About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, July 12, 2012

WAFANYAKAZI WA TANESCO LAWAMANI TUNDURU

Na Steven Augustino, Tunduru

WAFANYAKAZI wa Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wametuhumiwa kuwa wahujumu na wachakachuaji wa kubwa na wauzaji wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme ya shirika hilo.

Hayo yamesemwa na baadhi ya  wakazi wa Mji wa Tunduru kufuatia kuwepo na kujengeka kwa mazoea ya watumishi wa Shirika hilo kuuza mafuta hayo huku viongozi wao wakiwa wanawakingia vifua kwa visingizio kuwa mafuta yaliyo uzwa ni miongoni mwa mafuta yaliyotumika yaani machafu.
Baadhi ya wananchi hao ambao waliomba wasitajwe majina yao gazetini walidai kuwa wamelazimika kutoa kilio chao cha kuiomba serikali iwasaidie kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kuwaondolea adha hiyo.
Walisema kufuatia kukosekana kwa huduma hiyo kumesababisha kuwepo kwa ukubwa na gharama za maisha kutokana na bidhaa zote kupanda bei hasa vyakula ambako chanzo chake kimekuwa kikisababishwa na kuzimwa kwa Umeme mara kwa mara.

Aidha pamoja na mambo mengine zikiwemo kero tofauti zinazo sababishwa na uzimwaji wa huduma hiyo ukiwemo mdororo wa utoaji wa huduma katika huduma za Serikali Gazeti hili lilishuhudia kupanda kwa bei za unga na kufikia Shilingi 1500 kwa kilo moja kutoka Shikingi 600, mchele Tsh.2200 kutoka tsh.1500.

Alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo Kaimu Meneja wa Tanesco Wilayani humo Bosco Milumbe mbali na kukiri kuwepo kwa hali ya kutatanisha juu ya upatikanaji wa nishati hiyo alisema kuwa chanzo ni ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo.

Alisema hata hivyo wao hawana mamlaka ya kulishughulikia na kwamba wao hupokea mafuta baada ya kuandaliwa na Makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Dar Es Salaam ambao ndio hufanywa shughuli zote za manunuzi ya mafuta
Kuhusu tuhuma za watumishi kuchakachua mafuta alisema kuwa madai hayo siyo ya kweli akianisha kuwa Shirika hilo hupokea lita 30,000 za mafuta kila gari linapo fika na kwamba matumizi ya mitambo yake kwa siku ni wastani wa lita 3500 hadi lita 3600 ambapo hutakiwa kutumika wastani wa siku 10 tu.

Hata hivyo Milumbe alimaliza kwa kusema kuwa Shirika hilo limepanga kuwasha Umeme  kesho  kwa masaa mawili tu na kumaliza stoku ya mafuta lita 10.000 waliyokopa kutoka kwa mfanyabiashara binafsi kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wakazi wa mji huo kusaga na kukoboa nafaka zao na kwamba baada ya hapo huduma hiyo haitapatikana klwa muda usiofahamika.
Juhudi za kumtafuta Meneja wa Tanesco Kanda ya Nyanda za juu Kusini Eng. Boniface Njombe ili kuzungumzia hatima ya nishati hiyo kwa wakazi wa wilaya hiyo  hazikufanikiwa kutokana na simu zake  kutopatikana
MWISHO

No comments:

Post a Comment