NA STEPHANO MANGO, SONGEA.
WAFANYABIASHARA wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika
kufunga maduka yao kupinga kitendo cha kukamatwa Mwenyekiti wao wa Jumuia ya Wafanyabiashara
nchini David Minja na kwamba mgomo huo utadumu mpaka hapo watakapopata uhakika
wa usalama wake na si vinginevyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jana Ofisini Kwake
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Tawi la Ruvuma Isaya Mbilinyi
Mwilamba Alisema Kuwa Tumefunga Maduka tukiwa Tunamtafuta Mwenyekiti wetu Minja
kwani hatuna sababu ya kuendelea na biashara zetu wakati Kiongozi kakamatwa na
Jeshi la Polisi Nchini
Mwilamba Alisema kuwa Tunasitisha Shughuli mpaka Tujue Hatma
ya Kiongozi wetu ambaye Kimsingi ndiye Mtetezi wa Unyonyaji wa Serikali Kupitia
Mgongo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hata hivyo Hatufungui Maduka Mpaka Serikali
ituambie kwa kina kwanini wamemkamata kiongozi
huyo na endapo wakimuachia sisi tupo Tayari kufungua Maduka
Alifafanua kuwa Kiongozi wetu alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya
Majadiliano ambayo imeundwa kwa Pamoja Kati ya Wafanyabiashara na TRA yenye
lengo la Kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na malalamiko ya
wafanyabiashara kuhusu matumizi ya Mashine za Kietroniki za kulipia Kodi EFD
“Tunaitaka Serikali Izingatia Nia Njema ya kuundwa kwa
kamati hiyo ya Majadiliano na itoe taarifa stahiki kwa wafanyabiashara kwani
tunapata wasiwasi kuwa kukamatwa kwake kiongozi wetu kunatokana na juhudi za
wafanyabiashara kupinga ongezeko la kodi kwa Asilimia mia moja na matumizi ya
mashine za EFD” Alisema Mwilamba
Alisema Serikali inapaswa kutumia njia za kidemokrasia
kumaliza changamoto zake na sio kutumia nguvu kuzima madai ya msingi ya
wafanyabiashara hivyo ni vyema ikasikiliza kilio cha wafanyabiashara ambao
kimsingi ndio wachangiaji wakubwa wa kodi za Serikali
Katibu wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Ruvuma Kipara
Nziku alisema kuwa serikali imekurupuka
kumkamata mwenyekiti wao kwani tayari walishakuwa kwenye mazungumzo na TRA juu
ya mashine za EFD na swala la wafanyabiashara kukataa kulipa kodi hivyo
ingekuwa vyema kusubili muafka wa majadiliano hayo.
Alisema kuwa madai ya
serikali juu ya mwenyekiti huyo ya kwamba anachochea wafanyabiashara wasinunue
mashine za EFD pamoja na wafanyabiashara nchini wakatae kulipa kodi kimsingi
hayana mantiki yeyote hivyo ni lazima busara itumike.
Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara mkoani humo kuendelea
kuwa wavumilivu na watulivu kwa kipindi hiki ambacho wamesitisha hutuma hadi
hapo hatima ya mwenyekiti wao Minja itakapopatikana.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Apili Mbaruku
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema kuwa mgomo wa
wafanyabiashara ahuhusiki kabisa na TRA bali jambo hilo linahusika na jeshi la
polisi ambalo ndilo linajuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Minja amekamatwa kwa
sababu gani.
Hata hivyo Meneja huyo alipohojiwa na waandishi wa habari
juu ya athari gani ambazo wanazipata juu ya mgomo huo alisema kuwa kwa sasa ni
mapema mno kujuwa hasara kwani TRA wamekuwa wakikadilia mapato ya
wafanyabiashara kwa mwaka na sio kwasiku hivyo ni vigumu kuelezea.
Nae kaimu Afisa biashara Mkoa wa Ruvuma Furaha Mwangakala
alisema kuwa swala kwa sasa wapo mbioni kumfikishia mku wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu ili aweze kutoa kauli ya mwisho ya serikali ya Mkoa.
Katibu mtendaji wa Chemba ya wafanyabiashara ,Kilimo na
Viwanda (TCCIA)mkoa wa Ruvuma Philimon Moyo alisema kuwa kwa sasa hana cha
kusema kwa sababu jumuia hiyo ya wafanyabiashara mkoani humo imeonesha
kutowatambua TCCIA.
Jitihada za kumpata Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
ziligonga mwamba baada ya Katibu wake Revokatus Kasimba kuwaambia waandishi
kuwa mkuu wa Mkoa yupo kwenye kikao hivyo hataweza kuongea na waandishi wa
habari hadi hapo atakapomaliza kikao.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment