Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Songea Anna Mbogo
Na Gideon Mwakanosya,Songea.
WATU watatu wamejitokeza kuchukuwa fomu akiwemo katibu wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Menansi Komba za kuwania nafasi ya kiti cha udiwani kata ya Matimila Wilaya ya Songea vijijini Mkoa wa Ruvuma baada ya kuachwa wazi na aliyekuwa diwani wa kata hiyo Joseph Komba (CCM) kufariki dunia kwa ajari ya pikipiki.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana ofisini kwake Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Peramiho Anna Mbogo amewataja waliochukuwa fomu kuwa ni Eliutelius Pili wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juma Gawaza wa chama cha wananchi CUF na Menansi Komba wa chama cha Mapinduzi(CCM).
Mbogo amesema kuwa hata hivyo mwisho wa kurudisha fomu hizo ni septemba 9 mwaka huu majira ya saa 10 jioni na kwamba kampeni zitaanza rasmi septemba 10 hadi Oktoba 1 mwaka huu majira ya sa 12 jioni.
Hata hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya udiwani siku ya oktoba 2 mwaka huu kwani kumekuwepo na mazoea ya kutojitokeza kwenye zoezi la upigaji kura hali inayopelekea udororaji wa demokrasia nchini.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Songea Mbogo amesema kuwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya kiti cha udiwani katika kata ya Matimila unatarajiwa kufanyika oktoba 2 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Joseph Komba aliyefariki kwa ajari ya pikipiki wakati anaendesha kijijini hapo Machi 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment