About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, January 4, 2012

KINGONGWE CHA MNYONGA MJUKUU WAKE NA KIJANA AMBAKA MAMA YAKE MZAZI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Mwandishi Wetu, Songea
MWANAMKE mmoja Mary Michael (65) mkazi wa eneo la Ruhuwiko katika Halmashauli ya Manispaa Songea mkoani Ruvuma ametiwa mbaroni na Polisi kwa tuhuma ya kumyonga mjukuu wake aitwaye Fotinata Komba (14) mkazi wa eneo hilo.
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana ofisi kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea desemba 31 mwaka jana huko eneo la Ruhuwiko Manispaa Songea.
Kamuhanda ameeleza kuwa Fotinata kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na maradhi yake mwilini na alikuwa anauguzwa na bibi yake aitwaye Mary ambaye inahofiwa kuwa alifikia kukata tamaa baada ya kumuuguza kwa muda mrefu
Alisema kuwa siku hiyo ya tukio inadaiwa kuwa Fotinata aliitwa na bibi yake Mary na kuanza kumfunga kamba shingoni na kisha kumning’iniza kwenye mti na kumsababishia Fotinata kufariki dunia na baadaye polisi ilipata taarifa kwa raia mwema ambapo walipokwenda kwenye eneo la tukio wakiongozana na Daktari walimkuta Fotinata amening’inizwa kwenye mti.
Alisema kuwa Askari polisi wakiwa kwenye eneo la tukio hilo na kuwahoji baadhi ya watu ambao ni majirani walifanikisha kumkamata Mary ambaye kwa sasa anahojiwa na polisi na kwamba baada ya kukamilisha mahojiano hayo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Mwisho
TUKIO JINGINE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
MTOTO AVUNJA MLANGO NA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI AKIWA AMELALA
Na Mwandishi Wetu, Songea

JESHI la polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Frank Jota (26) mkazi wa kijiji cha Litisha Wilayani Songea kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi mwenye umri miaka 54 ambaye jina lake limehifadhiwa wakati amelala nyumbani kwake majira ya saa za usiku.
Kamanda wa Polisi Koa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea januari mosi mwaka huu huko katika kijiji cha Litisha kilichopo nje ya mji mdogo wa Peramoho.
Amesema kuwa siku hiyo ya tukio majira ya saa za usiku Jota alikwenda nyumbani kwao ambako alimkuta mama yake mzazi akiwa amelala na baadaye alianza kutafuta namna ya kuingia kwenye nyumba hiyo ambayo mlango wake ulifungwa na komeo kwa ndani.
Amefafanua zaidi kuwa Jota baada ya kuona mlango umefungwa kwa komeo kwa ndani aliamua kuuvunja mlango wa nyumba hiyo kisha aliingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba alicholala mama yake mzazi ambaye jina lake limehifadhiwa.
Amesema kuwa Jota akiwa kwenye chumba ambacho mama yake alikuwa amelala alianza kumtishia kwa kisu alichokuwa ameshika mkononi na baadaye alimkaba shingo na kufanikiwa kumvua ngo ya ndani aliyokuwa amevaa kisha alianza kufanya naye mapenzi.
Amebainisha zaidi kuwa wakati Jota akiendelea kufanya mapenzi na mama yake watu waliokuwa jilani na tukio walisikia kelele za mtu akipiga mayowe na walipofika kwenye eneo hilo la tukio waliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Jota akitokea kwenye chumba alicholala mama yake na baadaye alipowaona watu alijalibu kukimbia lakini majirani hao walifanikiwa kumkamata na kumpeleka kituo kidogo cha polisi cha peramiho.
Hata hivyo kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Kamuhanda ameeleza kuwa polisi baada ya kumuhoji mtuhumiwa amekili kutenda kosa hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.
 Mwisho.

No comments:

Post a Comment