About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, December 21, 2011

VETA SONGEA YATOA MAFUNZO KWA MADEREVA WA PIKIPIKI 106



Na Gideon Mwakanosya, Songea

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewahimiza vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha nne Mkoani humo ambao wameshindwa kupata nafasi ya kuendelea na masomo  ya elimu ya kidato cha tano waone umuhimu wa kujiunga na mafunzo ya elimu ya ufundi stadi yanayoendeshwa na VETA SONGEA ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na tatizo la ajira lililopo hapa nchini.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkao wa Ruvuma Said Mwambungu wakati wa maafari ya nne ya wanafunzi walio hitimu mafunzo ya udereva wa magari ya abilia yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA MJINI SONGEA).

Alisema kuwa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA SONGEA yameonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutoka wilaya za Mbinga, Tunduru, Namtumbo na Songea ambao wengi wao baada ya kuhitimu kozi walizosomea wameweza kupata ajira na wengine wamejiajili wao wenyewe.

Amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo serikali Mkoani humo inaendelea kuwahimiza wazazi wa watoto waliomaliza sekondari ambao wameshindwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano wawapeleke VETA ambako wataweza kupatiwa elimu ya ufundi stadi ambayo wakihitimu na kufahulu vizuri wataweza kuajiriwa serikalini, kwenye makampuni ya watu binafsi na wengine wataweza kujiajiri wao wenyewe badala ya kuwaacha waendelee kulandalanda mitaani ambako wanaweza kujifunza mambo mabaya.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha elimu na ufundi stadi (VETA SONGEA) Gideon Ole Lairumbe  alisema kuwa VETA SONGEA ni chuo cha mafunzo stadi ambacho kinatoa huduma Mkoani Ruvuma ambacho ni moja wapo ya vyuo vilivyopo chini ya mamlaka ya elimu na mafunzo stadi(VETA).

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo chuo chake kimeendesha mafunzo ya ufundi stadi kwa kozi mbalimbali ambapo alizitaja kuwa ni udereva wa magari wa madaraja yote, udereva wa pikipiki, saluni, kompyuta, uhazili, ufundi wakutengeneza kompyuta, umeme jua, umeme wa majumbani na ufundi wa magari.

Alibainisha zaidi kuawa kwenye maafari ya 4 ambayo wahitimu 106 wamepata vyeti ni wale waliokuwa wanajifunza udereva wa magari ya abilia ambao waliotokea  wilaya za Tunduru, Mbinga, Namtumbo na Songea ambapo alidai kuwa kwakuwa serikali ina mpango wa kubadirisha leseni za magari ya kubeba abilia VETA SONGEA tayari imetoa mafunzo yakinifu ya udereva wa magari makubwa yakiwemo ya kubeba abilia.

Ole Lairumbe alieleza kuwa pia VETA SONGEA imekuwa ikifanya kazi yakutoa mafunzo ya udereva wa magari na pikipiki kwa kushirikiana na taasisi zote ambazo kwa njia moja au nyingine zina uhusiano na fani hiyo kama vile Polisi, Sumatra, Takukuru, Kikosi cha zima moto na Bima.

Aliongeza kuwa kila mwezi kunakuwa na wahitimu takribani 40 ambo ni wa kozi wa kuendesha udereva wa pikipiki ambapo kwa wilaya ya mbinga VETA SONGEA inaendesha mafunzo ya udereva wa pikipiki kwa kushirikiana na chuo cha maendeleo ya wananchi mbinga (FDC) ambako novemba mwaka huu wanafunzi 56 wamehitimu mafunzo ya kozi ya kuendesha pikipiki na kwa wilaya ya Tunduru VETA SONGEA imekuwa ikiendesha mafunzo kwa kushirikiana idara ya ujenzi ambako wanafunzi 23 walikuwa wanachukua mafunzo ya udereva wa magari madogo na wanafunzi 45 walikuwa wanajifunza uendeshaji pikipiki.

Mkuu huyo wa Chuo cha VETA SONGEA Ole Lairumbe alisema  baada ya serikali kuruhusu pikipiki kutumika kama chombo cha usafiri wa kubebea abilia  jamii hapa nchini imeshuhudia ongezeko la ajali nyingi barabarani jambo ambalo limekuawa likisababisha hasara kubwa kwa serikali kwa kuwahudumia waathirika wa ajari zinazotokana na uendeshaji mbaya wa pikipiki hivyo kutokana na hali hiyo ndiyo maana chuo chake kimejikita kutoa mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki.

Na kwamba VETA inaendelea kuwahamasisha wakazi wa maeneo mbalimbali Mkoani humo wakiwemo wa vijiji vya Lituhi, Mbambabay na Kindimba juu amboko VETA imefungua madarasa ya kozi ya kuendesha pikipiki waone umuhimu wa kujifunza sheria za usalama barabarani na namna ya kumudu usukani kuliko kuendesha pikipiki bila ya kuwa na mafunzo ya aina yeyote jambo ambalo linaweza kusababisha ajali mara kwa mara.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment