Na Thomas Komba,Songea
HALI ya usafi ambayo tulizoea kuiona katika Manispaa ya Songea sasa imeanza kutoweka polepole hasa katika maeneo ya ghuba za kuhifadhia takataka na mifereji ya maji katika baadhi ya barabara mjini hapa .
Uchunguzi wa kina ulifanywa na mwandishi wa mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com Thomas Komba amebaini kuwa kuna ghuba nne maeneo ya Mfaranyaki zimekuwa kero kwa wakazi ,pia ghuba hizo zina dalili zote za kuzalisha magonjwa ya kuambukiza hasa kipindi hiki tunapoelekea masika .
Baadhi ya wakazi wa eneo la makaburi ya wahindi mtaa wa Bikuli wameulalamikia uongozi wa serikali ya mtaa kupitia Mwenyekiti wao Laurent Mbewe kuwa ghuba yao imezagaa takataka ambazo sasa zimekuwa ni karata kwa watoto wa maeneo hayo .
Mkazi mmoja wa jirani kabisa na ghuba hilo Semeni Msafiri alisikika akisema “Sasa hii ni hatari mbona kipindupindu kitatuua kwani sasa ni wiki mbili (2) hazijazolewa takataka mpaka zinanuka ,Mvua zikija hapatakalika “alimalizia Semeni
Wakazi wa eneo la Mkomi darajani nao wamelalamikia ghuba lao kwa kusema “Songea imeongoza kwa usafi mara tatu ,sasa kimetokea nini ,labda malumbano ya madiwani yanapelekea hali hiyo”,eneo hilo ghuba lake limejaa na halijazolewa muda mrefu .
Jambo la kusikitisha ni pale kituo cha Lizaboni pana kila aina biashara ya vyakula zikiwemo samaki na dagaa ,nyanya ,ndizi , na aina nyingine za matunda ,napo uchafu umejaa kwenye ghuba hilo kama kawaida ya ghuba zilizo tanguliwa kutajwa .
Mkazi mmoja wa eneo la soko la Mfaranyaki alisikika akisema kuwa “Heri tupewe kazi hiyo sisi na manispaa itulipe kuliko hali hii.
Hali hii iko karibu maeneo yote ya katikati ya mji wa Songea ,ikiwemo Bombambili ,Matarawe,Misufini ,Mahenge ,Ruvuma na mtaa wa polisi kata ya mjini .
Katika kuelezea tatizo hilo wataalamu wa Afya wamesema wanakumbana na changamoto ya makisio pamoja uhaba na magari ya kuzolea takataka.
Aidha mvua iliyonyesha hivi karibuni mjini hapa ,tayari imeonyesha hali ya mji itakavyo kuwa mbaya barabara zake zisipo wekewa mifereji ya maji mapema ,kwani kuna maeneo maji yataingia kwenye makazi ya watu,mfano mzuri ni Majengo ,Mfaranyaki ,Makaburi ya wahindi ,Misufini ,Bombambili eneo la sokoni na eneo la Washingitone kuvukia sekondari ya Muslimu,
Uchunguzi wa Jambo leo unaendelea ili kubaini uongozi wa manispaa Songea unakalibiana vipi na changamoto hizo .
Mwisho
No comments:
Post a Comment