About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, March 1, 2012

DEREVA WA ROLI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KATWILA ASAKWA NA POLISI KWA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA YEBOYEBO

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Dereva aliyefahamika kwa jina moja la Katwila aliyekuwa akiendesha gari lililokuwa likitoka Songea mjini kwenda Dar es salaam ambalo limedaiwa kuigonga pikipiki na kusababisha kifo cha mwendesha pikipiki hapohapo katika eneo la Bombambili Manispaa ya Songea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amemtaja aliyekufa kuwa ni Yassin Ally (32) ambaye ni mfanya biashara maarufu Songea Mjini na ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00  jioni huko katika eneo la bombambili kwenye barabara itokayo Songea kuelekea Njombe.
Amefafanua zaidi kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 707 AJA aina ya Skania ambalo lilikuwa lina tela lake lenye namba T 719 AHL ambalo lilikuwa likiendeshwa na Katwira ambaye alitoroka pasipojulikana mara tu baada yakutokea ajali hiyo.
Amesema kuwa gari hiyo inadaiwa kuwa iliigonga pikipiki yenye namba za usajili T 369 ARQ aina ya Sanlg iliyokuwa ikiendeshwa na Yassini Ally ikitoka Msamala kwenda Songea mjini na kumsababishia kifo chake hapohapo.
Kamuhanda amesema kuwa kwa sasa hivi polisi inaendelea kumsaka Dereva huyo na kwamba mara atakapo patikana taratibu zitaandaliwa za kumpeleka mahakamani ili kuweza kujibu mashtaka yatakayo mkabili na chanjo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni mwendo kasi wa roli hilo ambalo lilimsababishia dereva kushindwa kumudu msikani wa roli hilo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment