About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, October 10, 2012

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA

Na Stephano Mango, Namtumbo
VIONGOZI wa wananchi na Watendaji wa umma wametakiwa kushirikiana na Asasi za Kiraia nchini ili kuweza kuongeza wigo wa uwajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora kwa maendeleo endelevu

Wito huo umetolewa jana na Mathew Ngalimanayo Mwendeshaji wa mdahalo wa wazi unaolenga kupata taswira ya uwajibikaji wa wabunge, madiwani, wenyeviti wa vijiji na watendaji wa umma kwa wananchi wao ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kirai Wilayani Namtumbo(Naneciso) kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society uliofanyika kwenye ukumbi wa Faraja Villa

 Ngalimanayo ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NACONGO) alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa Wabunge na Watendaji wa umma wanaitwa kwenye midahalo ya wazi yenye malengo ya kuwaleta pamoja wananchi kutoka makundi mbalimbali,

 Asasi za Kiraia ili waweze kujadiliana kwa pamoja ili kupata taswira ya uwajibikaji wao hawafiki jambo ambalo linatia wasiwasi kiutendaji Alisema kuwa Asasi za Kirai ni nguzo muhimu ya kusukuma maendeleo nchini na ni kiunganishi cha wananchi wanyonge ambao wanashindwa kuwafikia Viongozi wao kutokana na urasimu uliopo katika ofisi za umma

Alieleza zaidi kuwa midahalo ya Asazi ya Kiraia ni fursa nzuri kwa Serikali kuuambia umma juu ya kile kinachofanyika katika eneo husika, pia wananchi wanapata nafasi ya kusikia ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali na wadau wengine kwa kuzingatia misingi ya utawala bora

Awali akifungua mdahalo huo Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Namtumbo( Naneciso) Asumta Ndauka alisema kuwa mdahalo huo umeshirikisha watunga sera, wafanya maamuzi,wafugaji, wanafunzi, wakulima na makundi mengine maalum unalengo la kuimarisha mahusiano ya wananchi na viongozi wao ili waweze kuwajibika ipasavyo

 Ndauka alisema kuwa mara baada ya mdahalo huo kumalizika tunatarajia kuimarika kwa wigo wa wananchi, viongozi wa umma na Asasi za Kirai katika eneo husika ili kuweza kufanikisha miradi na mipango mbalimbali inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi MWISHO

No comments:

Post a Comment