About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, April 30, 2012

WANACHAMA WA SACCOS YA WALIMU TUNDURU WALIDHIA ONGEZEKO LA MAKATO

Na Steven Augustino, Tunduru
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa chama cha Ushirika cha akiba na  Mikopo cha Walimu wa Wilaya ya Tunduru kimeridhia kuongeza makato yao na kufikia Shilingi 30,000 kutoka Shilingi 15,000 walizo kuwa wakikatwa awali zikiwa ni juhudi za kutunisha mfuko  kwa kutumia uwezo wa ndani.
Sambamba na kuthibitishwa kwa maapendekezo hayo wajumbe hao walipitisha bajeti ya mapato na matumizi ya shilingi Milioni 66,819,220 na kutumia jumla ya Shilingi 45,857,840 katika mwaka wa
fedha wa 2012 kukiwa na ongezeko la asilimia 78 % ikilinganishwa na bajeti ya shilingi milioni 52,666,000.  zilizotumika mwaka uliopita wa mwaka 2011.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu meneja wa  chama hicho Mwl.Hassan Isaya alisema kuwa kati ya Fedha hizo  shilingi 36,675,000 zinatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani , misaada na Ruzuku kutoka kwa wahisani wamepanga kuingiza jumla ya shilingi 800,000, na Tshs 27,851,220 zitatokana na faida ya mkopo wa CRDB.
Katika taarifa hiyo pia Mwl. Isaya  alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 chama hicho kiliweza  kukopesha jumla ya shilingi Milioni 95,970,325  kwa wanachama wake
 
Mwl. Juma Ado akisoma taarifa zilizotokana na mrejesho wa mikutano mbalimbali alidai kuwa uzoefu unaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa upungufu wa wanchama katika chama hicho pia udogo wa makato ya Tsh 15,000 wanayo katwa wanachama wake ni kikwazo kingine kinacho kwamisha
maendeleo ndani ya chama chao.
Aidha Mwl ,Ado katika taarifa hiyo alitolea mfano hatua za maendeleo zilizopigwa na vyama vya kuweka na kukopa vya UTWANGO SACCOS iliyopo katika Mkoa mpya wa Njombe na NEWALA SACCOS  Mkoani
Mtwara  ambazo zimemudu kujenga vitega uchumi vya kujenga  Nyumba  za kulala wageni kupitia mfumo wa  mbinu za uhamasishaji na kupeana majukumu ili miradi hiyo iwe vyanzo mbadala
vya kutunisha .
Pamoja na kutolewa kwa mapendekezo hayo wito ukatolewa kwa Viongozi wa chama hicho kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa wanachama wapya pamoja na kumpelekea salamu mwajiri wao kuwa siku atakayo chelewesha makato yao kupeleka katika chama hicho wapo tayari kufanya maandamano
zikiwa ni juhudi za kuongeza mapato ya ndani ili kujiletea maendeleo.
 
Awali akifungua mkutano huo Mkuu wa 12 wa mwaka wa wanachama wa umoja huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Klasta, Afisa elimu ya Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Rashid Mandoa alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanachama hao kukopa kwa busara na kulipa kwa busara mikopo hiyo.
Wakitoa nasaha kwa nyakati tofauti katika mkutano huo Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo Jalia Msangi na Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Tunduru Mwl. Lazaro Saulo waliwahimiza wanachama hao kuwa waumini wa chama hicho kwa kukubali kwa hiari zao kuongeza makato kulingana na malengo ya kila mwanachama na kujiletea maendeleo kulingana na mahitaji yao.

Walisema kulingana na taratibu na sheria zinazosimamia ushirika pamoja na kuweka utaratibu wa kujiunga na chama husika pamoja na kuwekwa kwa mikakati yake pia kuwe na utaratibu wa kuwaruhusu wanachama kuchangia fedha kulingana na mahitahi tu.
Akifunga Mkutano huo Mwenyekiti wa umoja huo Mwl. Hassan Nakoma pamoja na kuwahimiza wanachama hao kuendelea kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na umoja huo pia aliwataarifu wanachama hao kuwa ujenzi wa Ofisi ya chama hicho umepangwa kupitia uwezo wao wa ndani baada ya mfadhiri wao Daimu Mpakate kushindwa kutimiza masherti ya umoja huo
Mwisho

No comments:

Post a Comment