Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya,Songea
MTU mmoja mkazi wa eneo la kiblang’oma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea amekufa papo hapo kwa kupigwa risasi kichwani na walinzi wa shirika la umeme Tanzania (Tanesco) baada ya kujalibu kutaka kuiba mafuta aina ya Diesel akiwa na wenzake sita ambao wanazaniwa kuwa ni majambazi ambapo mmoja kati yao amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi mgongoni na mguuni na sasa amelazwa katika Hospital ya mkoa Songea.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea januari 5 mwaka huu majira ya saa 7 usiku eneo la power station ya Tanesco lililopo kibrang’oma nje kidogo ya Lizaboni Songea mjini.
Kamanda Kamhanda amemtaja aliye uawa aliyefahamika kwa jina moja la Emmanuel na aliye jeruhiwa ametajwa kuwa ni Solomoni Kilowoko (23) mkazi wa eneo hilo ambaye hali yake ni mbaya na kwa sasa yupo katika Hospital ya Serikali ya mkoa amelazwa.
Amebainisha zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio katika eneo la kibrang’oma ambako kuna power station ya Tanesco kundi la watu saba wanaodaiwa kuwa ni majambazi huku wakiwa wameshika mikononi mapanga na nondo walivunja uzio wa power station hiyo wakiwa na lengo la kutaka kuiba mafuta aina ya Diesel na vitu vingine vilivyokuwa katika eneo hilo.
Alisema kuwa kundi hilo la majambazi baada ya kufanikiwa kuvunja uzio waliingia ndani ya eneo la power station kisha walianza kuyabeba mapipa ya mafuta ambayo yalikuwa ndani ya uzio wa shirika hilo .
Alieleza zaidi kuwa watu wawili kati ya saba wanaodaiwa kuwa ni majambazi ndio walitangulia kuingia kwenye eneo hilo huku wengine watano wakiwa nje ya uzio na baadae walinzi waliokuwa zamu wa shirika hilo ambao waliokuwa na silaha aina ya short gun waliwaona na kuanza kuwafyatulia risasi ambapo Emmanuel alipigwa na risasi kichwa na kufa papo hapo na Kilowoko alipingwa risasi mgongoni na mguuni na alifanikiwa kukimbia kwenye eneo la tukio pamoja na wenzake watano waliokuwa nje ya uzio.
Alifafanua zaidi kuwa polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo hilo ambako walianza kuwasaka majambazi hao na baadae walifanikiwa kumkamata Kilowoko akiwa amelala nyumbani kwa Athumani Nchimbi ambaye anadaiwa kuwa ni mmoja wa majambazi waliohusika kwenye tukio hilo .
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka majambazi hao watano ambao wanadaiwa kutoroka baada ya tukio kutokea na kwamba wananchi wameombwa kuonyesha ushirikiano mzuri na polisi endapo watakapo waona majambazi hao waliotoroka watoe taarifa kwenye vyombo vya dola kwani wanafahamika.
MWISHO
No comments:
Post a Comment