About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, April 13, 2012

MKUU WA MKOA MWAMBUNGU UMENENA, NAKUUNGA MKONO KWANI NAMI NIMEWAHI KUANDIKA MAKALA HAYA

  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya SongeaoCharles Mhagama

     HALI YA USAFI KATIKA MANISPAA YA SONGEA IMESHINDIKANA?

Na Stephano Mango,Songea

HALI ya usafi ambayo tulizoea kuiona katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea  ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa wa Ruvuma sasa imeanza kutoweka polepole hasa katika maeneo ya ghuba  za kuhifadhia takataka na mifereji ya maji katika baadhi ya barabara mjini hapa .

Uchunguzi wa kina uliofanywa  na Dira ya Mtanzania umebaini kuwa Manispaa ya Songea kuna ghuba nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wakazi na kwamba ghuba hizo zina dalili zote za kuzalisha magonjwa ya kuambukiza  hasa kipindi  hiki tunapoelekea masika .

Baadhi ya wakazi wa Manispaa hiyo  wameulalamikia uongozi  wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kujali afya za wananchi wake kwani pamoja na ghuba zao kujaa takataka na zingine kuanza kuzagaa na kusababisha watoto kuchezea hali inayoweza kupelekea hatari kwa ustawi wao.

Kwa sasa hali ya Manispaa hiyo ilivyo haimvutii mtu kuja kupumzika au kufanya shughuli zozote za burudani kutokana na uchafuzi wa mazingira uliokithiri kwenye viunga vya mjini hapa.

Hakuna bustani iliyotunzwa vizuri kwa kuvutia hata watalii kupumzika ukiachia wakazi wa mji wa Songea kutokana na mipango mibovu ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo inaonekana ndio chanzo cha uchafuzi wa mazingira

Kwani imeshindwa kutenga maeneo ya kuweka bustani za kupumzika wakazi wa Manispaa hiyo wakati wa mchana au wa jioni tofauti na miji mingine ambayo inathamini maeneo hayo muhimu kwa wananchi wake.

Hata bustani za miti,maua na mboga mboga zipo chache na hazionekani kiurahisi kutokana na mipango yake mibovu inayosabibisha hewa ya Manispaa kuwa nzito kutokana na uchafu wa mazingira unaoendelea kukithiri

Ni wazi kuwa swala la usafi wa mazingira katika Manispaa hiyo bado halijatiliwa mkazo kwani wananchi wanajitahidi kukusanya takataka pamoja lakini haziondolewi jambo hili linawakera na kuonekana wazi kuwa mamlaka husika haziwajibiki

Kwani ili wananchi wawe na afya njema na hatimaye waweze kumudu kazi zao vizuri kwa kutopata magonjwa ya mlipuko ni lazima usafi uzingatiwe katika maeneo wanamoishi.

Kila mwaka kumekuwa na taarifa za watu kupatwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kushamiri kwa uchafu unaotupwa hovyo huku ikifahamika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.

Licha ya kuzagaa kwa mifuko ya plastiki na makopo mitaani kutokana na kutupwa ovyo na watumiaji wake kutokana na kuzipuuza kanuni na sheria ndogo za Halmashauri au kutozijua kwa wananchi wengi

Ukipita katika mitaa ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni lazima utakutana na malundo ya takataka ambayo yameoza na kupelekea kutoa halufu mbaya kutokana na uzembe wa watendaji wa Manispaa hiyo.

Hali hiyo pia ipo katika Masoko ya Manispaa hiyo kama vile Soko la Manzese,Mfaranyaki,Bombambili,Majengo na Soko kuu la Songea kwani kutokana na watendaji wake kutosimamia sheria na kanuni za usafi katika maeneo hayo

Kumepelekea wafanyabiashara kutupa taka ovyo na kusababisha harufu mbaya kutokana na kuoza kwa taka hizo ambazo nyingi huwa zile za majimaji ya nyanya,maembe,machungwa,maji yaliyooshewa utumbo wa nyama na vyakula vilivyolala.

Ili suala la kuzagaa kwa uchafu katika maeneo ya Manispaa ya Songea libaki historia viongozi wa Serikali hiyo wanapaswa kuonyesha mfano wa kusafisha mazingira kwa vitendo.

Endapo Serikali hiyo inataka ifanikiwe katika operesheni ya kuboresha  usafi wa mazingira ni lazima waache kuzungumzia usafi maofisini na kwenye majukwaa na badala yake waonyeshe mfano kwa wananchi kwa wao kujumuika nao na kusafisha mazingira.

Viongozi waonyeshe mfano kwa wananchi kwa sababu mfumo wa namna hii unafanyika duniani kote ili kuboresha mazingira ,kwani kwa wale viongozi wanaowaelimisha wananchi jukwaani baadae huwafuata katika maeneo yao na kujumuika pamoja katika kusafisha mazingira yao.

Serikali inapaswa kubadilika kwa kuchukua suala la usafi wa mazingira kimatendo zaidi na si maneno mengi ambayo hayaleti mabadiliko yeyote katika suala zima la usafi

Ikiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto nyingi zilizopo ikiwemo za vifaa vya kuzolea taka,uelewa mdogo wa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi,ikiwa na kuziweka wazi kanuni na sheria ndogo za usafi wa mazingira.

Ili wananchi waweze kutambua wajibu wao kikamilifu na umuhimu wa utunzaji wa mazingira yao kwa afya na ustawi wao kwani bila kufanya hivyo ufanisi wa jambo hilo unaweza usifikie viwango stahiki.

Mwandishi  anapatikana
Simu 0755-335051
www.stephanomango.blogspot.com

No comments:

Post a Comment