About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, January 13, 2012

WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI

Na,Gideon Mwakanosya, Songea
WATU wawili wamekutwa wakiwa wamekufa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika matukio mawili tofauti mkoani Ruvuma likiwemo mkazi mmoja Andrea Hyera  (35) mkazi wa kijiji cha Litembo Wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma amekutwa akiwa amekufa kwa kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasio fahamika na mwili wake kutupwa kando ya Barabara itokayo Litembo kwenda Kijiji cha Mbungu.
Habari zilizopatikana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda zimesema kuwa tukio hilo lilitokea januari 10 mwaka huu majira ya saa 7: 00 mchana huko katika kijiji cha Mtambotambo kilichopo wilayani humo.
Kamanda Kamuhanda amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Hyera alikutwa ameuawa na watu wasio fahamika ambapo mwili wake ulikuwa na majeraha kichwani ambayo yanahashiria kuwa yanatokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.
Amebainisha zaidi kuwa inadaiwa mwili wa Hyera ulikutwa kandokando ya barabara na watu walio kuwa wakipita kwenye eneo hilo ambao ndio walio toa taarifa kwenye Serikali ya Kijiji hicho.
Amesema kuwa uongozi wa Serikali ya Kijiji baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walikwenda kwenye eneo la tukio na baadaye taarifa ilitolewa Polisi kituo kidogo cha Litembo ambao waliwasiliana na Polisi wilaya ya Mbinga.
Ameeleza zaidi kuwa Askari Polisi wakiwa wameongozana na Mganga walikwenda kwenye eneo la tukio na kuukuta mwili wa Hyera ukiwa kandokando ya barabara itokayo Litembo kwenda Kijiji cha Mbungu huku ukiwa na majeraha kichwani ambayo yanadaiwa kuwa yalisababisha kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi bado inaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na mara utakapo kamilika na kuwabaini watuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa.

WAKATI HUO HUO ********* Mtu mmoja Oswadi Mgele (65) mkazi wa Kijiji cha Ugano kilichopo Kata ya Kambarage Wilayani mbinga amekutwa akiwa ameuawa na watu wasio fahamika huku mwili wake ukiwa na majeraha kichwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea januari 10 mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ugano wilayani mbinga.
Amesema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu walikuwa wakipita njia hafla walimwona mtu amelazwa kando ya barabara huku akiwa na majeraha kichwani ndipo waliutafuta uongozi wa serikali wa kijiji hicho kwa kuwajulisha kuwa kunamtu kauwawa na watu wasio fahamika na polisi walipewa taarifa kisha walifika kwenye eneo la tukio ambao walifuatana na daktari ambaye walisibitisha kweli Mgele ameshauwawa kwa kupigwa na kitu kichwani.
 Kamanda kamuhanda amefafanua kuwa Mgele kabla ajauwawa inadaiwa kuwa alikuwa akituhumiwa kijijini hapo na wanakijiji wenzake kuwa ni mshirikina hivyo inahofiwa kuwa chanzo cha mauwaji kinahusishwa na imani za kishirikina hata hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi na kuhusiana na tukio hilo.

1 comment:

  1. Hapa Mitambotambo ndio kijijini kwangu. Nimeshtuka sana kusikia habari hii ya kuuawa mtu hapo. Ni aibu sana. Natoa pole kwa ndugu na jamaa.

    Kijiji cha Ugano, kwa masimulizi ya wahenga, ndio chimbuko la sisi akina Mbele wa u-Matengo. Taarifa hizi za mauaji na imani za ushirikina, na fedheha nyingine.

    Kwa hivi, najikuta nimesongwa pande zote mbili, na masuala haya ya kusikitisha na kuaibisha. Tungojee taarifa za uchunguzi wa matukio haya.

    ReplyDelete