Ni miaka minne sasa toka nilipoandika makala haya, leo kutokana na umuhimu wake naomba ndugu wasomaji wa Blog hii muweze kujikumbusha nilichokiandika na kama itawapendeza niko tayari kufanya uchambuzi mpya na wa kina kuhusu makala haya, endelea kutafakari kupitia maandisha haya
picha nitaziweka hivi punde
MWANJA
; MAFANIKIO YA MBIO ZA BENDERA YAMELETA HAMASA
MPYA CCM
Na: Stephano Mango, Songea
MIONGONI mwa kazi za chama cha siasa kilichopo
Madarakani ni kuwa daraja la kuwaunganisha watu na serikali waliyoichagua
katika kufanikisha ahadi zilizo ahidiwa wakati wa kampeni.
Mbali na jukumu
hilo, wajibu wa chama ni kusaidia watu kuielewa serikali yao inafanya
nini kwa wakati gani na kwa lengo lipi.
Ni wajibu wa chama kutumia mbinu mbalimbali za
kidemokrasia kuwahamasisha watu ili washirikiane na serikali yao ili
kuwaondolea matatizo sugu ya umaskini, maradhi na ujinga ambao umewaelemea.
Chama pia kina wajibu wa kuhakikisha kuwa
serikali inaendelea kuyajua maoni, shida na matakwa ya watu katika kufanikisha
vita dhidi ya maadui ujinga, umaskini na maradhi.
Hata hivyo, chama kinawajibu wa kuwakemea
wanachama wanaokwenda kinyume na matakwa ya kanuni na taratibu za chama.
Ingawa pia kina wajibu wa kuwaelimisha watu na
wanachama wote kwa ujumla ili waweze kuona shughuli zinazofanywa na serikali
yao katika kuwaletea maendeleo kusudiwa.
Hivyo basi, chama cha mapinduzi (CCM) kuelekea
uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu, na mwaka 2010 katika uchaguzi wa
Madiwani, Wabunge na Rais
Kimejiandaa kushinda kwa kishindo katika chaguzi
hizo kwa sababu katika uwanja mpana wa siasa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo
wa uchaguzi mwingine
Na lengo kubwa la Chama chochote cha siasa
katika Nchi yoyote duniani ni kushinda katika uchaguzi Mkuu na kuunda Serikali
yaani kukamata dola
Kwa mantiki hiyo, Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi
Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM
Mkoa wa Ruvuma iliamua kupeleka ujumbe kwa Wanachama na Wananchi kwa kutumia
mbio za Bendera ya Chama Cha Mapinduzi
Mbio hizo za Bendera zilizinduwa rasmi Mei 28
mwaka huu wa 2009 Wilayani Tunduru katika Kijiji cha Matemanga Mkoani Ruvuma na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Coleneus Msuha.
Akizungumzia malengo ya mbio hizo za Bendera
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Bw. Emmanuel Mteming’ombe anasema
kuwa mbio za Bendera ni ngeni na kwa mara ya kwanza zimekimbizwa Mkoa wa Ruvuma
na kuleta mafanikio.
Anasema malengo ya mbio hizo za Bendera ni
kukifanya Chama kionekane kwa watu na kwa Wanachama, kisha kisikike na watu
waonyeshe dalili ya kusikia uwepo wa Chama hicho.
Ni lazima Chama kitumie mbinu mpya katika
kujipenyeza kwa Wananchi katika Siasa za ushindani ili kuweza kuwahamasisha
waingie Chamani anasema Kiongozi wa Mbio za Bendera Nestory Mwanja
Mwanja anaendelea kufafanua kuwa tumeamua
kukimbiza Bendera ili kuwahamasisha Wanachama wawe hai kwa kulipia ada zao za
Uanachama na kuhudhuria vikao vya Chama kuanzia ngazi ya mashina, matawi,
Wilaya na Mkoa.
Mbio hizo za Bendera zimefanya kazi kubwa ya
kuwaeleza Wanachama wote ujumbe kutoka Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC kuhusu
mabadiliko ya upigaji kura za maoni kuhusu kumpigia kura Diwani, Mbunge na Rais
anasema Kiongozi huyo.
Anasema pia mbio hizo zimetumika kupeleka ujumbe
kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura
katika
Misingi ya Demokrasia.Kueleza Sera imara za CCM kwa Wananchi ili waweza
kuzitafakari na kushawishika kuingia Chamani
Kwani kila Chama kinapaswa kujipambanua kwa
Wananchi ili waweze kuchukua maamuzi sahihi ya Chama gani Wajiunge nacho
anasema Kiongozi huyo wa CCM Mwanja
Kinachoonekana sasa, baadhi ya Watu wanakimbilia
kujiunga katika Chama chochote cha Siasa, wanakimbilia katika hivyo sio kwa
sababu ya kuvutiwa na itikadi zake zinazo ambatana na imani, bali wanakwenda
kwa sababu wamevutiwa na sera papo kwa papo ambazo huwa zinamwagwa jukwaani
bila kuwepo kwa mikakati stahiki ya kuzitekeleza sera hizo anasema Mwanja
Mbio za Bendera zimetumika pia kuwahamasisha
Wanachama kuanzisha miradi mipya na kuiendeleza miradi ya zamani ya Chama ili
kijikwamue Kiuchumi. Kwa sababu Siasa ni Uchumi bila Uchumi imara hatuwezi
kufanya Siasa katika Chama hivyo Chama imara ni chenye Uchumi imara anasema
Mwanja
Anaendelea kufafanua kuwa, mbio hizo za Bendera
zimetumika kuelezea bayana mafanikio ambayo Serikali ya CCM imeyapata kwa
kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Kwani kuyaanika hadharani mafanikio hayo
kutawafanya Wananchi waelewe jinsi ilani ya Chama Cha Mapinduzi ilivyotekelezwa
chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ambaye ndiye Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwani tunatambua kufanya hivyo kutaziba mianya
kwa Viongozi wa vyama vya upinzani ambao kila kukicha wanajifanya vipofu na
viziwi kwa kudai eti hakuna jambo lolote la maendeleo ya Watanzania
linalofanywa na Serikali ya CCM huku wakijua wanayoyasema sio ya kweli anasema
Mwanja
Anaendlea
kufafanua kuwa, CCM bado ni Chama makini kilicho na malengo makubwa ya kuwainua
Wananchi wake hivyo wanapaswa kuwa na subira na kuridhika kwa yale mazuri
yanayofanywa na Serikali pamoja na Chama tawala.
Kwani mambo mengi tumetekeleza kama ilani
inavyoelekeza na katika maeneo mengine hasa katika Nyanja za miundo mbinu ya
barabara, maji, afya na elimu, kuna mipango mbalimbali ya utekelezaji
inaendelea anasema kiongozi huyo.
Mwanja anasema kuwa mbio hizo zimetumika pia
kumpongeza Rais Kikwete kwa kazi nzuri alayoifanya ya kutekeleza vyema ilani ya
Chama Cha Mapinduzi. Kwani ni dhahiri juhudi zake za kuanzisha saccos na kutoa
mitaji kwa wajasiriamali, kukuza Demokrasia katika misingi ya amani.utulivu na
mshikamano.
Hata kuendeleza miradi ya Afya, barabara, maji,
elimu na maboresho mbalimbali ya mishahara katika Sekta za Umma na mengineyo ni
miongoni mwa utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi anasema Mwanja
Anaendelea kufafanua Mwanja , mbio hizo za Bendera zimepita kwenye
mashina na Matawi yote ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Ruvuma na kufanikiwa
kuingiza jumla ya wanachama wapya 3951.
Na imezindua jumla ya miradi 35 ya Chama kwa
Mkoa mzima, yaani imeweka mawe ya Msingi katika Ofisi za Matawi na pia
zimefanikiwa kufungua Ofisi tano za Matawi.
Miradi hiyo imeghalimu jumla ya shilingi Milioni
380 ikiwa ni jitihada za Wanachama kutoka kwenye mashina na Matawi kwa
ushirikiano Mkubwa na Uongozi wa CCM Mkoa.
Hata hivyo anasema mbio hizo zimepita kuangalia
pia miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya nne.
Pia zimepita kuangalia miradi ya Wananchi na
Wanachama wa CCM ya ufugaji wa Kuku, mbuzi,ng’ombe pamoja na ujenzi wa nyumba
bora za watu binafsi ambapo miradi hiyo yote inagharimu Milioni 750.
Katibu wa
CCM Mkoa Ruvuma Emmanuel Mteming’ombe, amewashukuru wakimbiza Bendera kutoka
katika Jumuiya ya umoja wa Vijana wa CCM Mkoa UVCCM.
Ambao amewataja majina ya Mwanahamisi Ngaje
kutoka Wilaya ya Namtumbo, Doris Ngareka kutoka Mbinga, Hamis Nkali kutoka
Tunduru, Mkandu Ngonji kutoka Songea Vijijni, Nestory Mwanja ambaye ndio
Kiongozi Mkuu, Hilda Mgao na Mwajuma Rashid kutoka Songea Mjini,
Mteming’ombe anamalizia kwa kusema mbio hizo
zenye mafanikio makubwa zilifikia kilele chake Juni 19 katika Kata ya Mletele iliyopo Manispaa ya
Songea ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Coleneus Msuha.
Hata hivyo, Nestory Mwanja ambaye ndiye kiongozi
wa mbio hizo za bendera amewataka Vijana wajiunge katika Chama kwani mhimili wa
Taifa lolote ni Vijana.
Mwandishi wa Makala hii
Anaptikana kwa simu no. 0755 335051
Barua pepe:
Stephano12mango@yahoo.com
No comments:
Post a Comment