Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Mwandishi Wetu, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Jaibu Alli ambaye umri wake haukuweza kufahamika mara moja kwa tuhuma za kumbaka msichana wa umri wa miaka kumi na sita ambaye jina lake limehifadhiwa anayesoma katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Kalembo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi jioni majira saa kumi jioni huko katika eneo la Matogoro Songea Mjini nyumbani kwa Wazazi wake.
Kamuhanda amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio msichana huyo akiwa jirani na nyumbani kwake alikutana na Jaibu ambaye alikuwa ni Mwanafunzi mwenzake katika Shule ya Kalembo na amehitimu Elimu ya Sekondari mwezi mmoja uliopita na walisalimiana na baadaye mvulana huyo alianza kumwambia maneno ambayo msichana huyo hakukubaliana nayo .
Ameeleza zaidi kuwa baada ya Jaibu kuona kuwa msichana huyo hakubaliani na maelezo aliyoyatoa ya kumtaka afanye mapenzi naye ndipo inadaiwa kuwa aliamua kumbaka kwa kutumia nguvu na kumsabishia sehemu za siri kuharibika na baadaye alikimbizwa katika hospitali ya Serikali ya Mkoa kwa matibabu ambako amelazwa akiendelea kupata matibabu.
Amesema mara tu baada ya kutokea tukio hilo mzazi wa msichana alitoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi cah Songea na askari walipokwenda kwenye eneo la tukio walifanya upelelezi wa awali kisha walifanikisha kumkamata Jaibu.
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi bado inaendelea kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo na kwamba ukikamilika mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.
WAKATI HUOHUO Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Simon Mkazi wa Soko la wakulima Mbinga Mjini kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kiwanjani Mbinga Mjini ambaye jina lake limehifadhiwa.
Kamuhanda amesema tukio hilo lilitokea novemba 20 mwaka huu majira ya saa nane mchana huko katika eneo la mtaa wa soko la wakulima lililopo Mbinga Mjini ambako inadaiwa kuwa msichana wa umri wa miaka 12 akiwa nyumbani kwa wazazi wake alivamiwa na kubakwa na mtu mmoja ajulikanae kwa jina moja la Simon.
Amesema kuwa mtuhumiwa alitoroka mara tuu baada ya kumfanyia kitendo cha kinyama msichana huyo na kwamba kwasasa hivi Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma linamtafuta mtuhumiwa huyo ambaye anadaiwa kuwa amekimbia na kutokomea kusikojulikana.
MWISHO
Inauma, inasikitisha sana kuona/kusoma habari hii ya kinyama. Vyombo vya sheria visiache kuwapa haki zao hao watuhumiwa. Naishiwa na maneno kwa hasira naona niishie hapa.
ReplyDelete