About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, December 27, 2011

MUUGUZI WA KIJIJI CHA MANGO AJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI

                                              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya ,Songea
MUUGUZI wa Zahanati ya kijiji cha Mango kilichopo kata ya Kihagara wilayani Mbinga Bosco Nchimbi (29) amekutwa  kwenye kenchi ya chumba chake akiwa amekufa baada ya kujinyonga  kwa kujitundika  juu ya kenchi kwa kutumia kamba ya katani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi jioni  huko katika kijiji cha Mango , ambapo katekista wa kijiji cha Tumbi  Joseph Nchimbi ndiye aliyegundua   kuwepo kwa tukio la kujinyonga Nchimbi .
Amefafanua kuwa, Inadaiwa siku ya tukio kateksta Nchimbi alikuwa ameenda nyumbani kwa Marehemu  kwa ajili ya kumpa ushauri  baada ya kuwepo malumbano  kati yake na Mwanamke aliyezaa naye mtoto  anayedaiwa kuwa alikuwa akilalamikiwa kuwa ameanza kufanya ngono na wanaume wengine wakati mtoto wao bado ni mchanga.
Kamanda alieleza zaidi kuwa Katekista Nchimbi  baada ya kugundua  tukio hilo  alitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mango  ambao nao ulitoa taarifa polisi  na askari polisi walipofika katika eneo la tukio wakiwa wameongoozana na Mganga walikuta mwili wa marehemu  ukiwa unaninginia  .
Kamanda amesema,chanzo cha kujinyonga ni wivu wa mapenzi   kati yake na mwanamke aliyezaa naye ambaye wakati wote alikuwa akimuonya kuacha tabia ya kufanya mapenzi na wanaume ovyo kwani anamuaharibu mtoto  wao mchanga lakini mwanamke huyo aliendelea hali iliyosababisha apandwe na hasira na kuchukua huamuzi huo.
MWISHO.

No comments:

Post a Comment