Na Gideon Mwakanosya ,Songea.
WATU 19 wamenusurika kufa baada ya basi dogo maarufu kwa jina la daladala walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka katika mteremko uliopo katika barabara ya Bombambili katika Manispaa ya Songea na kusababisha watu watatu kati yao kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Naftan Mantamba alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11 jioni huko katika eneo la mteremko wa Bombambili .
Alisema kuwa gari hilo lenye namba za usajiri T301 AQD aina ya Nissan Haice ambayo ilikuwa inaendeshwa na Frenk Honde iliacha njia na kupinduka na baada ya tukio hilo dereva alikimbia.
Mantamba alisema kuwa baada ya gari hilo kupinduka abiria 19 wamejeruhiwa lakini kati yao abiria 3 wamejeruhiwa vibaya sana na hali zao ni mbaya kwa sasa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa kwa matibabu na wengine walitibiwa na kuruhusiwa kurudi majumbani mwao.
Amewataja majeruhi ambao hali zao ni mbaya kuwa ni Sakila Ramji(22) Abdul Mohamed (34) na Emma Komba(30) wote wakazi wa Songea mjini.
Chanzo cha ajari inadaiwa kuwa gari iliaribika likiwa kwenye mwendo mkali na kusababisha dereva kushindwa kumudu usukani kisha likaacha njia na kupinduka.
Kwa upoande wake Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea Dkt. Benedkto Ngaiza amethibitisha kupokea majeruhi wa ajari hiyo ambapo alieleza kuwa walioletwa walikuwa 19 lakini ambao hali zao ni mbaya wapo watatu na wamelazwa kwenye wodi ya majeruhi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment