About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, December 14, 2011

JAY BLACK MSANII CHIPUKIZI ANAYEIBUKIA KWA KASI KWENYE MUZIKI WA BONGO FREVA

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya James Damian Jay Black

JINA lake ni James Damian maarufu kwa jina la Jay black ni mwanamuziki wa muziki wa bongo fleva , alianza rasmi kujishughulisha na kazi hii mwaka 2006 ingawa hakufanikiwa kurekodi kama anavyoendelea kuongea na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com
Msanii huyo James Damian anafafanua kuwa Mnamo mwaka 2008 alibahatika kuingia studio na kurekodi nyimbo iliyofahamika kwa jina la MAISHA kwenye Albam ambayo ilikuwa na nyimbo nne ambazo ni Mashamsham, na Maisha japo hazikubahatika kuvuma, na mnamo mwaka 2009 alikutana na Mr. T muandaaaji wa muziki studio ya Gita music  iliyopo songea mjini na kufanikiwa kurekodi nyimbo iliyokwenda kwa jina la WANGU DUU.

Amesema kuwa  2011 alifanikiwa kuitolea video nyimbo hiyo katika studio za Fm Production chini ya muandaaji Geofrey Mhagama wa Songea Mjini  na hapo ndipo mafanikio yalipoanza kuonekana kwani nyimbo imebahatika kuchezwa katika vituo tofauti tofauti vya redio na televisheni za hapa nchini.
Amebainisha zaidi kuwa hivi karibuni mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu anatarajia kuachia audio na video itakayofahamika kwa jina la ATUPELE BINTI MWAFRIKA iliyoandaliwa na Prodyuza Mr. T wa studio ya Gita records na baada ya hiyo itafuatiwa na nyimbo itakayoenda kwa jina la MAPENZI NA SHULE  ambayo hiyo nyimbo imejaribu kuongelea hali halisi inayowakuta wanafunzi na wanazuoni wanao ingia katika mapenzi wakiwa masomoni.
Amesema kuwa Shoo yake kubwa aliyowahi kuifanya na kuwavutia Wapenzi wengi wa Muziki wa Kizazi kipya  ni Miss Mbinga ilifanyika kwenye ukumbi wa Umoja wa Vijana (UVIKAMBI) uliopo Mbinga Mjini na Miss Ruvuma 2011 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Songea Parokia ya Bombambili Mjini Songea.
Msanii huyo James Damian anaeleza kuwa  amejitokeza kwenye safu hii kuomba support kwa wadau mbalimbali hapa nchini waweze kumsaidia hasa kimawazo ili aweze kutoka hapa alipo hadi hatua nyingine ya kimuziki.
Amesema kuwa Elimu yake ya sekondari amemaliza mwaka 2007 katika shule ya sekondari ya St. Agrey Mbeya na mwaka 2009 alijiunga na chuo cha Maendeleo ya jamii kilichopo Mlale Wilaya ya Songea na amehitimu Elimu ngazi ya Cheti Mwaka huu kwa sasa yupo mtaani akiangalia upande wa pili wa maisha unaendaje kwani msaada wake mkubwa katika maisha yake ni mama yake mzazi Suzan Fussy ndio tegemeo lake ambaye Kabila lake ni Mndendeule Mzaliwa wa Kijiji cha Hanga Kilichopo Wilayani Namtumbo na baba yake Mzazi ni Damian whiter Mashale mzaliwa wa Rombo Mkoani Kilimanjaro ambapo amedai kuwa yeye mwenyewe James Damian alizaliwa Octoba 3.1988 katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Songea na ni mtoto wa Mwisho kati ya watoto watatu wa  familia yao .
Msanii huyo wa Kizazi kipya anamaliza kusema kuwa anapenda kuwaeleza Watanzania kuwa amani na upendo ndio nguzo imara katika maisha na usije ukamdharau mtu yeyote kwani hujui wapi mtakutana na usijeukamtendea ubaya mwenzako kwani tangu Dunia hii iumbwe na mwenyezi Mungu Milima iliyopo kwenye Dunia hii haijawahi kukutana lakini Binadamu wanaweza wakapotezana kwa muda mrefu lakini baadaye wanaweza wakakutana.
Kwa Wadau watakaoonyesha nia ya kutaka kumsaidia msanii huyo Mchanga wa Muziki wa Kizazi kipya aliyepo Mjini Songea kwa Mawasiliano simu na. 0657784199 email. jayblack4real@gmail.com .

No comments:

Post a Comment