Na Gideon Mwakanosya,Songea
WATU 26 wamenusurika kufa baada ya basi dogo waliokuwa wakisafilia kutoka Songea Mjini kwenda Chipole kuligonga loli lililokuwa limeegeshwa kandokando ya barabara kwenye kona karibu na Daraja la mto Mlale ambalo lilikuwa bovu linasubiri kutengenezwa.
Kaimu kamanda Polisi Mkoa wa Ruvuma Naftari Mantamba amesema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 31 mwaka huu majira ya saa 10:45 jioni huko kwenye eneo la daraja mto mlale uliopo katika kijiji cha Msanga Wilaya ya Songea vijijini
Mantamba amefafanua zaidi kuwa basi hilo dogo linalofahamika kwa jina la Tumaini ambalo linamilikiwa na kanisa Katoliki Jimbo kuu la Songea , Parokia ya Chipole lilikuwa linatoka Songea Mjini kwenda Chipole huku likiwa limebeba abilia 26 akiwemo Dereva wa gari hilo pamoja na tingo wake.
Ameeleza kuwa basi hilo dogo ambalo lilikuwa linaendeshwa na Christofa Mapunda (42), iliigonga lori lenye namba za usajili T 770 AYL aina ya skania ambalo lilikuwa limeegeshwa kandokando ya barabara bila kuweka alama ya aina yeyote ya kuashilia kuwa mbele kuna gari bovu.
Amebainisha zaidi kuwa basi hilo dogo lenye namba za usajili T 182 ANV aina ya Isuzu baada ya kuligonga loli imesababisha watu wa 5 wakiwemo dereva na tingo wake kujeruhiwa vibaya na kwamba kwasasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Peramiho kwa matibabu zaidi na abilia wengine wamepata majeraha madogo madogo na kwamba wamepata huduma ya kwanza katika zahanati ya Misheni katoliki parokia Chipole na kuruhusiwa kurudi majumbani kwao.
Amewataja majeruhi walio pelekwa Peramiho ambao hali za mbaya kuwa ni dereva wa gali hilo Christofa mapunda (42) mkazi wa Songea Mjini, utingo wa basi hilo Englibeti Mbepera (26) mkazi wa Mbinga Mjini Sista Hapiñes Kihwili na Sista Leliana Muhanje miaka (25) wote wanatoka Shirika la chipole pamoja na mwalimu Velinaundi Kawonga (48) wa Shule ya Msingi chipole
Amesema kuwa gali hilo ambalo lilikuwa na abilia 26 ambapo kati yao walio jeruhiwa vibaya ni wale waliokuwa wamekaa kwenye viti vya mbele na chanzo cha ajali hiyo ni kuwa lori likuwa limegeshwa kandokando ya barabara karibu na daraja bila kuweka alama ya aina yeyote ambayo ingemwonyesha dereva wa basi dogo kuwa mbele kuna gari bovu limeengeshwa kandokando ya babara na kusababisha kuligonga.
No comments:
Post a Comment