Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
Na, Augustino Chindiye Tunduru
VIONGOZI wa kuchaguliwa na waliopewa mamlaka ya kulitumikia Taifa wameombwa kuitumikia Jamii kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu vinginevyo kuna hatari ya amani hiyo inayojivuniwa na taifa letu kutoweka.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- Masasi Castory Msemwa wakati akiongea na waamini waliohudhulia katika Misa takatifu ya kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo ya Noeli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Xavery mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo kupitia Mahubiri hayo Askofu Msemwa alisema kuwa pamoja na Viongozi hao kufahamu hayo lakini wamekuwa walafi hali ambayo imekuwa ikiwasukuma kuwatesa Wananchi waliowapa nyadhifa hizo .
Alisema mbali na hali hiyo kuonekana wazi kwa Viongozi wa Serikali lakini pia matukio kama hayo yamekuwa yakiwakumba viongozi wa Dini ambapo wamekuwa wakipenda kujinufasha ili waendeelee kuongeza furaha mioyoni mwao kwa kujipangia marupurupu yao wenyewe bila kuwajali wengine na kuiacha jamii ikiteseka bila misaada yao.
Askofu Msemwa akatumia nafasi hiyo kuhimiza upendo miongoni mwetu na kueleza kuwa endapo upendo utaendelea kutoweka kuna hatari ya amani tunayo jivunia kumomonyoka na kuipeleka nchi yetu pabaya.
Katika hutuba hiyo pia Askofu Msemwa akaikumbusha jamii kuiga mwenendo wa mwasisi wa Taifa la Watanzania Mwenyeheri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtumishi wa Mungu Sister Bernadeta wa Jimbo la Perahimo ambaye amekuwa gumzo kubwa kutokana na watu wengi kwenda kuomba katika kaburi lake na kufanikiwa.
Alisema Sister Bernadeta alitangazwa hivi karibuni kuwa mtumishi wa Mungu ukiwa ni mchakato wa kufikia nafasi ya Mwenyeheri na kongeza kuwa mapendo ya kweli katika jamii yao ndiyo yaliyowafanya waendelee kukumbwa na jamii yao .
Mwisho
No comments:
Post a Comment