About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, April 26, 2012

WAKULIMA WALALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA MAZAO TOKA SHAMBANI                             
MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Augustino Chindiye, Tunduru


WAKATI wakulima wa mazao ya Chakula Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakilalamikia
kutozwa ushuru mkubwa kupitia vizuizi vilivyo wekwa na Wakala aliyeshinda zabuni ya kukusanya ushuru wa mazao ameahidi kuto msaidia mtumishi yeyote atakaye bainika kukiuka maelekezo yake.

Pamoja na kuitolewa kwa kauli hiyo Meneja wa kampuni ya StetyBussiness inayo kusanya ushuru huo katika halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Rashid Akbal aliwafananisha watumishi hao na mafisadi ambao wamekuwa wakiichafulia kasi ya Utendaji Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kampuni yangu inafanya kazi kulingana na maelekezo tuliyosaini katika Mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo” alisema Akbal na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima watakao fanyiwa vitendo viovu na watumishi hao kutoa taarifa zenye ushahidi kwake ili waweze kuwawajibisha.


Akbal ambaye alikuwa akijibu swali la kwanini kampuni yake inatoza ushuru hadi wakulima wa kawaida wanaobeba kuanzia debe mbili aliendelea kueleza kuwa maelekezo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa
kampuni hiyo ni kutoza wafanyabiashara wanaonunua mazao ya wakulima tu na si kuwatoza hadi wakulima wanao rudisha mazao yao kutoka shambani.

Akizungumzia hali hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo Mary Ding`ohi mbali na kukiri kupokea malalamiko mengi juu ya tozo hizo alisema kuwa ofisi yake ina andaa utaratibu wa kumwita mzabuni huyo na kumpatia maelekezo upya zikiwa ni juhudi za kuondoa kero hiyo.


Alisema katika maelekezo ya awali mzabuni huyo alielekezwa kukusanya kiwango kisicho zidi asilimiaa 5% kutoka kwa wafanyabishara hao wa mazao ya Chakula na kwamba mkataba huo pia uliwaondoa katika tozo hiyo wakulima wanaorudisha mazao yao kutoka shambani baada ya kuyavuna.


Akizungumzia kero hiyo katibu wa Umoja wa Chama Cha wauzaji na wanunuzi wa mazao ya wakulima (WAMANATU) Wilayani Tunduru Athuman Milanzi alisema kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwa kero hiyo inasababishwa na Mzabuni huyo kulazimisha kukusanya tozo hiyo kwa zaidi ya asilimia 5 iliyo kubaliwa katika mkataba wao.


Mwisho

No comments:

Post a Comment