaotengeneza bidhaa bora kuliko hizo’alisema na kuongeza kuwa
 
Inatakiwa jamii na Serikali kubadilika na kuwatumia mafundi waliohitimu VETA kwa kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa zao zenye ubora wa hali ya juu tofauti na bidhaa za nje ambazo alidai zina ubora mdogo.
 
Alisema kwa sasa wanawatumia mafundi wao badala ya Wakandarasi kujenga Vyuo kila Wilaya ambapo wamekiteua Chuo cha Ufundi stadi Mpanda kufanya kazi hizo kwa Nyanda za juu kusini na kwa sasa wanajenga Chuo cha VETA Makete na baada ya kumaliza huko watakuja kujenga  madarasa Veta Songea baada ya wanafunzi kuwa wengi.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Songea  Gideon Ole Lairumbe alisema wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika Chuo hicho zikiwemo wazazi kuleta wanafunzi wa darasa la saba wenye uwezo mdogo wa kuelewa masomo na ukosefu wa vitendea kazi.
 
Hata hivyo aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) kuwapa msaada wa Kompyuta nane zenye thamani ya Tsh milioni 3.5 ambazo zilikabidhiwa siku hiyo na  Afisa wa Mamlaka hiyo Deograsias Nyoni ili ziweze kusaidia kwenye mafunzo ya Kompyuta Chuoni hapo ambapo alisema kuwa elimu ya Kompyuta na mawasiliano ni muhimu katika dunia ya leo.
MWISHO

DC WA TUNDURU JUMA MADAHA KATIKA MNYUKANO MKALI NA MBUNGE WA TUNDURU KUSINI ABDALAH MTUTURA

                                                   DC WA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Steven Augustino Tunduru

MBUNGE wa Jimbo la Tunduru Kusini Alhaji Mtutura Abdalah Mtutura amedai kuwa hakubaliani na hataunga mkono tamko la Uongozi wa Serikali ya Wilaya hiyo juu ya zoezi la kupiga marufuku wa magari ya mizigo aina ya CANTER kuchukua abiria.

Alhaji Mtutura alitoa kauli hiyo alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya Oparesheni ya kamatakamata ya magari hayo inayotekelezwa na Jeshi la Polisi Wilayani humo wakidai kuwa magari hayo hayaruhusiwi kubeba abiria na mizigo.

Akifafanua taarifa hiyo Mbunge huyo alisema kuwa msako huo unaendeshwa kwa uonevu mkubwa kwa madai kuwa miundombinu ya Barabara  na mazingira ya  Wilaya hiyo bado hayaruhusu kuwepo kwa mabasi ya abiria yatakayo weza kufanya safari katika maeneo ya Vijiji vyote,

Adhi Mtutura aliishauri Serikali kuweka mikakati ya utoaji wa elimu ya kuwataka madereva wa magari hayo aina ya CANTER kubeba abiria kidogo pamoja na kuwashauri wamiliki wake kuyasajiri ili yapatiwe leseni ya kubeba abiria pamoja na kulipa kodi ili waendelee kutoa huduma kwa wananchi.      

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa  Wilaya hiyo Mkoani Ruvuma waliiomba Serikali kuingilia kati tatizo hilo la kukosekana kwa Usafiri wa kuelekea vijijini na kuhakisha kuwa huduma hiyo inapatikana muda wote ili waweze kuondokana na kero ya upatikanaji wa huduma wakidai kuwa hivi sasa wanapata wakati mgumu wanapotaka kwenda kufuata mahitaji yao.

Miongoni mwa waliopaza sauti zao juu ya malalamiko hayo  ni pamoja na Mwenyejiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tunduru  Kanduru kasim Kanduru, Alli Selemani na Halima Saidi ni miongoni Wananchi ambao walipaza sauti zao baada ya kukosa usafiri kwa siku mbili baada ya Jeshi la Polisi Wilayani humo kuanzisha msako kabambe wa kukamata na kuyaondo kabisa magari ya mizigo ambayo yamekuwa yakibeba abiria hao kutoa Tunduru Mjini kuelekea Vijijini.

Wakati wananchi hao wakipaza sauti zao nao wamiliki wa magari hayo wamelilalamikia Jeshi hilo kwa kitendo hicho cha uonevu unaolenga kudidimiza utendaji wao kibiashara na kuwakwamisha kulipa mikopo waliyo nunulia magari hayo.

Wakiongea kwa masharti ya kuomba majina yao yasitajwe kwenye mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com  kwa hofu ya kushughulikiwa wafanya biashara hao walisema kuwa mbali na uonevu wanaofanyiwa na Jeshi hilo wa kutozwa faini isiyo pungua Tsh. 150,000 pindi wanapo kamatwa pia mpango huo unalenga manufaa ya wajanja wachache kutafuta Fedha za sikuku za mwisho wa mwaka.

Walisema kama zoezi hilo lingekuwa ni halali lilitakiwa kufanyika nchi nzima ama ndani ya Mkoa mzima lakini cha kushangazo zoezi hilo limefanyika Wilayani Tunduru pekee hali inayo onesha ulakini katika uhalali wake

Akiongea kwa njia ya Simu ya kiganjani Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Juma Madaha mbali na kukiri kuwa magari hayo yamezuiliwa kuendele kutoa huduma hiyo ,wananchi walisema hatua hiyo ni sawa na kukatika kwa mawasiliano kati ya wananchi wa Tunduru Mjini na vijijini hasa kwa wasio kuwa na uwezo wa kukodi Pikipiki ambaapo hatima yao haijulikani walidai kuwa zoezi hilo ni agizo la Serikali na linatakiwa kutekelezwa nchi nzima.

``Ni kweli zoezi hilo lipo na linaendelea, lakni hebu fanya mawasiliano na Kamanda wa Polisi wa Wilaya kwa ufafanuzi zaidi`` alisema Dc, Madaha na kuongeza kuwa yeye alipatiwa taarifa hizo na Kamanda huyo kuwa agizo hilo linatekelezwa baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda katika maelezo yake alikiri kuwa zoezi hilo ni halali na kwamba tayari wamiriki wa magari hayo walikwisha pewa maelekezo ya kufanya mabadiliko kwa kununua mabasi ili waendelee kutoa huduma hiyo miezi mitatu iliyo pita lakini walikaidi.
 Mwisho