About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, April 28, 2012

WAKULIMA WA KOROSHO WAGOMA KUPOKE MALIPO NUSU NUSU YA FEDHA ZAO

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Steven Augustino ,Tunduru

BAADHI ya wakulima wa korosho katika vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo wamegoma kupokea fedha za malipo yao huku wakidai kuto kuwa na imani na maelekezo yanayotolewa na viongozi wao.

Mgomo huo umefuatia kuwepo kwa maelekezo kuwa mkulima anayedai Shilingi 1200 kwa malipo ya korosho hizo atatakiwa kupokea mkononi Shilingi 850  na makulima anayedai Shilingi 350 atatakiwa kupokea Shilingi 200 huku kukiwa na maelekezo kuwa fedha nyingine watalipwa baada ya kuwasili kwa fedha zingine.

Wakiongea kwa nyakati tofauti miongoni mwa wakulima hao Mahamudu Ponera wa chama cha Msingi Nakayaya mashariki na Maghreth Mingwe walisema kuwa kitendo cha viongozu hao kuyumbisha malipo hayo kinalenga kuendelea kuichafulia sifa Serikali.

Walisema msimamo wao wa kukataa kupokea fedha hizo unatokana na wakulima kuelezwa kuwa baada ya kupokea fedha hizo watatakiwa kuacha Stakabadhi za malipo hayo na kubakia wakiwa hawana vielelezo vyovyote vinavyo onesha kuwepo kwa madai mengine katika vyama hivyo.

Alipo takiwa kuzungumzia hali hiyo Meneja wa Chama Kikuu cha wakulima wa wa Wilaya ya Tunduru  Iman Kalembo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kwamba msimamo wakutoa malipo hayo umetokana na fedha zilizofika kuwa ni kidogo hivyo wao hawakuona mkulima wa kumuacha wakati wa malipo hayo na kusisitiza kuwa fedha zikifika wakulima wote watakamilishiwa malipo yao.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo alidai kuwa hakubaliani na utekelezaji wa zoezi hilo na kuongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kulipa fedha zote na siyo kidogo kidogo na kwamba kama kuna kosa lilifanyika na viongozi hao ni uzembe wa viongozi wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru Msangi alisema kuwa malipo hayo yanatokana na Benki kutoa Tsh. 2,587,506,900 zimepangwa kughalimia malipo ya Kilo 1200 tu kati ya Kilo  7,367,689 zilizopokelewa katika maghala kati ya Kilo
7,570,000 zilizo zalishwa na akulima hao katika msimu wa mwaka 2011/2012.

 Msangi aliendelea kueleza kuwa mchanganuao wa malipo hayo unaonesha kuwa kiasi kingi ne cha Shilingi 119,759,340 zitalipwa awamu ya pili na kwamba hali hiyo inatokana na taratibu za malipo hayo kuchelewa kupelekwa Benki.

Alisema fedha hizo zinatokana na malipo ya kilo 560,101 ambapo kati yake kilo 53,347 zenye thamani ya Shilingi 64,016,400 ni korosho za daraja la kwanza na shilingi 55,742,940  zinatokana na kilo 506,754 za daraja la pili.

Mwisho

No comments:

Post a Comment