Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba
Na Gideon Mwakanosya,Nyasa
WANANCHI wa vijiji vya Mwelampya, Mkaya, Ngingama, Kihulu na Litui Wilayani nyasa Mkoa Ruvuma na wananchi wa vijiji vya kipingu, ngelenge, msungu na mbongo Wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa wameilalamikia serikali kupitia wizara ya ujenzi hapa nchini kwa kuchukua uamuzi wa kuing’oa injini 1 kati ya injini 2 zilizokuwa zikitumika kwenye pantoni ambayo ilikuwa ikiwasaidia wananchi wa vijiji hivyo kuvuka kwenye mto Ruhuhu na kuiamishia kwenye pantoni iliyoko mto Ifakara Kilombelo Mkoani Morogoro
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao wa www.stephano,mango.blogspot.com huko katika kijiji cha Lituhi wameonesha kusikitishwa kwa kiasi kikubwa pale Meneja wa wakala wa ufundi na umeme Mkoani Ruvuma (TEMESA) pamoja na timu yake kufika ghafla kwenye kijiji hicho na kwenda kuingoa injini moja iliyokuwa ikitumika kwenye pantoni iliyoko mto Ruhuhu ambayo kwa sasa imesimamishwa .
Benadi Komba mkazi wa kijiji cha Lituhi ameelaza kuwa kwa muda mrefu wananchi wavijiji vilivopo kandokando ya ziwa nyasa walikuwa na kero kubwa ya usafiri kwenye ziwa nyasa pamoja na kivuko cha mto Ruhuhu ambako kwa miaka iliyopita wananchi wa vijiji hivyo walikuwa wakivuka mto Ruhuhu kwa kutumia mitumbwi huku wakiofia maisha yao na wengine kupoteza maisha.
Amesema kuwa kufuatia kilio hicho walichokuwa nacho kwa muda mrefu kupita kwa Mbunge wa jimbo la mbinga magharibi Kapteni mstaafu John Komba serikali ilisikia kilio hicho kisha ilileta pantoni ambayo imekuwa ikiwasaidia kuvuka mto huo kwa urahisi zaidi lakini ameshangazwa na kitendo cha wakala wa ufundi wa umeme Mkoni Ruvuma (TEMESA) kufika Lituhi na kuingoa injini iliyokuwa kwenya pantoni ambayo ilikuwa ikiwasaidia kwa urahisi kutoka Lituhi kwenda vijiji vya ngerenge, Ilele, Msungu, Mbongo na Kipingu Wilayani Ludewa Mkoani Iringa ambako kunahuduma muhimu za kilimo na biashara.
Sebasiani Inju mkazi wa kijiji cha kihuru ameiomba serikali kupitia wizara ya ujenzi kuchukua hatua za haraka kuirudisha injini hiyo iliyochukuliwa kwenye pantoni iliyoko kwenye mto Ruhuhu kwa madai kuwa imepelekwa Ifakara, Kilombelo Mkoani Morogoro ambako injini 1 ya pantoni ilikuwa imeharibika.
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kijiji cha Lituhi Joseph Chawala amesema kuwa kwa muda mrefu kanisa katoliki Jimbo la Mbinga limekuwa likitoa huduma ya afya nzuri kwa wakazi wa vijiji vilivyo kandokando ya ziwa nyasa kupitia kituo chake cha afya ambacho kipo lituhi ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma na wilaya ya Rudewa Mkoani Iringa ambapo alihoji ni kwanini serikali ilishindwa kutambua umuhimu wa maeneo hayo kwani kuna wananchi wengine kutoka wilaya wanapoumwa wanakuja kupata matibabu lituhi kupitia kivuko cha pantoni iliyoko mto ruhuhu .
Naye Gaitani Ngatunga mkazi wa kijiji cha kipingu wilayani Rudewa ameeleza kuwa wananchi wa vijiji vya ngerere,ilela isungu na mbongo walikuwa wakitegemea kwa kiasi kikubwa kwenda wilayani nyasa kupata huduma ya matibabu pale wanapoumwa hasa ikizingatiwa maeneo ya kandokando ya ziwa nyasa wanasumbuliwa sana na homa ya Malaria .
Ngatunga amemwomba mbunge wa jimbo la Rudewa Deo Filikunjombe na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba kuchukua hatua za haraka za kuishawishi Wizara ya ujenzi kurudisha injini hiyo
Mbunge wa jimbo magharibi keptani mstaafu komba ameiambia nipashe kuwa ofisi yake imepokea malalamiko kwamba TEMESA Ruvuma wamengoa injini 1 iliyopo mto ruhuhu na kuipeleka Ifakara kilombelo ambako kuna pantoni inayowasaidia wananchi kama pantoni inavyowasaidia wilaya ya nyasa na Ludewa jambo ambalo limeñaza kuleta hofu kunbe wananchi wa jimbo lake pamoja na wananchi wa Ludewa sio wananchi wa Tanzania.
Akizungumzia hilo Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba alisema ameshangwazwa sana na kitendo cha TEMESA Ruvuma cha kuondoa injini 1 kwenye pantoni iliyokuwa inawasaidia wapiga kura wangu kwenda Rudewa kwa shughuri zao kwa kufika Lituhi kwa kutumia pantoni iliyopo mto Ruhuhu kuja kupata mahitaji yao na wengine kuja kupata matibabu ya afya katika kituo cha Lituhi
Ameeleza zaidi kuwa kero hiyo ya kuondolewa injini kwenye pantoni mto Ruhuhu iliyokuwa ikiwasaidi wapiga kura wake anatarajia kuifikisha kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kinachotarajia kufanyika mapema januari mwaka ujao, kwani kitendo cha TEMESA kuamisha injini kwenye pantoni mto Ruhuhu na kuipeleka kwenye pantoni nyingine iliyopo Ifakara Kilombelo ni usaliti mkubwa na imeonekana kuwa na lengo baya kwa wananchi wa mwambao mwa Ziwa Nyasa
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com ofisini kwake Meneja wa wakala wa ufundi na umeme Mkoa Ruvuma (TEMESA) Mhandisi Afred Ngwani amesema kuwa agizo la kuiondoa injini hiyo kwenye pantoni iliyoko mto Ruhuhu lilikuwa limetoka kwa Katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Bw. Mlango ambaye alimwagiza aiondoe haraka iwezekanavyo baada ya kuona pantoni iliyoko mto Ruhuhu imesimama kutokana na kina cha maji kupungua na kujaa mchanga .
Mhandisi Ngwani amesema sababu kubwa ya kuhamisha injini hiyo kwenye kivuko cha mto Ruhuhu kwenda kwenye pantoni ya kivuko cha Ifakara kilombelo kiliharibika na kushindwa kuvuka mto huo ambacho kinadaiwa kuwa kina umuhimu mkubwa huko kwani kinawavusha watu zaidi ya 1000 kwa kila siku na Magari kati ya 200 hadi 400 kwa siku tofauti na kivuko cha mto Ruhuhu ambacho kilikuwa kinawavusha watu wachache na Magari kati ya 4 hadi 6 kwa wiki.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment