ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKIWAWEKA CHINI YA ULINZI WAHALIFU
NA,STEPHANO MANGO,SONGEA
SERIKALI kupitia Vyombo Mbalimbali Vya Ulinzi na Usalama Mkoani
Ruvuma Imepongezwa kwa Hatua Iliyozichukua za kuwabaini na Kuhakikisha Mtandao wa Wahalifu wa Mabomu ya
Kutegwa ya Kienyeji unasambaratishwa kwa kukamatwa na Vyombo vya dola
Pongezi hizo zimetolewa na Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya
Songea ambao wamesema kuwa Kitendo cha Kuunasa Mtandao huo kimewafanya wakazi
wa Manispaa hiyo Kuondokana na Hofu Iliyokuwa imetanda kufuatia kutokea Matukio
Matatu tofauti ya milipuko ya Mabomu
Kwa Upande wake Michael Westi Mkazi wa Bombambili
amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na Vyombo Vingine Vya Ulinzi na Usalama kwa
Juhudi zilizofanywa za Kuunasa Mtandao huo ambao ulikuwa unahatarisha Amani na Usalama kwa Wananchi
Westi Alisema kuwa Kukamatwa kwa Mtandao huo Wananchi hao
kwa sasa hivi wamekuwa na Utulivu na amani imerejea tena kwa Wakazi wa Manispaa
hiyo hivyo Vyombo vya Dola vinapaswa kuendelea kufanya kazi zaidi ya kuwabaini
wahalifu katika maeneo yote Mkoani Ruvuma hasa Ukizingatia kuwa Mkoa wa Ruvuma
upo Mpakani mwa Msumbiji na Malawi
Selestini Komba Mkazi wa Mfaranyaki ameiomba Serikali Mkoani
Ruvuma Kuona Umuhimu wa Kufanya Misako ya Mara kwa Mara katika Maeneo
Mbalimbali yenye lengo la kuwabaini Waharifu ambao walishaanza kuleta hofu
kwenye maeneo mengi
Jonas John Mkazi wa Majengo Manispaa ya Songea alisema kuwa
ni vyema Wananchi Katika Maeneo
MBlimbali Mkoani humo wawe wanaonyesha Ushirikiano na Vyombo vya Dola Na Kama
Kuna Mtu wanakuwa na Mashaka naye sio vibaya kutoa Taarifa kwenye vyombo husika
ili akamatwe na ahojiwe
Alifafanua zaidi kuwa Wamiliki wa Nyumba wajitahidi kuweka
utaratibu wa kuwatambua wapangaji wao na shughuli wanazo fanya na sio
vinginevyo na Serikali ione umuhimu wa kuwa na daftari la Wakazi wa eneo husika
ili kuwabaini wakazi ambao sio Raia wema
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa
Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mwambungu aliiambia Tanzania
Daima kuwa Matukio hayo matatu ya Mabomu yaliyotokea Songea yalimfanya atumie
muda kufikiria njia gani sahihi ya kuwadhibiti wahalifu hao
Mwambungu alieleza zaidi kuwa pamoja na jitihada kubwa ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini
walifanikiwa kugundua kuwa Matukio yote Matatu ya Mabomu yaliyotokea Mjini
Songea yalikuwa ni ya Kigaidi na Kwamba kwa sasa hivi Mtandao wote
umeshabainika hivyo amewataka wananchi waondoe hofu ambayo ilikuwa imetenda
miongoni mwao
MWISHO
No comments:
Post a Comment