Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Dereva wa Kampuni ya Sinohydro inayotengeneza barabara kwa kiwango cha lami kutoka Songea kwenda Mbinga Said Ibrahim kwa tuhuma za kumnyang’anya Simu tatu za mkononi zenye thamani ya shilingi laki 6 na kumjeruhi kwa kumpiga na nondo kichwani Majianxin mwenye umri wa miaka (40) ambaye ni raia wa China mfanyakazi wa Kampuni hiyo ya ujenzi.
Kamanda wa Polisi wa Moka wa Ruvuma Michael Kamuhanda ameuambia mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ kuwa tukio lilitokea jana majira ya saa nane mchana kwenye eneo la Mkako Wilayani Mbinga.
Amesema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Majianxin mwenye asili ya kichina akiwa kwenye shughuli zake za ujenzi wa barabara majira ya saa nane mchana alinyang’anywa simu tatu za mkononi na dereva wa Kampuni ya Sinohydro aliyejulikana kwa jina la Said Ibrahimu.
Amefafanua kuwa inadaiwa kabla ya Ibrahimu kumnyang’anya simu hizo alichukua nondo na kumpiga Majianxin na badae alikimbia na kutokomea kusikojulikana na kwasasa hivi Majianxin amepata majeraha makubwa kichwani na anaendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya Wilaya Mbinga.
Ameeleza zaidi kuwa Majianxin alinyang’anywa simu tatu ambapo kati ya hizo mbili ni za aina ya Samsung na nyingine ni aina ya nokia zote zikiwa na thamani ya shilingi laki 6.
Hata hivyo Kamuhanda alisema kuwa kufuatia tukio hilo kutokea kwasasa hivi Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea kumsaka mtuhumiwa ambaye anadaiwa kuwa ametorokea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
MWISHO
No comments:
Post a Comment