About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, January 24, 2015

NEWFORCE YAGONGA SONGEA , MAJERUHI ATELEKEZWA PERAMIHO

NEWFORCE YAGONGA SONGEA , MAJERUHI ATELEKEZWA PERAMIHO
NA ,GIDEON MWAKANOSYA, SONGEA.

MKAZI wa Matogoro  Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ,Hamis Kinana (20)amelazwa katika Hospital ya  Rufaa ya Misheni Peramiho baada ya kugongwa na  gari la Abiria la Kampuni ya Newforce linalofanya safari zake Songea na Dar-Es salaam na kumsababishia kulazwa katika chumba cha Wagonjwa  Mahutitu [ICU] .

Akiongea na Nipashejana Swalehe Kinana ambaye ni Kaka wa Majeruhi huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 17 mwaka huu majira ya 2:15 jioni katika maeneo ya stendi kuu msamala wakati mdogo wake alipokuwa akirudi Nyumbani akiwa anatokea shambani kwao Mlete.

Kinana ambaye ndiye anayemtunza mdogo wake Hamis Kinana hospitalini hapo  alisema kuwa baada ya gari hilo kufanya tukio hilo liliendelea na safari bila dereva kuchukua hatua zozote dhidi ya mwathirika huyo.
Alisema kuwa wao kama familia walipata taarifa kuwa ndugu yao amegongwa na gari la abiria linalofanya safari zake kutoka ,Songea kwenda Dar es salaam kisha kubebwa na Wasamalia wema hadi Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma na ndugu walipoona hali yake ni mbaya wakaamua kumpeleka katika Hospital ya Rufaa ya Misheni Peramiho ambako amelazwa Chumba Maalum cha Uangalizi kwa Wagonjwa Mahututi [ICU]

“Tangu ndugu yetu Tumlete hapa Hospitalini hatujamuona hata Mfanyakazi yeyote wa Kampuni hiyo ambayo imefanya tukio hilo kufika kumjulia hali jambo ambalo limetusikitisha sana sisi wanafamilia”alisema ,Swalehe
Kwa upande wake Mganga  Muuguzi wa zamu katika Wodi hiyo ,Adili Msanga  alikili kumpokea ,Hamis Kinana akiwa ana Majeraha ya kichwani na Mdomoni ambayo alidai yameonyesha yametokana na ajali na kuwa kulingana na hali yake waliamua kumuweka chumba cha uangalizi Maalumu  [ICU]

Naye kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela Akizungumzia Tukio hilo jana alikili kutokea kwa tukio hilo lililotokea Katika Barabara ya Songea-Njombe na kuhusisha Gari ya Kampuni ya  NewForce yenye namba za Usajiri T.485 CTF ikiwa inaendeshwa na Godwin Boniface Mkazi wa Jijini Dar Es Salaam aina ya Zongtong na Pikipiki yenye Namba za Usajiri MC.287 ADF aina ya Sanlg iliyokuwa inaendeshwa na Hamis Kinana

Msikhela  Alisema kuwa hali ya Majeruhi ni mbaya na amelazwa Katika Hospital ya Rufaa ya Misheni Peramiho  akiendelea kupatiwa Matibabu na Kwamba Dereva wa NewForce  Amekamatwa, amehojiwa na Jarada lake Limepelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  wa Serikali Kanda ya Songea kwa Hatua Zaidi
       MWISHO.


No comments:

Post a Comment