HOTUBA YA KUFUNGA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI KONGANO
Chini ya Pan African Competitiveness Forum – Tanzania Chapter
Tarehe 01.03.2012
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume Sayansi na Teknolojia
Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Kongano Bunifu (Innovative Clusters)
Washiriki Wa mafunzo haya,
Wana habari, Mabibi na Mabwana
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza washiriki wote kwa kutumia muda wenu ilikuweza kushiriki mafunzo haya ambayo yalianza tarehe 27Feb mpaka leo hii tarehe 1March2012. Najua ni jinsi gani unahitajika kiakili ili uweze kupata manufaa yaliyolengwa. Kama nilivyofundishwa mimi, mafunzo haya yanalenga kukuza uwezo wenu katika kuhamasisha na kuanzisha ushirikiano kati ya sekta binafsi, serikali na wanataaluma katika kongano mahsusi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini kwetu. Katika nchi nyingi ushirikiano huu umekuwa kichocheo kikubwa cha ubunifu ambao husaidia katika kutoa bidhaa zenye viwango na sifa zinazoweza kuhimili ushindani ndani na nje ya nchi.
Ndugu washiriki, nimefahamishwa kuwa mmeshiriki mafunzo haya kwa moyo wote na kuonyesha kuwa mnania na mmedhamiria kutumia ujuzi mlioupata hapa katika kuimarisha kongano bunifu ambazo ziko katika mazingira yenu mnakofanyia kazi.
Nimeambiwa kuwa ofisi ya waziri mkuu ndio ilifungua mafunzo haya hasa kutokana na uhusiano wa karibu ulioko kati ya madhumuni ya kuendeleza Kongano na mikakati iliyoko katika idara ya maendeleo ya sekta binafsi.
Ndugu washiriki wa warsha hii, napenda kuwaambia kwamba kongano bunifu zinauwezo mkubwa wa kupunguza umaskini na kutoa nafasi nyingi za kazi kwa jamii. Vilevile Kongano hizi huleta mahusiano ya karibu sana kati ya wanachama wa kongano na wadau wengine wa maendeleo kama vile wanataaluma,sekta binafsi na serikali.
Nyie mliofuzu mafunzo haya leo hii nakupewa vyeti,mna majukumu makubwa ya kuhakikisha kwamba lengo la mafunzo haya linafikiwa kwa kujituma kwa vitendo na kushirikiana na wenzenu pindi mtakapo rudi nyumbani. Kama mlivyoona ya kuwa hakuna jambo lisilowezekana, leo hii tunazungumzia mafanikio yanayotokana na kongano la Mwani – Zanzibar na Uhandisi Morogoro. Naamini kuwa katika mafunzo mengine yatakayo fanyika basi tutazungumzuia pia mafanikio ya Kongano zenu.
Ningependa kuwashukuru uongozi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia kwa kuwa katika mstari wa mbele katika kuhakikisha Sayansi na Teknolojia inawasaidia wananchi kwa kuendeleza ubunifu nchini. Ni naamini jitihada hizi zimeshaanza kuleta matunda na ni matumaini yangu mafanikio yatakuwa mazuri zaidi na kwa Kongano zote hapa nchini licha ya kuwa na changamoto mblimbali.
Nimefarijika sana kuambiwa kuwa washiriki wa mafunzo haya wanatoka nchi nzima yaani Tanzania Bara na visiwani na zinajumuisha kongano za Asali (Waziri mkuu mdau mkubwa), usindikaji wa mafuta ya alizeti, uhandisi ,Viungo Zanzibar na Kilimo cha samaki(fish farming), useremala,utalii, Uyoga, ufugaji wa kuku, uchongaji wa sanaa(Wood crafts), na useketaji (Handloom Cluster) na kilimo cha mboga mboga.
Ningependa kutoa pongezi kwa wawezeshaji wa mafunzo haya ambao wote ni Watanzania wanaowezesha pia katika nchi zingine kama vile vile Mozambique, Ghana, Nigeria, Senegal na Kenya. Hii inaonyesha kuwa sisi kama waTanzania tunauwezo wa kuiongoza Afrika katika mambo muhimu ambayo yanalenga kutatua tatizo kubwa la umaskini.Naamini kila mtu ameelewa na kuwatumia wataalamu wetu vizuri.
Kutokana na kuwa Watanzania ndio wawezeshaji wakuu wa Maswala ya Kongano Afrika basi tuna kila sababu ya kuwa mstari wa mbele kwa bara zima la Afrika katika kuonyesha umuhimu wa Kongano kwa kuonyesha ni jinsi gani zimesaidia katika kuongeza pato la taifa, ajira na maendeleo ya jamii na uchumi.
Najua mmetoka hapa na mpango kazi ambao mtawashirikisha wadau wote wa kongano katika kutekeleza mpango kazi huo.
Bila ya kupoteza muda, ningependa kuwatakia safari njema ya kurudi nyumbani na vilevile kazi njema ya kuendeleza kongano bunifu na kuonyesha matokeo ya mafunzo haya mliopata kwa siku nne.
Sasa napenda kutamka rasmi kuwa Mafunzo haya ya wawezeshaji wa Kongano Bunifu yamefungwa rasmi.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
Mgeni rasmi Mhandisi Stella Manyanya (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimpatia cheti cha ushiriki wa Mafunzo ya Wawezeshaji Kongano mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com, Stephano Mango, kushoto Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dk Dugushilu Mafunda, wa kwanza toka kulia ni Mwezeshaji Kongano Dk Flower Msuya, wa pili Mhandisi Peter Chisawilo kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo |
Washiriki wa Mafunzo ya Wawezeshaji Kongano wakifuatilia maelekezo mbalimbali kutoka kwa wakufunzi wa mafunzo hayo |
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
HOTUBA YA KUFUNGA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI KONGANO
Chini ya Pan African Competitiveness Forum – Tanzania Chapter
Tarehe 01.03.2012
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (Engineer Stella Manyanya)
Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Kongano Bunifu (Innovative Clusters)
Washiriki Wa mafunzo haya,
Wana habari, Mabibi na Mabwana
Kwanza kabisa kwaniaba ya mkurugenzi mkuu na Uongozi wote wa tume ya sayansi na teknolojia, napenda kutoa shukrani za dhati kwako kwa kuamua kuja kwako. Hii inaonyesha jinsi unavyotilia mkazo kwa vitendo maendeleo ya Kongano bunifu hapa nchini. Ni jambo la kufurahisha sana kuona kwamba umeweza kupata muda wa kujumuika nasi hapa leo na kukubali kufunga mafunzo yetu.
Mbele yako ni wanawarsha 46 waliokuwa katika mafunzo ya kuwa wawezeshaji wa Kongano. Wanawarsha hawa wanatoka sehemu mbalimbali hapa nchini ambako kuna kongano ambazo zinahitaji kuendelezwa. Naamini madhumini ya mafunzo haya kwako si kitu kipya kwani na wewe ulipata nafasi ya kushiriki katika mafunzo ya kwanza. Kongano zinazotegemewa kuendelezwa katika mafunzo haya ni 26.
Mafunzo haya yameandaliwa na tume ya sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na PACF –Tanzania. Mafunzo haya yalianza tarehe 27Feb2011 na yanamalizika leo 1March2012.
Tunashukuru sana ufadhili wa wenzetu wa Sweeden(SIDA) kwa kutuwezesha kufanikisha swala hili ambalo tunaamini litasaidia katika kuendeleza ubunifu na kuleta maendeleo kijamii na kiuchumi.
Kwakuwa wewe ni mdau mkubwa katika Kongano na vilevile ni mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kongano hapa nchini aamini kuwa unamengi ya kutuelekeza.
Bila ya kupoteza muda, napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kutoa vyeti vya wahitimu wa mafunzo haya, kutuambia machache na mwisho kufunga mafunzo haya.
Karibu Mheshimiwa.
No comments:
Post a Comment