Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Cyril Chami akisalimiana na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mbinga Lugano Mwampeta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya maonyesho mjini Mbinga
Mgeni rasmi katika maonyesho ya nane ya Sido kanda ya kusini,Waziri wa viwanda na biashara Dkt Cyril Chami akizindua maonyesho hayo katika banda la SIDO kwenye viwanja vya CCM mbinga,wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo.Maonyesho hayo yameanza septemba 9-12 na kushirikisha wajasiliamali 200 kutoka katika mikoa ya mbeya,Lindi,Mtwara,Iringa na Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma(mwenye suti nyeusi) akikagua banda la wajasiliamali JKT Mlale kabla ya mgeni Rasmi ajatembelea banda hilo na kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ya Serikali,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa habari na Masoko Sido makao makuu Jannet Ninja
Mkurugenzi wa habari na Masoko wa Sido Jannet Ninja akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Christine Ishengoma (mwenye suti nyeusi)sehemu atakayoanza mgeni rasmi kukagua mara atakapowasili kwenye viwanja hivyo vya maonyesho,wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya MBINGA Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa,wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT)wilaya ya Mbinga Lusiana Ndunguru
Askari wa Skauti akimvesha skafu Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami ikiwa ishara ya kumkaribisha katika viwanja vya maonyesho,wa kwanza kushoto ni Mbune wa jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo,wa pili ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma
Mgeni rasmi akipata maelezo katika banda la muungano wa wajasiliamali vijijini(MUVI) alipotembea katika banda hilo jana
Mgeni Rasmi akiangalia kwa umakini ingini ya mashine ya kusaga kutoka kwa wajasiliamali wa Mbeya alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho
Mjasiliamali wa usindikaji na uuzaji wa vinywaji aina mbalimbali ikiwemo Mvinyo kutoka Seedfarm Songea chini ya Kampuni ya Jeim Product Magdalena Talimo akimuonyesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni yake Mgeni Rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami alipotembelea banda la kampuni hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa akiwa amepumzika kutokana na uchovu wa kuzunguka kukagua mabanda ya wajasiliamali na kupata kahawa katika banda la MCCCO
Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta SONGEA akimpa maelekezo mgeni rasmi Dkt Chami ya namna mashine ya kusukia nywele inavyofanya kazi alipotembelea banda hilo
Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa Ruvuma wakimsindikiza Mgeni rasmi waziri wa viwanda na biashara Dkt Cyril Chami kuelekea jukwaani na kuhutubia wajasiliamali waliopo kwenye viwanja vya CCM wilayani Mbinga
Mgeni Rasmi Dkt Chami akiangalia kwa umakini kikundi cha ngoma ya chioda kinavyotumbuiza maonyesho hayo
Mgeni rasmi Dkt Chami akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga kanali Edmund Mjengwa mara baada ya kumaliza kukagua mabanda yote ya maonyesho(PICHA ZOTE NA STEPHANO MANGO)
WAZIRI Dkt CHAMI AZIANGUKIA TAASISI ZA FEDHA NCHINI
Na Stephano Mango,Songea
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt .Cyril Chami ameziangukia taasisi za fedha nchini kuona umuhimu wa kuweka masharti nafuu ya mikopo kwa wajasiliamali ili waweze kukopa fedha kulingana na michanganuo ya miradi yao kwa lengo la kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla
Wito huo aliutoa jana wakati akihutubia mamia ya wajasilimali waliojitokeza katika uzinduzi waa maonyesho ya nane ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(Sido) kanda ya kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ccm Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Dkt Chami ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa taasisi za fedha nchini zinatakiwa kubuni utaratibu wenye masharti nafuu wa kuwakopesha wajasilimali wadogo na wakati kwani uzoefu wan chi nyingi unaonyesha kuwa wajasiliamali wadogo na wakati ndio walipaji wazuri wa mikopo
“Natoa wito kwa taasisi hizo kushirikiana na Sido pamoja na vyombo vingine vya kuendeleza wajasiliamali wadogo na wakati ili ziweze kubuni mbinu muafaka za kuwakopesha wajasiliamali na kutoa elimu itakayowawezesha wajasiliamali kukopesheka’alisema Dkt Chami
Alisema kuwa wajasiliamali wanakabiliwa na changamoto nyingi katika shughuli zao ikiwemo changamoto ya kutokujua kusoma vipimo hasa kwa wale wanaojihusisha na ujasiliamali wa mazao ya kilimo na misitu kama vile uuzaji wa mahindi,maharage,viazi,alizeti,ufuta na asali wamekuwa wakipata hasara sana na kurudisha nyuma ukuaji wa uchumi kwa mjasiliamali hivyo aliwataka wakala wa vipimo kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wazalishaji hao ili kuweza kuleta ustawi na maendeleo sawa kwa wananchi wote
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Sido Michael Raizer alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuwawezesha wananchi kufahamu bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vidogo nchini ili ziweze kuwasaidia katika harakati zao za kukuza uchumi
Raizer alisema kuwa maendeleo ya sekta ya wazalishaji wadogo na wakati ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi endelevu na kuondoa umaskini hivyo licha ya serikali kuandaa sera ya ununuzi 2004 bado sera hiyo haijasaidia wazalishaji wadogo kwani sera hiyo haizazingatia umuhimu wa kukuza soko la ndani hasa kukuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vidogo
Awali Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa wajasiliamali wa mikoa ya kanda ya kusini wanatakiwa kuandaa mikakati ya kutumia fursa za ukanda wa maendeleo wa mtwara ili kuweka kitovu cha bidhaa zinazozalishwa kutokana na rasilimali zilizopo kwenye maeneo yetu ili wageni watakapokuja waweze kuona kuwa mikoa hii inatumia kikamilifu rasilimali zilizopo kuanzisha na kuendesha viwanda,kuongeza ajira na kipato
Aidha Dkt Ishengoma aliwataka wajasiliamali kuongeza ubora wa bidhaa na kuzalisha bidhaa kwa wingi kwani bidhaa bora zinauzika kwa haraka hivyo ni muhimu kuelewa kuwa tatizo la bidhaa zetu na nchi za nje siyo kukosa soko bali ni uwezo mdogo wa uzalishaji na usiozingatia mahitaji ya soko husika na ubora wa bidhaa
MWISHO
No comments:
Post a Comment