About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, October 19, 2011

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATEMBELEA WILAYA YA MBINGA NA YA NYASA

Na Mwandishi Wetu,Songea
MKUU wa Ruvuma Said Mwambungu amefanya ziara ya siku mbili Octoba 17 na Octoba 18 mwaka huu katika Wilaya ya Mbinga na Wilaya mpya ya Nyasa na kutembelea miradi mbalimbali na kujitambulisha kwa wananchi wa maeneo hayo
Ziara hiyo ya Mwambungu siku ya kwanza alianza kwa kukagua mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia pacha ya Peramiho hadi Mbinga,kukagua ujenzi wa Zahanati ya Gereza la Kitai ambapo pia alizungumza na wananchi,kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Mwambungu alitembelea Kijiji cha Mtupale kata ya Chiwanda na kuzungumza na wananchi ambako ilielezwa kuwa katika kijiji hicho ukiachia Wabunge na wakuu wa Wilaya waliowahi kuongoza Wilaya hiyo, kiongozi wa kwanza wa kitaifa kufika hapo ni Mkuu wa Majeshi na Ulinzi Jenerali David Mwamunyange ambapo alitembelea kijiji hicho mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu
Siku ya pili Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alikagua bandari ndogo ya Mbamba bay,kukagua ujenzi wa bandari ndogo ya Ndumbi ambapo pia alizungumza na wananchi,kukagua kivuko cha mto Ruhuhu(Feri ya Lituhi)na kutembelea na kukagua eneo la machimbo ya makaa ya mawe Ruanda

No comments:

Post a Comment