MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na,Augustino Chindiye,Tunduru
WAKATI Serikali ikiwa imetoa tamko la kuwafutia Leseni Wanunuzi wa
Korosho nchini, Wakulima wa zao hilo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma
wamehoji hatima ya Soko la Korosho zao.
Hayo yalitokea katika kikao cha wadau wa Korosho kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Kikuu cha Wakulima (TAMCU) na kuwashirikisha Waandishi na Wenyeviti wa Vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo na wakaituhumu Serikali ya awamu ya nne kuwa imekuwa butu katika kutoa maamuzi hali ambayo inawafanya Wanachi kukata tamaa juu ya utendaji wake.
Wawakirishi wa Wakulima kutoka Chama cha Msingi Litungulu Mohamed
Matoto na Yasini Masiano wa Chichilimbe walisema kuchelewa kutolewa
kwa maamuzi kunako fanywa na Serikali kumewafanya viongozi wa vyama
vya msingi kuishi katika hofu ya kufanyiwa fujo na wakulima wao.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Wakulima Wa
Korosho (TAMCU) Mohamed Katomondo mbali na kupongeza hatua zilizo
chukuliwa na Serikali kwa kunukuu kauli ya Makampuni hayo
kunyang`anjwa Leseni bila majadiliano iliyotolewa na Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa katika
tamko hilo hakukuwa na kipengele wala maelekezo yaliyozungumzia hatima
ya Korosho za wakulima.
Aidha katika taarifa hiyo Katomondo alionesha mashaka ya kuendelewa
kwa zao hilo kutokana na wakulima wengi kukatishwa tamaa na utaratibu
wa mfimo wa Stakabadhi ghalani wakidai kuwa mfumo huo unanyonya nguvu
zao.
Akitoa taarifa ya mdororo wa Korosho hizo Meneja wa Chama Kikuu cha
Ushirika wa Wakulima wa Korosho Wilayani Tunduru (TAMCU)Imani
Kalembo alisema kuwa katika msimu wa Mwaka 2011/2012 chama hicho kupitia
vyama vya msingi vya wakulima takwimu zinaoneshja kuwa uzalishaji
umeongezeka kutoka kilo 4,135,042 za mwaka 2010/2011 hadi kilo 7,570,000.
Kalembo aliendelea kufafanua kuwa hadi kufikia Februari 29 mwaka huu
takwimu zinaonesha kuwa Korosho zilizopokelewa Maghalani ni Kilo
6,842,446 na kilo 641,230 zipo katika maghala ya watu binafsi na
zingine zipo nje ya ofisi za chama hicho na kilo 86,324 bado zipo
mikononi mwa wakulima huku takwimu hizo zikionesha kuwa ni kilo
1,890,384 tu ndizo zilizouzwa katika mnada mmoja kati ya minada tisa
iliyofanyika hali inayotishia chama hicho kushindwa kulipa malipo ya pili ya wakulima ambapo TAMCU inadaiwa Jumla ya Shilingi 2,441,870,350/= .
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa deni hilo limetokana na chama
hicho kununua jumla ya Kilo 6,976,821 ambazo Chama hicho kupitia vyama
vya msingi vimeweza kuzilipia kwa asilimia 70% pekee, sambamba na Deni
la Shilingi 608,260,000 zilizotokana na Mkopo wa kilo 506,855 za Korosho za zilizo kopeshwa na wakulima kwa vyama vya Msingi.
Kalembo aliendelea kueleza kuwa wakati hayo yakiendelea Chama
hicho pia kinakabiliwa na changamoto ya Chama kushindwa kununua jumla
ya kilo 86,324 zenye Dhamani ya Shilingi Milioni 17,264,800 ambazo
bado zipo mikononi mwa wakulima wa zao hilo hali inayo endelea
kuwakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Mjini Songea Katibu
Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Wilgisi Mbogoro,
alisema takwimu za Korosho zote zilizokwama baada ya wanunuzi
kutunisha misuli kuzinunua ni kilo 72,978,340 zenye thamani ya
shilingi Bilioni 113.7
Wakitoa salamu za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha namlajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoani Ruvuma WatsonNganiwa walisema kuwa msimamo wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Korosho zote zinanunuliwa kutoka kwa wakulima na wakatumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima kuwa na subira wakati taratibu za mchakato wa kufanikisha hayo zikiendelea.
Mwisho