Na Stephano Mango, Songea.
WAFANYABIASHARA wa
maduka mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
wamegomea kufungua maduka yao kwa kile kinachodaiwa kuwa serikali imeshindwa kuwasikiliza kilio chao
cha mashine za kielektroniki (EFD) ambazo zinatakiwa kwa muda mrefu
waliomba zishushwe bei .
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa mjini Songea umebaini kuwa
katika mitaa yote ya Manispaa ya
Songea maduka yote yamefungwa na kwamba katika eneo la soko kuu kwenye vibanda
vinavyolizunguka soko hilo navyo
vimefungwa isipokuwa wafanya biashara ndogondogo
wanaouza mchele, unga , nyanya na mbogamboga ndio wanaoendelea kufanya biashara
.
Badhi ya wafanya biashara waliohojiwa
kuhusiana na mgomo huo walisema kuwa
kwa muda mrefu waliiomba mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) Mkoa wa Ruvuma iangalie uwezekano wa kushusha bei ya
mashine za kielektroniki amabazo zimekuwa zikiuzwa kati ya shilling laki
sita na laki nane jambo ambalo walidai kuwa bei hiyo
wafanyabiashara wengi wanashindwa kuimudu .
Walisema kuwa hivi karibuni alifika mijini Songea Naibu Waziri
wa fedha Mwigulu Nchemba na kufanya
mkutano mkubwa kati yake na wafanya
biashara lakini alishindwa kutoa maelezo
yakinifu kuhusiana na bei ambayo imeonekana kuawa ni kandamizi kwa
wafanyabiashara hao.
Walifafanua kuwa wafanyabiashara hawagomei kuzinunua mashine
hizo isipokuwa wamedai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana kwa kuitaka
serikali iangalie namna ya kuzishusha bei ambayo wafanyabiashara wanaweza
kuimudu tofauti na hivi sasa.
Wameelezakuwa mawakala wa kuuza mashine hizo mkoani Ruvuma
wameteuliwa wachache na kuonekana kuwa kuna viwingu namna ya upatikanaji wa
mashine hizo hivyo wameiomba serikali itumie mfumo wa soko huria.
Kwa upande wake
meneja wa mamlaka ya mapato [TRA] mkoani Ruvuma Apili Mbaruku alithibitisha
kuwa maduka katika manispaa ya Songea kuwa yamefungwa lakini alieleza kuwa
ofisi yake inafanya utaratibu wa kuangalia tatizo jinsi lilivyo.
Naye katibu mtendaji
wa chama cha wafanyabiashara [TCCIA]mkoani Ruvuma ,Moyo akiongea kwa njia ya
simu alisema kuwa kuanjia majira ya saa za asubuhi wafanyabiashara kwa pamoja
waliamua kufunga maduka yao wakidai kuwa bei za mashine za kielektroniki ni
kubwa tofauti na biashara wanazo zifanya lakini kufuatia tukio hilo la mgomo
tayari mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ameitisha kikao kwa mazungumzo
zaidi.
Hata hivyo mkuu wa
mkoa wa Ruvuma Mwambungu akiongea kwa njia ya simu alithibitisha kuwepo kwa
mgomo huo na kwamba anatarajia kukutana na wafanyabiashara pamoja na maafisa
kutoka mamlaka ya mapato ili kuangalia tatizo hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment