VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA
Na Stephano Mango, Namtumbo
VIONGOZI wa wananchi na Watendaji wa umma wametakiwa kushirikiana na Asasi za Kiraia nchini ili kuweza kuongeza wigo wa uwajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora kwa maendeleo endelevu
Wito huo umetolewa jana na Mathew Ngalimanayo Mwendeshaji wa mdahalo wa wazi unaolenga kupata taswira ya uwajibikaji wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa vijiji na watendaji wa umma kwa wananchi wao ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kirai Wilayani Namtumbo(Naneciso) kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society uliofanyika kwenye ukumbi wa Faraja Villa
Ngalimanayo ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NACONGO) alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa Wabunge na Watendaji wa umma wanaitwa kwenye midahalo ya wazi yenye malengo ya kuwaleta pamoja wananchi kutoka makundi mbalimbali,
Asasi za Kiraia ili waweze kujadiliana kwa pamoja ili kupata taswira ya uwajibikaji wao hawafiki jambo ambalo linatia wasiwasi kiutendaji
Alisema kuwa Asasi za Kirai ni nguzo muhimu ya kusukuma maendeleo nchini na ni kiunganishi cha wananchi wanyonge ambao wanashindwa kuwafikia Viongozi wao kutokana na urasimu uliopo katika ofisi za umma
Alieleza zaidi kuwa midahalo ya Asazi ya Kiraia ni fursa nzuri kwa Serikali kuuambia umma juu ya kile kinachofanyika katika eneo husika, pia wananchi wanapata nafasi ya kusikia ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali na wadau wengine kwa kuzingatia misingi ya utawala bora
Awali akifungua mdahalo huo Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Namtumbo( Naneciso) Asumta Ndauka alisema kuwa mdahalo huo umeshirikisha watunga sera, wafanya maamuzi,wafugaji, wanafunzi, wakulima na makundi mengine maalum unalengo la kuimarisha mahusiano ya wananchi na viongozi wao ili waweze kuwajibika ipasavyo
Ndauka alisema kuwa mara baada ya mdahalo huo kumalizika tunatarajia kuimarika kwa wigo wa wananchi, viongozi wa umma na Asasi za Kirai katika eneo husika ili kuweza kufanikisha miradi na mipango mbalimbali inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi
MWISHO
Wednesday, October 10, 2012
Tuesday, October 2, 2012
WANANCHI WAILALAMIKIA SERIKALI KUCHELEWESHA MAENDELEO
Na Stephano Mango, Tunduru
WANANCHI wa Kijiji cha Kalanje Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameilalamikia Serikali kuwa imekuwa kikwazo cha kupeleka maendeleo kwa wananchi wake.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Barton Chuma wakati akichangia mada ya changamoto za maendeleo vijijini katika kikao cha Wazee kilicho fanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini hapa. Chuma alisema kuwa mbali na kuwepo kwa changamoto kubwa ya wananchi kukataa kujitolea yeye kwa kuwa shirikisha viongozi wa vyama vya Siasa wamefanikiwa kufyatua tofari laki nane zilizopangwa kutekeleza ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Kijiji chao.
Alieleza kuwa kinacho washangaza wananchi wa kijiji hicho ni kutopokea Shilingi Milioni 15 ambayo ni asilimia 60% waliyo ahidiwa na Serikali kupitia halmashauri yao ili kuwa wezesha kuanza kwa ujenzi huo. Alisema kufutia hali hiyo wananchi wameanza kupoteza imani kuwa huenda asilimia hiyo 40% ya nguvu zao hizo zikapotea bure na kuendelea kuvunja ari ya wananchi kupenda kujitolea pindi wanapo himizwa kufanya shughuli za maendeleo.
Chuma aliendelea kufafanua kuwa hofu hiyo inatokana na kuanza kwa dalili za kunyesha mvua huku mradi huo ukiwa haujulikani utaanza lini na kwamba endepo fedha hizo zitaendelea kuchelewa ipo hatari ya kuwakosa hata watu wa kusaidia ujenzi katika kipindi hicho ambacho kila mtu huhamia mashambani.
Wakizungumzia vitendo vya jamii kugomea maendeleo kwa madai kuwa kazi zote zinatakiwa kufanywa na Serikali Adam Ausi, Chikambo Mapunda na Eluminata Mdamu walisema kuwa tatizo hili linalelewa na Serikali yenyewe kutokana na kutoa Uhuru wa kuongea uliopitiliza.
Walisema pamoja na kuruhusu vyama vingi ambavyo hivi sasa vinatumiwa kama mwamvuli wa kuficha kundi hilo la wavivu na wapinga maendeleo kama Serikali ikitumia vizuri makali ya Mamlaka iliyopewa vitendo hivyo vilitakiwa kuondolewa kwa kukemewa na kuchukua hatua kwa walengwa bila kujali vyama wanavyo toka.
Akijibu kero hiyo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Wilaya hiyo Rashid Mandoa pamoja na kukiri kuwepo kwake alisema kuwa tayari taratibu za kukamilisha na kuingiza fedha hizo katika akaunti ya kijiji zinaendelea vizuri.
Alisema Kijiji hicho ambacho kilipangiwa jumla ya Shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, fedha hizo zilikwama kutokana na kuchelewa kufanyika kwa ukaguzi uliotakiwa kufanywa na kamati ya Fedha uongozi na mipango inayo undwa na madiwani wa halmashauri hiyo.
Mandoa aliendelea kufafanua kuwa baada ya kamati hiyo kutembelea eneo la ujenzi na mahali zilipo hifadhiwa tofari Septemba 26 mwaka huu na kujiridhisha tayari kamati hiyo imetoa ruhusa na baraka zote kwa ajili ya kuruhusu fedha hizo.
Nae Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho katika hotuba yake alisisitiza kuwa serikali haita kuwa na mchezo na haita mvumilia mtu yeyote atakaye pita na kuhamasisha wananchi kugoma kujitolea.
“Sita kuwa tayari kuwavumilia watu wanaopinga maendeleo huku majengo ya taasisi mbali mbali yakiwemo majengo ya Shule za Msingi na sekondari yakiwa Chakavu na mahitaji ya majengo mapya yakiwemo’’ alisema Dc, Nalicho.
Alisema katika kipindi chote cha Uongozi wake atahakikisha kuwa Wilaya yake inapiga hatua za kimaendeleo pamoja na kuhakikisha kuwa amani na utulivu vinalindwa kwa nguvu zote. Mwisho

Subscribe to:
Posts (Atom)