RC Ruvuma Said Mwambungu
DC Mbinga Kanali Edmund Mjengwa
Mbunge Mbinga Magharibi Kapteni John Komba
Na Stephano Mango,Nyasa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amechangia shilingi milioni tatu katika kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika shule ya Sekondari ya Lituhu iliopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma ili kukomesha utoro na mimba kwa wasichana wa shule hiyo
Akizungumza na Mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ Ofisini kwake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Lituhi Benjamin Mwingira alisema kuwa wananchi wa kaya ya Lituhu wakiwemo wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo kwa pamoja wameridhia mpango wa ujenzi wa Hosteli ya wasichana ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi wa kike kuondokana na tatizo sugu la utoro na upatikanaji wa mimba
Mwingira alisema kuwa kwa sasa wananchi hao tayari wamefyatua na kuchoma tofari laki sita zitakzotumika kwenye ujenzi huo ambapo kazi iliyobaki ni kuanza kujenga Hosteli hiyo kwa kasi kubwa mara baada ya mvua kusimama kunyeshaAmewahimiza wazazi kuthamini michango iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni Mstaafu John Komba kwa kuhakikisha kuwa jingo hilo la Hosteli kwa wasichana linakamilika kwa wakati ili wanafunzi wa kike 200 kati ya wanafunzi 403 wa shule hiyo waweze kulitumia
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni Mstaafu John Komba alisema ametoa bati 50 na michango midogomidogo kwa ajili ya kuezekea hosteri hiyo na pia amewashukuru Rais Kikwete kwa kuwachangia shilingi milioni tatu,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kwa kutoa mifuko 50 ya saruji na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ametoa mifuko 10 ya saruji
Komba aliwaomba wananchi wa kata ya Lituhi na wananchi waliopo nje ya kata ya Lituhi wakiwemo waliowahi kusoma shule hiyo kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi huo ambao unaboresha miondombinu ya shule hiyo na kupelekea utolewaji wa elimu bora
MWISHO
No comments:
Post a Comment